Facebook Comments Box

Thursday, April 10, 2014

HABARI YA KIUNGO WA ARSENAL ALIE JIUNGA NA JIHAD


Kiungo wa zamani wa Arsenal na Real Madrid
anayekipiga katika klabu ya Lokomotiv Moscow
Lassana Diarra amekanusha madai kwamba ni
mfuasi wa vita ya kidini nchini Syria.
Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Diarra (29)
alijiunga na vita inayoendelea Syria baada ya
kutolewa kwa video inayomuonyesha mtu akiwa
kajifunika uso huku akijitambulisha kwamba ni
Lassana Diarra.
Hata hivyo kiungo huyu wa timu ya taifa ya
Ufaransa ambae aliwahi pia kuitumikia
Portsmouth na Chelsea, ametoa taarifa rasmi
kupitia wakili wake na kusema hahusiki kabisa
na hiyo video.
“Hajawahi kukanyaga nchini Syria, yeye ni mwanasoka
anayeichezea Lokomotiv Moscow,” amesema
Mwanasheria wake.


WATOTO WA TANZANIA WALIOSHINDA KOMBE LA DUNIA WAWASILI NCHINI

''Tunaipongeza timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kuchukua ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani majuzi (Aprili 6
mwaka huu) baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali
uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Ushindi kwa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa
kituo cha Mwanza ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na
wadhamini na wafadhili walioiwezesha kushiriki fainali hizo kwa
mara ya pili mfululizo.
Vilevile ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa
mpira wa miguu kuwa watoto wa mitaani ni sehemu tu ya vipaji
vilivyotapaa nchini, hivyo iliyopo ni kuvisaka na kuvibaini vipaji
hivyo kwa ajili ya ustawi wa mchezo huo nchini.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tutaendelea
kushirikiana na kituo hicho cha Mwanza, na vingine vyote ambavyo
vinajishughulisha na mchezo huu, lengo likiwa ni kuundeleza na
hata kutoa ajira kwa vijana hapo baadaye kupitia mpira wa miguu.
Timu hiyo imerejea nchini leo ambapo imetua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 na nusu jioni kwa ndege
ya Emirates''
Viongozi wa watoto wa mitaani wakiwasili na vikombe walivyo nyakua huko Brazili 


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU