Facebook Comments Box

Monday, August 18, 2014

ALLY KIBA AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA DIAMOND

Ally Kiba afunguka kuhusu bifu linalosemekana lipo kati yake na Diamond. Akiwa anahojiwa katika kipindi cha mkasi kinachorushwa na runinga ya EATV kila jumatatu saa tatu na nusu ya usiku Ally Kiba alisema japo hajawahi kuwa mshikaji na Diamond, anafurahishwa kwa kazi nzuri ambayo anaifanya. Lakini anakerwa kwa
namna ambavyo watu wanamfananisha na Diamond japokuwa hilo pia halimuumzi.

Haya ni maneno mazuri ya busara na kizalendo yalionesha ukomavu wake katika sanaa. Pia aliongeza kwa kumsifia kwa kupata tuzo marekani na kusema pale inatakiwa tuweke utanzania mbele.




HII NDIO RADIO ILIYO MCHUKUA MAULID KITENGE

Maulid Baraka Kitenge akiweka saini mkataba
Maulid Kitenge akipena mkono kwa furaha na mmoja wa viongozi wa Efm baada ya kusaini mkataba wa kutumikia kituo hicho cha radio kipya kinacho tingisha jiji la.Dar es Salaam na viunga vyake kwasasa.



UNAJUA TIMU KUBWA ZIMETUMIA KIASI GANI KWENYE USAJILI MPAKA SASA?

Chini ni jedwali la uanishi wa kiwango cha fedha kilicho tumika katika usajili katika majira ya joto ikaanza na timu iliyotumia hela nyingi zaidi mpaka ya chini kwa timu za ulaya.



MAHAKAMA YAMWACHIA MANSOUR HIMID KWA DHAMANA

Mahakama ya Mkoa,Vuga imempatia dhamana aliekuwa waziri wa zamani wa serikali ya Mapinduzi (SMZ),Mansour Yussuf Himid anaetuhumiwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria ya Zanzibar, baada ya kupata maelekezo kutoka Mahakama kuu.
Hakimu Khamis Ramdhani ametoa dhamana hiyo leo baada ya kutakiwa kusimamia maamuzi yakupatiwa dhamana yaliotolewa na Mahakama kuu chini ya Jaji Abraham Mwampashe kufuatia kusikilizwa kwa ombi la dhamana lililowasilishwa Mahakama hapo na mawakili
wanaomtetea Mh.Mansour.
Mapema Jaji Abraham Mwampashe, akitoa dhamani hiyo, amesema Mahakama yake imeangalia hoja za kisheria zilizotolewa na pande zote mbili za muombaji na mpigaji dhamana zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa pande zote mbili. Jaji mwampashe amesema kutokana na kifungu cha sheria cha (150) kifungu kidogo cha nne(4) sheria No (7 )ya mwaka (2004) sheria ya Zanzibar,kinaipa uwezo Mahakama kuu kutoa dhamana kwa mtuhumiwa ikiwa itaridhika na hoja zilizowasilishwa.
“hakuna kosa lolote lisolokua na dhamana,kifungu kidogo cha nne (4) kiko wazi kimeeleza Mahakama kuu ina uwezo wa kutengua makosa yote yaliokuwa hayana dhamana ikiwa itajiridhisha kama yalivyoorodhesha katika kifungu kidogo cha kwanza” Alisema Mwampashe.
Amesema baada ya kuangalia hoja za kisheria pia amechanganya na akili zake mwenyewe kwa kuangalia faida na hasra za mtuhumiwa kuwepo nje na kuwepo kizuizini. Amesema gharama za kumhudumia na kumleta Mahakamani mtuhumiwa kunaitia hasara jamii ,hivyo Mahakama hiyo haioni sababu ya mtuhumiwa kuendelea kubaki kizuizini. Mwampashe amesema hasa akiangalia mtuhumiwa hana historia ya uhalifu,pia mtuhumiwa anamajukumu ya kuendesha biashara zake ambazo kunafaida ya ajira kwa vijana walioajiriwa hapo katika vitega uchumi vyake.

Amesema Mahakama hii haiwezi kumyima mtu dhamana bila ya kuambiwa sababu ya msingi kuwepo kwake nje kuweza kuathiri mwenendo mzima wa kesi yake. Pia amefahamisha kwamba endapo Mahakama kuu itamnyima mtuhumiwa dhamana,huku kesi inaendelea na kufikia kufutwa au mtuhumiwa kushinda kesi, jamii inayomzunguka wataingia hasara ikiwemo kukosa huduma muhimu kutoka kwa ndugu
wanaemtegemea.
Aidha Jaji Mwampashe ametowa masharti ya dhamana kwa mtuhumiwa huyo kutoa dhamana ya shilingi milioni tatu tasilim za Tanzania, wadhamini wawili wanaoaminika kwa kusaini dhamana ya milioni tano za maandishi, kwa kila mmoja. Pia mtuhumiwa huyo alitakiwa kukabidhi Mahakamani hapo hati zake za kusafiria, pia hatoruhisiwa kutoka nje ya Nchi bila ya kuiarifu
Mhakama.
Wakati huo, huo Hakimu Khamis Ramadhani alihairisha kesi mama inayomkabili mtuhumiwa huyo hadi Agosti 28,mwaka huu na mtuhumiwa yuko nje baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana.


TRAFIKI APATA AJALI BAMAGA

Askari mmoja wa kikosi cha usalama barabara ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amenusurika kufa baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki ya polisi,ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajili T 681 CUX eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam.


MAULID KITENGE AACHANA NA ITV NA RADIO ONE


Maulid Baraka Kitenge

Mtangazaji maarufu wa michezo Maulid Baraka Kitenge ameacha kazi katika kampuni ya IPP Media wamiliki wa Radio One na ITV ambako alifanya kwa miaka 14 kama mwandishi zaidi ikiwa kama mhariri wa habari za michezo.

Katika barua hiyo mtangazaji huyo amelalamika ukuaji wa gharama za maisha hii ikionesha kiasi anacholipwa hapo hakikidhi ndio maana kaamua kuacha na kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine. Pamoja na hayo amerudisha sehemu ya mshahara wake kama sheria ya kazi isemavyo. 
Hii ni barua aliyo uandikia uongozi wa ITV na Radio One
Hii ni tweet yake baada ya kuwasilisha barua


TETESI:JAJI LEWIS MAKAME AFARIKI DUNIA

Kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kuwa aliekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Lewis Makame amefariki dunia katika hospital ya AMI masaki alipokuwa amelazwa.
Jaji Lewis Makame

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Lewis Makame aliyelazwa katika hospital ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es salaam



 CHANZO: JAMII FORUM


WAYAHUDI WAANDAMANA WAKIPINGA MYAHUDI KUOLEWA NA MUARABU

Maandamano ya kupinga ndoa ya myahudi na muarabu nchini Israel

Wayahudi wanne wenye msimamo mkali wamekamatwa nchini Israeli baada ya kuzua rabsha katika sherehe ya kuadhimisha harusi ya mwanamke myahudi aliyebadili dini na kuwa Muislamu na kisha kuolewa na mwanamume Mwarabu raiya wa Israeli. Mamia ya watu waliandamana nje ya ukumbi uliotumika kwa
sherehe hiyo katika mji wa Rishon LeZion Jumapili wakipinga ndoa hiyo licha ya kuwepo kwa maafisa wa Usalama. Bwana harusi, Mahmoud Mansour, alikuwa amechukua hati ya
mahakama ya kupinga kufanyika kwa maandamano ya kupinga nikah yake lakini maafisa wa usalama wakashindwa kuzima maandamano hayo.

Maandamano ya kupinga ndoa hiyo

Rais wa Israeli Reuven Rivlin amekashifu upinzani dhidi ya ndoa hiyo. Muungano wa wayahudi wenye msimamo mkali Jewish Lehava walipewa ruhusa ya kuandamana kupinga ndoa hiyo ilimradi tu wasikaribie chini ya mita 200 karibu na ukumbi wa sherehe hiyo. Kundi hilo linapinga ndoa kati ya Wayahudi na Waarabu.

Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi kwa kukiuka masharti yao kulingana na mtandao wa habari wa kiyahudi.Sadfa ni kuwa kundi lingine linalounga mkono ndoa kati ya Waarabu na Wayahudi lilifanya maandamano kuunga mkono ndoa hiyo na hivyo kuwalazimu maafisa wa usalama kufanya kazi ya ziada kuzuia makabiliano baina ya makundi hayo hasimu.

Polisi wakiwadhibiti waandamanaji

Bi Harusi Morel Malka, alikuwa amewaalika wageni 500 katika hafla hiyo. Bi Malka, 23, alikuwa amesilimu kabla ya sherehe hiyo kuambatana na desturi za kiislamu. "Kwa kweli tunaishi pamoja kwa amani na sielewi kwanini ndoa hii inawahusu watu." alisema bwana Mansour, 26. Rais Rivlin alifananisha maandamano hayo dhidi ya ndo hiyo na ''panya anayengata msingi wa unaoliunganisha taifa hilo la Israeli''.

 CHANZO: BBC SWAHILI


SHIBUDA AFICHUA SIRI ZA CHADEMA

SIKU moja baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu,Bw. John Shibuda kutangaza kuachia ngazi ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mbunge huyo ameibuka tena na kusema aliahidiwa kupewa helikopta mbili na uongozi wa chama hicho aweze kuzitumia katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 lakini hakupewa.

Alisema uongozi wa chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbrod Slaa, ulimwahidi kumpa helikopta hizo kwenye kampeni zake na kumpigia debe Katibu huyo aliyekuwa akiwania nafasi ya urais.
Bw. Shibuda aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Malampaka, wilayani Maswa na kuongeza kuwa, alijitolea kutumia pesa zake katika uchaguzi huo na kuahidiwa kurudishiwa lakini mpaka sasa bado kurudishwa. "Katika kampeni za mwaka 2010, mbali ya kuahidiwa helikopta, pia nilikuwa chanzo kikubwa cha Dkt. Slaa kupata kura nyingi kwa mara ya kwanza na kuongoza kwenye Wilaya ya Maswa akimzidi mgombea mwenzake kutoka CCM, Rais Jakaya Kikwete. "Helikopta nilizoahidiwa, hata wakati wa kampeni sikupewa,
nilipouliza niliambiwa nitapewa...mimi ndiye chanzo kikubwa cha Rais Kikwete kupata kura ndogo katika jimbo langu, nilitumia gharama zangu kumfanyia kampeni Dkt. Slaa," alisema.
Wakati huo huo, Bw. Shibuda alisema msimamo wake ni Serikali mbili na kusisitiza hawezi kuwaunga mkono wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao msimamo wao ni Serikali tatu ambazo zitawaongezea mzigo wananchi wangu ambao ni wakulima na wafugaji.

Bw. Shibuda alisema wananchi wake hawataki kuongezewa mzigo wa Serikali; bali wanataka kutatuliwa kero walizonazo hasa zinazohusu kilimo cha pamba, migogoro ya wakulima na wafugaji. "Siko tayari kuunga mkono muundo wa Serikali tatu kwa sababu wakulima wa pamba wana matatizo makubwa katika bei ya zao hili
na pembejeo, pia katika wilaya yangu kuna migogoro mikubwa ya wakulima na wafugaji inayopaswa kutatuliwa kwa serikali hii
tuliyonayo," alisema Bw. Shibuda.
 
Katika mkutano huo, Bw. Shibuda alikwenda mbali zaidi akimfananisha Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lissu na kundi la Interahamwe lililochochea ubaguzi wa kikabila uliosababisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda akidai mbunge huyo amekuwa mchochezi wa vita ndani na nje ya chama.
"Tundu Lissu ni Interahamwe kwani amekuwa mtu mchochezi mwenye tabia ya kuwatukana wenzake, hana tofauti na kundi hili kama wenzake walivyosababisha mauaji nchini Rwanda," alisema.


MARCO REUS NI CHAGUO SAHIHI KWA ARSENAL HII

Marco Reus
Kama watanzania wapenda Arsenal wanavyo ona kuwa winga ya kushoto na mshambuliaji imekuwa tatizo kidogo kwenye kikosi cha Arsenal. Sidhani kama Jack au Santi ndio jibu sahihi kwa hili ni kama Giroud ambavyo ameshindwa kukidhi haja pale mbele.
Ufumbuzi wa swala hili ni Marco Reus. Nadhani hamna haja ya kuwashawishi sana kuwa huyu ni chaguo sahihi bali naweza kuwaambia kuwa huyu ni mtu ambae anahitajika kwa muda huu pale Arsenal. Akisajiliwa kama winga wa kushoto nakuwa na uhakika wa makombe pale Emirate hebu angalia kidogo takwimu zake ana magoli 42, pasi za mwisho za magoli 39 katika mechi 94. Huyu ni winga mwenye uwezo wa kupenyeza kwenye msitu wa watu,kufunga na kupiga krosi ambazo kwasasa tunazikosa pale Arsenal hata ukiangalia mechi na Crystal Palace zilikosekana. Sio hayo bali huyu jamaa bi bingwa wa upigaji mipira iliyokufa.

Kila mtu anataka mshambuliaji bila kujua washambuliaji wapo ila inachotakiwa ni kuwaimarisha kwa kuwapa pasi na kutengeneza nafasi za kutosha kwa kumsajili Reus. Hebu fikiria pale mbele Reus, Sanchez na Walcott (wakibadilishana majukumu kulingana na kiwango cha timu) 

SASA TURUDI UPANDE WA UFUNDI:
Reus amekataa hela ambayo amepewa hii ni kutokana na yeye kuwa na soko kubwa. Kama £30/35 milioni zinaweza zikawashawishi Dortmund wakatuuzia mchezaji huyo na sidhani kama kuna mshabiki yoyote wa Arsenal atakaona ni hela nyingi kwa mchezaji huyu muhimu. Wakimuwekea mshahara wa £60,000, ukizingatia kwasasa tuna wajerumani pale Arsenal ambao watampa kampani ya kutosha na kumshawishi mchezaji huyu tunae Rosicky ambae ni gumzo la uingereza ambae Reus akiangalia uchezaji wake atavutiwa kucheza timu moja nae. Nafikiri huu ni muda wa kumpa Reus kiasi kikubwa tu ambacho klabu haijawahi kufikiria kwa wachezaji wa kiwango chake,tena sio klabu yetu tu tumpe kiasi ambacho hata Barcelona na Madrid wasingeweza kumpa nina uhakika ataturudishia zaidi ya hicho uwanjani.

Nafikiri hofu kubwa kwetu ni kuwa kwasasa imebaki usajili wa mchezaji mmoja, tunajiuliza amsajili winga wa kushoto,mshambuliaji au beki wa kati? Ni vizuri kujipa ujasiri kuwa tutampata Carvalho na sio Reus. Na tukimpata Carvalho nitajisikia vibaya kumkosa Reus.

Sisi ni Arsenal tunaojua biashara na najivunia kwa hilo maana biashara zetu zote huenda vizuri. Sisi sio Man City tunaotumia bila kujali kwa hiyo sidhani kama tunaweza kumpata winga mshambuliaji kwa £30 milioni na beki wa kati kwa £30 milioni, hapana sisi tunaangalia mbele zaidi hatujazi tu wachezaji.  Reus ndio mchezaji tunaemtaka kwasasa ili kuimarisha timu yetu.
Haya ni maoni yangu kama mpenda Arsenal kwa hiyo naomba nisihukumiwe,  Naipenda timu yangu na ninataka maoni yangu watu wayajue. 

Ahsanteni.
COYG!


MAGAZETI YA LEO: JUMATATU 18/08/2014

     






 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU