Facebook Comments Box

Wednesday, August 29, 2012

MBUYU TWITE KUWASILI KESHO

Mchezaji alieleta mtafaruku mkubwa katika usajili wake atawasili kesho majira ya saa tisa alasiri. Msemaji wa Young Africans Sports Club Luis Sendeu ameomba washabiki na wapenzi waote wa yanga kujitokeza kumpokea mchezaji huyo. Sendeu pia amehabarisha kuwa suala la Mbuyu kukamatwa wao wanaona ni kama porojo tu.Wakati huo huo timu ya Young Africans Sports Club inatarajiwa kujitupa uwanjani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kupambana na Coast Union ya Tanga.
Mbuyu Twite akiitumikia Yanga huko Rwanda

Mbuyu Twite akisaini Yanga mbele ya Bin Kleb



AKUFFOR NA NGASSA WAING`ARISHA SIMBA ARUSHA

Daniel Akuffor akikabidhiwa jezi ya simba wakati wa usajili
Simba wameibuka kidedea baada ya kutoka kifua mbele kwa mabao mawili kwa moja. Mabao ya Simba yalifugwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ghana Daniel Akuffor na mshambuliaji aliehamia hapo ktoka Azam FC Mrisho Khalfan Ngassa. Goli la Ngassa lilifungwa kwa tictak.

BABA LEVO,LINEX NA SUMA LEE WAPATA AJALI KIGOMA

Wasanii wa bongo fleva Baba levo Linex na Suma lee wamepata ajali wakati wakielekea katika show yao kigoma. Ajali hiyo ilitokana na basi lililokuwa limepaki katikati ya barabara kwenye kona. Gari la wasanii hao lilikuwa linaendeshwa na Suma lee ambae ndio mmiliki wa gari hilo. mtu mmoja tu ambae ni dancer wa suma lee yeye ndio alie umia mguu tu. Suma lee alijaribu kulikwepa gari hilo ndipo akashindwa kulimudu gari vizuri kitu kilichosababisha kutoka nje ya barabara na kugonga mti. Linex anasema kitu kilichosababisha kusiwe na majeruhi ni mwendo ambao dereva alikuwa akiendesha ulikuwa sio mkali sana. Wasanii hao watakuwa na show kigoma Jumamosi na Jumapili baada ya hapo wataenda Bujumbura kwa shows mbalimbali.
Kitongoni tunawapa pole na safari njema
Linex

Baba Levo



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU