Kuanzia juzi longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika utakuwa unaongopa mchana kweupe.
Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa
Tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa
Tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea maelezo ya kina ya ujumbe huo (Pressing and holding an individual message shows the Message Info option) Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa
Whatsapp haijatoa sababu za kufanya mabadiliko hayo ambayo yamewakera baadhi ya watumiaji.
Kuanzia juzi huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook- itakuwa ikionesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao.mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.