Facebook Comments Box

Wednesday, August 24, 2016

UVCCM WATARAJI KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI AGOSTI 31, 2016 KWA AJILI YA KUELEZA UTENDAJI WA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI



Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa habari Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa maandamano hayo wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo.
 
Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu, la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.




SAFARI MPYA YA TRENI KUANZA SAFARI ZAKE KWENDA BARA



Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara  ambayo itaondoka  Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanzai takuwa Jumapili hii ya  Septemba 04,2016 saa 9 alasiri. 

Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa  12 kutokea   Dar  es Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili kulala na mawili daraja la kwanza. Katika stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa  mabehewa mawili mawili ya daraja la tatu.

Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam. 

Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3
kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..

Wakati huohuo  Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria
wa kupeleka huduma za kuuzwa  tiketi za safari zake  mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kutoa huduma hiyo kwa  wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya jirani . 
 
Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za  behewa moja la daraja la 3. Pia kuna mpango wa  kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,

Nd Focus Makoye Sahani,

Dar es Salaam,

Agosti 23, 2016.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU