Facebook Comments Box

Friday, May 10, 2013

TAARIFA MPYA YA WIZARA YA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo.

Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba

KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10/05/2013


HII NDIO BARUA YA FIFA ILIYOMLETEA MATATIZO SHAFFIH DAUDA

Mtandao wa shaffihdauda umeripoti kwa kuiweka barua halisi ya FIFA kwa TFF. Kitu ambacho TFF wamemjia juu Shaffih Dauda na kumpa siku saba aeleze ameipata wapi barua hii ya kiofisi.

MGOMO WA DALADALA WAITIKISA IRINGA LEO

Huko mjini Iringa, daladala za Manispaa hiyo zimegoma kufanya biashara leo kutokana na  kile  wamiliki na madereva  wanachodai ni kuchoshwa na manyanyaso ya Afisa mpya wa SUMATRA wa mkoa wa Iringa.

Francis Godwin katika blog yake anasema kiini cha mgomo huo ni kinatokana na kuchukizwa na uamuzi  wa SUMATRA mkoa wa Iringa kufuta stendi ya Posta pamoja na kuzuia daladala kukaa kwa muda katika eneo la stendi ya daladala ya Miyomboni maeneo ambayo walikuwa wakikaa siku zote, hivyo, madereva  hao wamesema hawatafanya kazi hadi hapo SUMATRA Iringa itakapofuta maagizo yake hayo.
Picture
Picture
Picture



KIBONZO: ANGALIA WACHEZAJI WA MAN U WAKIMLILIA FERGUSON NA BABA WA MWAKA

Kibonzo cha picha kinaco onesha wachezaji waMan U wakimlilia SAF
Huyu amepewa tuzo ya ubaba wa mwaka


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU