Facebook Comments Box

Wednesday, April 17, 2013

HII NDIO SABABU YA KIFO CHA BI KIDUDE

Kidude
Mjukuu wake aitwaye Omar ameiambia Bongo5 kwa simu muda mfupi uliopita kuwa Bi. Kidude alikuwa amelazwa kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe kwenye kongosho.
“Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu akachukua roho yake,” amesema Omar.
 Omar amesema mazishi yanaweza kufanyika kesho. Mungu ailaze roho ya marehemu Fatuma binti Baraka mahala pema peponi. Amen.





HEBU SIKILIZA TUSI ALILOTUKANA HUYU MBUNGE LEO BUNGENI

Bunge letu linaelekea wapi? hebu sikiliza hili tusi alilotoa huyu mbunge leo ndani ya bunge.







KIBONZO: KIPANYA AKIZUNGUMZIA MATUSI WANAYOTUKANANA WABUNGE NDANI YA BUNGE




BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia hivi punde amefariki dunia. Habari hizo zimepatikana kutoka moja ya Tv kubwa ya burudani Afrika Mashariki na kuenezwa vile vile na watu mbali mbali mashuhuri kama tulivyo ziweka hapo chini.Inna Lillah wa Inna Illayhi Rajiuun. 



DR BILAL AFUNGUA RASMI MKUTANO WA WANASAYANSI WA AFRIKA


Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali akifungua rasmi Mkutano wa Pamoja wa Kimataifa wa Watafiti Wanasayasi Afrika ulioandalia na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS) ya Afrika Kusini. Kushotoni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela. Mkutano huo wa siku nne unafanyika Jijini Arusha. 

Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na Dk Martha Lemnge mara baada ya kuwakabidhi tuzo zao hii leo. 

Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na Dk Martha Lemnge mara baada ya kuwakabidhi tuzo zao hii leo. Kulia ni Mkurugenzi wa NIMR, Dk Mwele Malecela. 


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu TanzaniaNIMR), Dk Mwele Malecela akisoma hotuba yake.





Badhi ya Watafiti Wanasayansi kutoka Taasisi zaidi ya 35 barani Afrika wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa NIMR wakati wa hotuba yake ya ukaribisho. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS), Mark Rweyemamu akisoma risala yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Jijini Arusha. 

Viongozi wa NIMR na Watafiti mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa SACIDS. 

Mkurugenzi wa OHCEA, Japhet Kilewo akitoa hotuba yake. 

Meza kuu ikifuatilia kwa ukaribu Hotuba ya Mkurugenzi wa OHCEA. 

Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dk Ahmed Hamdy akizungumza na Wanasayansi watafiti. 

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid nae alisoma Hotuba ya Wizara na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo. 



Wakuu wa Taasisi za kitaifa na Kimataifa pamoja na wanasayansi watafiti wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.



Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela wakizindua rasmi awamu ya nne ya Vipaumbele vya Tafiti za Afya kwa mwaka 2013-2018.


Pia Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzindua Mpango wa Afya Moja nchini Tanzania 

Aidha Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal pia alizindua Mpango wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS).


WABUNGE WANNE WAFUKUZWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

Chama tawala nchini Uganda cha National Resisitance Movement-NRM- kimewafukuza baadhi ya wanachama wake wanne, wote wakiwa ni wabunge, kwa kile kilichoitwa utovu wa nidhamu.

Mbunge mwingine yeye amesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu kwa sababu za ulevi.

Katibu mkuu wa chama hicho Amama Mbabazi anasema hii kwa tafsiri yake inamaanisha kuwa wabunge hao wamepoteza viti vyao, jambo ambalo wahusika wanapinga.

Katibu mkuu wa chama tawala cha NRM na wakati huo waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi, ametangaza maamuuzi ya kamati kuu ya chama hicho kuhusu majaliwa ya wabunge wanne waliopewa jina la ‘wabunge waasi’ kutokana na misimamo yao dhidi ya masuala mbalimbali katika chama hicho.

Mbabazi alitoa kauli hiyo na kusema, “Muhammad Nsereko afukuzwe kutoka NRM;kuwa Theodor Sekikubo afukuzwe kutoka NRM; kuwa Barnabas Tinkasimire afukuzwe kutoka NRM; kuwa Wilfred Nuwagaba wamefukuzwe kutoka NRM; na kuwa Vicent Kyamadidi Muzuni asimamishwe uana chama wa NRM kwa muda wa miezi mitatu.”

Wabunge wanne waliofukuzwa kutoka chama: Nsereko; Sekikubo; Tinkasimire pamoja na Niwagaba wamekuwa wakipinga na kukosoa saana uongozi wa sasa wa chama hususan kutokana na madai ya ufisadi dhidi ya vigogo wa chama.

Na wanasema hatua hii ni ya kuwaandama kisiasa kwa kusema ukweli dhidi ya wanachoita uongozi mbaya. Hatua ya kuwafukuza wanachama hao , inasekena ni kutokana na utovu wa nidhamu.

Wabunge hao walishtakiwa katika kamati ya nidhamu ya chama na kukabiliwa mashataka saba: kuwapigia debe wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mdogo; kupaka matope wagombea rasmi wa chama cha NRM wakati wa uchaguzi mdogo; kutoa madai ya uongo kwa vombo vya habari dhidi ya chama cha NRM; kutumia majukwaa haramu, kama vile vyombo vya habari na mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kuzungumzia masuala yanayowakera;kujihusisha katika uundaji wa genge ndani mwa NRM; matumizi ya lugha chafu;na mwisho kukaidi kamati ya nidhamu ya chama.Wote licha ya kuwaita kufika mbele ya kamati hiyo kujieleza walipinga.

Hii ndiyo mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi kuanza tena mwaka wa 2006, chama cha NRM kufukuza wanachama wake.

Na hii imezusha tafsiri tofauti kwa wabunge wanaofukuzwa chama.Katibu mkuu wa NRM anasema kuwa hii inamaanisha kuwa wamepoteza viti vyao vya ubunge.

Mbabazi aliongeza kusema kuwa ''Kulingana na sheria za Uganda, hususan kifungu 83 cha katiba ya taifa ni kuwa mtu anaweza kuwa mbunge pindi tu ikiwa amechaguliwa kama mbunge wa kujitegemea,au ikiwa amechaguliwa baada ya kuungwa mkono na chama Fulani,au ni waziri,au kama mwanajeshi.''

Hakuna njia nyingje ile. Wabunge hao wanasema kuwa katiba haikubali mbunge yeyote kubadili chama bungeni.Ikiwa mtu atapoteza uungwaji mkono wa chama chake hii ina maana kuwa amepoteza kiti chake.

Lakini hilo limepingwa na mbunge muathiriwa na tena wakili, Wilfred Niwagaba.

Niwagaba alisema ''Ikiwa anadhani kwa kutusimamisha au kutufukuza uanachama ina maana kuwa tunapoteza viti vyetu,nasikitika sikubaliani na tafsiri hiyo.Hakuna hata mmoja wetu ameondoka kutoka chama kwa hiari.''Hata hivyo mwenzao Vincent Kyamadidi amesimamishwa uanachama kwa muda kutokana na madai kuwa alilewa na kujaribu kupigana hadharani jambo ambalo linakwenda kinyume na maadili ya chama.

Aidha yeye alipoita kujieleza alifika mbele ya kamati hiyo.

Bado kuna vuta ni kuvute kuhusu majaliwa ya wabunge wanne, ikisemekana wamekwenda mahakani kupinga kufukuzwa kwao.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU