Facebook Comments Box

Monday, October 7, 2013

VIJANA WAKUTWA MSITUNI WAKIFANYA MAZOEZI MAKALI

Kamanda Zellothe Stephen akionesha CD za mafunzo ya kijeshi zilizokuwa zinatumiwa na kundi hilo.

Na Abdallah Bakari, Mtwara — POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab.
Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen ameuambia “mtandao wa Kusini Leo” kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema: “CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al-Shabaab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd Amin na Mogadishu Sniper,” alisema Stephen.
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha Sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.
Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary (39) mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail (27). Abdallah Y. Hamisi (32), Salum Wadi (38), Fadhili Rajabu (20), Abbas Muhidini (32), Ismail Chande (18), Said Mawazo, Issa Abeid (21), na Ramadhani Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha Likokona.
Kuhusu vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda Zelothe alisema, “Tumekamata mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi, Betri, Simu za kiganjani 5, Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu, Vitabu mbalimbali wa dini ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150 na virago vya kulalia. Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima.


IRINGA FOOTBALL FOR HOPE CENTRE WATENGENEZA KITUO NA UWANJA WA KISASA

Mkurugenzi wa Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) mkoani Iringa, Jonnie Nkoma akimweleza Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osia juu ya kituo kipya cha Iringa Football for Hope Centre kitakachozinduliwa wiki hii ili kukuza vipaji vya watoto na Vijana mkoani humo. Kushoto ni Mwanachama wa Tabata Veteran, Ipyana Mwakasege. (picha: Mpoki Bukuku)

Kituo cha kisasa cha vijana cha Iringa Football for Hope Centre kinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii mjini Iringa ikiwa ni sehemu shamrashamra za uzimwaji wa Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza mjini Iringa juzi Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osiah alisema kituo hicho kilichojengwa na Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) la mkoani Iringa kimefadhiriwa na shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) ili ukuza vipaji vya mpira na kutoa elimu na ushauri nasaha: "Mradi huu haupitii moja kwa moja katika vyama vyetu vya michezo bali katika
taasisi zinazotoa eklimu za kijamii na kufundisha soka," alisema Angetile.
Alipongeza shirika la IDYDC kwa kukamilisha mradi huo na kusema kitendo hicho kitafanya FIFA kutoa fedha zaidi kwa ajili ya miradi kama hiyo nchini: "FIFA watafurahi kuiona fedha walizotoa zinatumika ipasavyo kitu ambacho kitawafanya wawe radhi kutoa misaada zaidi na hii itasaidia kukuza soka letu."
Mkurugenzi wa IDYDC, Jonnie Nkoma alimweleza Katibu Mkuu wa TFF kwamba kwa sasa ujenzi wa kitu hicho uko katika hatua za mwishoni kukamilika na kwamaba kitaanza kuhudumia timu za watoto na vijana zaidi ya 120 kitakapofunguliwa.
Nkoma alisema kituo hicho kitakuwa kinatumika usiku na mchana kwani wanafunzi na watoto watakuwa wakipata mafunzo nyakati za jioni wakati vina na watoto wa mitaani watatumia usiku kwa ajili ya mazoezi ya kukuza vipaji vyao: "Mbali na michezo vijana watakuwa wanapata mafunzo ya afya ya uzazi na ugonjwa waUkimwi na pia watapata nafasi ya kujua afya zao kwa kupima UKIMWI bure papa hapa kituoni.
Mbali na uwanja, kituo hicho pia kina ofisi, vyumba vya kutoa elimu na ushauri nasaha, upimaji wa VVU, chumba cha kompyuta na darasa.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU