Facebook Comments Box

Friday, March 1, 2013

ANGALIA MAANDAMANO YA CHADEMA KWA PICHA KATIKA JIJI LA MBEYA
















POLISI MKOA WA KINONDONI YAKAMATA MAJAMBAZI NA SILAHA


Baadhi ya silaha zilizokamatwa klatika msako na Polisi Mkoa wa Kinondoni zikiwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akionesha bastola zilizokamatwa na Polisi wakati wa msako wa majambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akionesha nondo zilizokamatwa wakati wa msako huo.


MNYIKA: NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAO WA UMEME


Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema Mh John Mnyika-
---
Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012. 

Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme. 

Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo. 

Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.


Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012. 

Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika. 


Wenu katika uwakilishi wa wananchi, 

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini 

27 Februari 2013
CHANZO CHA HABARI HII: www.dj-sek.blogspot.com


SIRI YA MTUNGI; SEHEMU YA SABA (EPISODE 7)




POLISI WANATUHUMIWA KUMPIGA RISASI MWALIMU HUYU


PictureMwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari Kitulo wilayani Makete aliyefahamika kwa jina la Casto Sote Kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi, Makete

Mkuu wa polisi wa wilaya ya Makete, SP Peter Kaiza akizungumza na FrancisGodwin blog kuhusu tukio hilo lililotokea katika eneo la benki ya NMB tawi la Makete juzi majira ya saa moja na robo alisema  kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya  kutolea  pesa ya ATM akiwa na pikipiki, na kuamriwa na askari mmoja aitwaye Jose Msukuma, kuvaa kofia.

Inadaiwa  kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai ya kutokuvaa kofia na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindoni.

Hata  hivyo  mmoja kati ya  askari ambaye   jina lake halikufahamika mara  moja alisikika  akidai kuwa  chanzo cha mtu huyo kupigwa  risasi  ilikuwa akihisiwa  kuwa ni jambazi baada ya  kufika kwa usafiri wa pikipiki (bodaboda) na kuhisiwa kuwa amefika  kwa ajili ya kuora katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya  kujihami alimpiga risasi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete, Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao Mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea.

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.
kwa habari zaidi na picha ingia FrancisGodwin blog


RUFAA YA JOHN MNYIKA DHIDI YA UENDESHAJI MBOVU WA BUNGE WA JOB NDUGAI

RUFAA DHIDI YA UENDESHAJI WA BUNGE USIOKUWA WA HAKI NA UKIUKAJI WA KANUNI WA NAIBU SPIKA JOB NDUGAI KATIKA KUONDOA HOJA BINAFSI YA MAJI

Tarehe 28 Februari 2013 nimewasilisha rasmi rufaa kwa mujibu wa Kanuni ya 5 (4) dhidi ya uendeshaji wa Bunge usiokuwa wa haki wa Naibu Spika Job Ndugai kwa kukiuka kanuni ya 58 (5) kwa kulihoji bunge kinyume na kanuni kufanya uamuzi badili wa kuondoa hoja binafsi kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es salaam.

Nimefanya hivyo baada ya kupata kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) za kikao cha tano cha tarehe 4 Februari 2013 cha mkutano wa kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Mkutano huo Naibu Spika Job Ndugai alisema na kufanya maamuzi kwamba: “Sasa ninahoji wanaoafiki kwamba hoja hii iondolewe waseme ndiyo…..hoja imeondolewa. Walioafiki Wameshinda”; wakati mtoa hoja sikuwa nimeomba idhini yoyote ya hoja yangu kuondolewa.

Maamuzi hayo ni kinyume na Kanuni ya 58 Fasili 5 ambayo inaelekeza kwamba “Endapo hoja imefikishwa Bungeni, mtoa hoja anaweza tu kuiondoa hoja yake kwa kusimama mahali pake na kusema ‘Ninaomba ruhusa kuondoa hoja’ na papo hapo Spika ataliuliza Bunge kama linaafiki hoja hiyo kuondolewa na inapotokea Wabunge walio wengi watakubali, Spika atasema ‘hoja hiyo inaondolewa kwa idhini ya Bunge’ na hoja hiyo itakuwa imeondolewa na Bunge litaendelea na shughuli inayofuata”.

Ushahidi wa Kumbukumbu Rasmi za Bunge (Hansard) za kikao tajwa unathibitisha ukiukwaji huo wa kanuni kama ifuatavyo:

“…WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuwa hoja iliyo mbele ya Bunge lako Tukufu ni kuitaka Serikali kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka Jijini Dar es Salaam, ambalo tayari linatekelezwa na mpango maalumu uliotengewa fedha nyingi na Serikali, hivyo naomba kutoa hoja kwamba hoja hii iondolewe. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja…

MBUNGE FULANI: Waziri amesema uongo, amedanganya!

NAIBU SPIKA: Sasa ninahoji wanaoafiki kwamba hoja hii iondolewe waseme ndiyo.

WABUNGE FULANI: Sasa utaihoji vipi wakati tuna majadiliano?

WABUNGE FULANI: Ndiyooooooooo!

NAIBU SPIKA: Wanaokataa waseme siyo.

WABUNGE FULANI: Siyooo!

NAIBU SPIKA: Hoja imeondolewa. Walioafiki wameshinda.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)
(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)
(Hoja Binafsi ya Mheshimiwa John Mnyika iliondolewa na Bunge)

MHE. TUNDU M. LISSU: Aaaaaa! Aaaaaaaaaaah! Aibu!

NAIBU SPIKA: Hoja imeondolewa na Bunge linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi…”

Hivyo, pamoja na kuwa Kanuni ya 8 inataka Spika kuendesha shughuli za Bunge na kutoa maamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba ya Nchi na Kanuni za Bunge, Naibu Spika wa Bunge alifanya maamuzi yenye kukiuka kanuni ya 58 Fasili ya 5 kwa kuruhusu hoja yangu kuondolewa kwa hoja iliyowasilishwa na Waziri wa Maji.

Kufuatia rufaa hii Spika atataarifiwa kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) na kuitisha kikao cha kamati ya kanuni kwa mujibu wa kanuni ya 5 (5) ya kanuni za Kudumu za Bunge na kulijulisha bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU