Facebook Comments Box

Thursday, August 15, 2013

VIDEO: KAMA ZAMANI - MWANA FA

kam





MKURUGENZI WA CRDB KORTINI KWA TUHUMA ZA KUDHALILISHA KIJINSIA

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro, Francis Mollel jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kwa tuhuma za kumdhalilisha kijinsia mteja ndani ya benki hiyo, Lulu Kajembe.

Mwendesha mashitaka, wakili wa serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Swai alieleza kwamba Lulu aliwahi kufanya kazi kwenye benki hiyo na kwamba siku ya tukio Juni 1, 2013, mlalamikaji alikuwa kwenye foleni akisubiri kuhudumiwa ndani ya benki hiyo na ndipo mshitakiwa alimtolea maneno ya udhalilishaji wa kijinsia.

Hata hivyo, mshitakiwa anayetetewa na wakili Kitomo, alikana kosa na mahakama hiyo kumpa dhamana ya shilingi milioni moja na wadhamini wawili wanaotambulika. Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana ambapo amezuiwa kusafiri nje ya mkoa na kuwasilisha stakabadhi zote za kusafiria.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 21 itakapotajwa. --- (TANZANIA DAIMA)


MUUAJI WA BILIONEA WA ARUSHA AKAMATWA

 
Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya. 
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.
“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.
Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.
Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio kisha zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.
Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri ingawa jina lake halijatajwa.
   


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU