Facebook Comments Box

Friday, August 30, 2013

MASAA NANE YATUMIKA KUTENGANISHA MAPACHA MUHIMBILI

karima_98974.jpg
Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.
 
Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.
 
Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).
 
Akizungumza baada ya upasuaji huo, Dk Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye hakuwa amekamilika na kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia mbali kutokuwa na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila alikuwa na uti wa mgongo.
 
"Uti wa mgongo ulikuwepo na ndio uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha mguu."
 
Alisema kinachoratibiwa kwa sasa ni kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye anaendelea kupumua na kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea mtoto huyo itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.
Upasuaji
 
Kazi ya upasuaji huo ilianza saa mbili asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike aliyetimia kuchukuliwa vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na vingine vingi kabla ya upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.
 
Dk Shaaban alisema ni mara ya kwanza kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya folic acid.
 
Kabla ya upasuaji kuanza, mama wa mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa kufanya maombi maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari kuendelea na upasuaji huo.
 
Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: "Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu."Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya Jang'ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.


PICHA: DIAMOND AZINDUA VIDEO YAKE NA KUMPA MZEE GURUMO GARI


1

Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni arobaini za Tanzania, Video hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu na watu maarufu mbalimbali

2

Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo
3

Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari
6

Diamond akimuonesha Mzee Gurumo gari
7

Diamond akizungumza machache kushukuru mashabiki wake na watu mbalimbali waliomsaidia kufikia hapo alipo
  5  
9

Diamond na madansa wake wakitumbuiza katika hafla hiyo
10

Wasanii mbalimbali pamoja na MaDJ walikuwepo katika hafla hiyo hapa ni Dully Sykes na MawanaFA wakiwa na baadhi ya MaDJ
11

Maurice Njowoka kutoka Cocacola wa pili kutoka kushoto na Mwanamuziki AY wa tatu kutoka kushoto pamoja na wadau wengine
12

Mwigizaji Jaquiline Wolper naye alitia timu
     
13

Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond
15

Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo
17

Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari
18

Hawa marafiki zangu wakakumbushia miaka kadhaa waliyofunga ndoa kwa kulishana mishikaki ilipendeza katikati ni Nancy Sumari akishuhudia
19

Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi
20

Kushoto AY na Salama Jabir wakipiga story na wadau mbalimbali
22

Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa katika hafla hiyo.
  16  
21 



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU