Facebook Comments Box

Sunday, March 31, 2013

ANGALIA SIRI YA MTUNGI SEHEMU YA 11 HAPA




LADY JAY DEE: CLOUDS FM NI WANAFIKI WANATAKA WAHONGWE NDIPO WAPIGE NYIMBO ZA WASANII

Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. "Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"

Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhuru. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

"Hee! Kuna watu wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"

" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"

Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa.

SOURCE:JAMII FORUM

ANGALIA MSIMAMO WA LIGI KUU BARA BAADA YA MICHEZO YA JANA TAR 30/03/2013, JUMAMOSI.


MSIMAMO WA LIGI KUU BARA BAADA YA MICHEZO YA JANA TAR 30/03/2013, JUMAMOSI


YANGA WAKAMATWA NA POLISI HUKO MKOANI MOROGORO


 Kikosi kamili cha timu ya Yanga kilichowekwa Korokoroni hapo jana Morogoro.(Yanga 0-Polisi 0)
 Kikosi cha Timu ya Polisi kilichoiwekea ngumu Yanga huko Morogoro jana kwa kutoka nayo bila kufungana.



UHURU KENYATA AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMANI BAADA YA MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUWA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA HAKI

MAHAKAMA:
Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki,  na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili  9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.

 Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.

uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nne walichaguliwa kwa
haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi huu, akimaanisha Kenyatta na
mgombea mwenza na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.

Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa
kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta
binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani,
utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.

Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya
asilimia 43,28 za Odinga.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU