Facebook Comments Box

Thursday, April 24, 2014

MACHOZI YA SHEIKH HAMID JONGO BUNGENI.


Mashekh wa BAKWATA hakika wana mambo sana.Kuna kitu
kinaitwa ''theatrics,'' masheikh wa BAKWATA ni mabingwa na wana
medali za dhahabu. Sheikh Mkuu wa BAKWATA Shaaban
Simba aliwahi kutoa medali kumpa Reginald Mengi kwa utumishi
wake uliotukuka kwa Waislam. Hakika umma ulipigwa na butwaa.
Umma ukajiuliza. Sheikh Shaaban Simba hajapata kumsikia Sheikh
Hassan bin Amir bingwa wa tafsir ya Qur'an na bingwa wa lugha ya
Kiarabu aliyeandika vitabu lukuki mpaka akapewa shahada ya
heshima na Al Azhar, Cairo mwaka 1964?Ukiachia sifa yake ya
kupigania uhuru wa Tanganyika nk. nk.
Umma ulijiuliza Sheikh Shaaban Simba hajamsikia Sheikh Mohamed
Ayub aliyesomesha dini maisha yake yote na ana wanafunzi Afrika
ya Mashariki nzima na hao wote wanafunzi wake wana vyuo
wanaisomesha Qur'an? Sheikh Shaaban Simba hivi kweli hajapatapo
hata siku moja kumsikia Sheikh Aboud Maalim aliyejenga misikiti
chungu mzima kwa kuwahamasisha Waislam matajiri na masikini
wachangie ujenzi kila mtu kwa uwezo wake alojaaliwa na
Allah? Sheikh Aboud Maalim akaweza kujenga Msikiti wa Manyema,
Msikiti wa Ngazija, Msikiti wa Maamur, Msikiti wa Mwinjuma
Mwinyikambi na mingine tusiyoijua. Achilia mbali kuanzisha
scholarship kwa vijana wa Kiislam kusoma Udaktari na Uhandisi
Uturuki chini ya taasisi aliyoanzisha, Tanzania Muslim Trust Fund.
Sheikh Shaaban Simba hawa wote hakuwaona ila kamuona
Reginald Mengi?
Kwa wasiowajua masheikh wa BAKWATA hakika wanapata tabu.
Kwa wanowajua masheikh wa BAKWATA hawashangazwi.
Wakati mwingine hakika huwa vioja na vichekesho khasa mtu
unatamami kucheka lakini kinachokuzuia ni kuwa jambo lenyewe si
la kuchekesha.
Kuna msemo wa Kiarabu unaosema,''Sababu ikijulikana ajabu
huondoka.'' Naamini Sheikh Jongo anaujua msemo huu.
Sasa hili la kulia Sheikh Jongo ni mlolongo tu wa hizo ''theatrics'' za
masheikh wa BAKWATA.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU