Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetangaza rasmi kuanza kwa zoezi la kupiga kura ya NDIYO juu ya uundwaji wa kampuni au kura ya HAPANA kwa kutoridhia klabu kuwa kampuni maazimio yaliyofikiwa katika mkutano mkuu uliofanyika Januari 16, 2013.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga kaimu katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema zoezi hilo linanza leo kwa wanachama hai kufika makao makuu ya klabu na kupiga kura ya NDIYO au HAPANA na zoezi hilo litaendelea mpaka novemba 10, 2013.
Ifuatayo ni Taarifa kwa Wanachama na Waandishi wa Habari
MAONI YA WANACHAMA YA KUUNDA KAMPUNI
Katika Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 16 Januari 2013 Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama wafikirie mapendekezo ya YANGA kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa YANGA.
Nachukua nafasi hii kuwaambia Wanachama wa YANGA kuwa kuanzia leo tarehe 16 Oktoba 2013 mpaka tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja (1) hapa Klabuni kwa ajili ya kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni (HAPANA)
Kila Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.
Zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya YANGA.
“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
LAWRENCE MWALUSAKO