Msanii Yesaya Ambilikile a.k.a YP aliye katikati ya Chege Chigunda kushoto na Mheshimiwa Temba kulia.
Hapa Yesaya Ambilikile anaonekana akiwa amesimama Kulia Kwa Stuko na Dogo Asley, na Waliokaa chini ni Said Fela a.k.a Mkubwa Fela(Meneja wa Kundi hilo) na Mheshimiwa Temba.
Aliyewahi kuwa msanii wa
kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile"YP"alifariki dunia
usiku wa kuamkia jana(21-10-2014, Jumanne) katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda
mrefu na ugonjwa wa kifua.
Utakapo taka kumtaja au kumkubuka YP ni lazima utamkumbuka au kumtaja Msanii
Y-Dash kwakuwa wawili hao walikuwa Wanaume Famili kabla ya kutoka kwa
madai kuwa hawapati maslahi yao wakiwa ndani ya kundi hilo na kuamua
kuunda kundi lao ambalo lilijulikana kwa jina la majina yao ambalo ni 'YP NA Y-DASH'.
Kabla ya kuondoka Wanaume family YP anakumbukwa zaidi pale aliposhiriki vizuri kwenye Wimbo wa Chege Dar mpaka Moro,
Kabla ya kuondoka Wanaume family YP anakumbukwa zaidi pale aliposhiriki vizuri kwenye Wimbo wa Chege Dar mpaka Moro,
Wasanii hawa walitoka baada ya msanii nguli wa Temeke Juma Kassim Kiroboto a.k.a JumaNature kujitoa ndani ya kundi hilo kwa madai kuwa kuna wasanii wengi ndani ya kundi hawapewi nafasi na hivyo hali hiyo inaweza kusababisha kuuwa vipaji vyao, ndipo akajitoa na kwenda kuunda Wanaume Halisi akiwa na Dolo. Na wakafanikiwa kurekodi wimbo wao wa Kwanza ujulikanao kama NDEGE TUNDUNI.
Akizungumza
na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo Said Fela, amethibitisha kutokea kwa msiba
huo. “Mpaka
sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunamsubiri kaka yake kwa sababu
huyo mtu kafariki usiku hospitali.
Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndiyo
watasema tunazike vipi, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa saba
mchana ratiba itakuwa tayari,” alisema Fela.
“Tatizo
alikuwa anaumwa kifua muda mrefu, lakini alishaanza kunywa dozi na juzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu akamchukua.
wazazi wake yaani Baba na Mama walifariki ila ndugu zake wapo keko, na kuna kibanda
waliachiwa na wazazi wao, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”