Facebook Comments Box

Tuesday, December 31, 2013

BASI LA BM LAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU NA KUUWA SITA PALEPALE

Habari tulizo zipata muda huu zinasema basi la BM likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha limegonga watembea kwa miguu na watu sita wamefariki hapohapo.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Boma la ng'ombe moshi na chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo alipokuwa akimkwepa dereva wa pikipiki.



RAIS KIKWETE AMUAPISHA IGP MPYA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Ads not by this site
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Ads not by this site
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU*+-


Saturday, December 28, 2013

HII NDIO HABARI MPYA KUHUSU TV IMAAN

Picha chini ni CEO wa Tv Imaan Br Ally Ally Ajiraan akionesha bahasha ya barua waliopewa na Tume ya mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye maelezo kuhusu Tv Imaan.

Na chini ni barua yenyewe. Hii ni ishara nzuri inayo ashiria kuwa Tv hiyo ambayo ni kipenzi cha waumini wa kiislam na Tv ya kwanza ya kiislam nchini Tanzania itakuwa hewani muda si mrefu.


Thursday, December 26, 2013

JE WAMJUWA ALIYEBUNI JINA TANZANIA? HEBU MJUE HAPA

UNAPOTAJA historia ya nchi Tanzania, ni dhahiri kwamba hutaacha kutaja majina ya wapigania uhuru na viongozi mbalimbali walioiongoza tangu enzi za ukoloni, hadi kupata uhuru.

Hata hivyo, katika kila historia ya taifa lolote iliyojengwa, kuna watu waliofanikisha historia hiyo, lakini kwa sababu moja au nyingine, michango ya baadhi yao imesahaulika na pengine kutotajwa kabisa kwenye historia hizo.

Wengi wa Watanzania tunafahamu kuwa jina la nchi yetu Tanzania, limetokana na majina ya nchi mbili zilizoungana na kuwa moja ambazo ni Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo tulivyofundishwa shuleni. Wengine wanaamini kuwa Rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania.

Lakini ukweli ni kwamba, jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari  Mzumbe.

Ilikuwaje?:
“Nilikuwa maktaba najisomea, nilishika gazeti la Daily News, wakati huo likiitwa The Standard, ndipo nikaona tangazo hilo,” anaeleza Dar alivyopata hamasa na kuongeza:

“Siku hiyo hiyo, nikafanya majaribio ya kutafuta jina bila hata ya kuishirikisha familia yangu. Nilichukuwa karatasi na kalamu, lakini kabla sijaanza kufanya chochote, nilimwomba Mungu aniwezeshe kwa maana naamini Mungu, ndiye kila kitu wakati wa kufanya jambo lolote.”

“Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili;  Iqbal na Ahmadiya,” anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na  Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.

Kupata jina Tanzania:
Akisimulia alivyopata jina Tanzania, anasema kuwa ilimchukua dakika tano tu kufikiria na kulipata jina hilo.

“Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,”anasimulia Dar.

Anabainisha kuwa baadaye alifikiria na kugundua kuwa majina mengi ya nchi za Afrika yanaishia na IA mfano akitoa mfano wa Ethiopia, Gambia, Tunisia, Nigeria, Algeria, Somalia, Zambia, Namibia na kwamba baada ya kubaini hilo aliamua kuongezea herufi hizo mbili na kupata jina Tanzania.

“NIlituma maombi yangu katika shindano hilo, bila kumwambia mtu yeyote nyumbani,” anasema Dar. Baada ya muda mfupi baba yake, mzee Tufail Ahmad Dar, alipokea barua kutoka Wizara ya Habari na Utalii (wakati huo), ambapo ndani yake kulikuwa na ujumbe wa pongezi ya kwamba kijana wake ameshinda katika shindano hilo.

“Wakati naandika, sikuwa na matumaini kama nitashinda kwa kuwa shindano hilo lilikua wazi kwa watu mbalimbali, hivyo sikuwa na tarajio lolote kama ningeshinda,

“Jioni wakati narudi nyumbani, baba mzazi alinifungulia mlango wakati si kawaida yake kwani mama ndiye alikuwa akinifungulia siku zote, hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa. Lakini, nilikaribishwa na tabasamu la baba, pamoja na pongezi nyingi, nilifurahi sana,” anaeleza.

Tuzo:
Dar anasema kuwa kwa ushindi huo, alitunukiwa ngao pamoja na fedha taslimu Sh200 kama zawadi ya ubunifu wake.

Pamoja na kuibuka mshindi wa ubunifu huo na hadi leo jina la Tanzania alilolibuni yeye linaendelea kutumika, lakini Dar anadai kuwa mchango wake huo kwa taifa ni kama hautambuliwi na Serikali imemsahau katika kuandika historia ya taifa la Tanzania.

“Sijui kwa nini sitambuliwi tangu wakati huo? Hakuna chochote kinachoelezea uhusika wangu katika kupata jina la Tanzania na ukiwauliza watu, wengi watakwambia ilikuwa ni Nyerere aliyeleta jina Tanzania, hii inaumiza,” anasema akilalamika.

Tanzania ya sasa:
Baada ya miaka 13 tangu kufariki kwa Nyerere,  Dar anasema kuwa Tanzania haimtendei haki mwasisi huyo wa Taifa, ambalo ni kisiwa cha amani. “Ni kama imepita miaka mingi sana tangu kifo chake. Watanzania wamesahau kila kitu alichokiota Mwalimu Nyerere. Nakumbuka moja ya vita kubwa aliyopigana ni dhidi ya rushwa, yeye aliichukia rushwa lakini kwa sasa, rushwa imekua kama ndiyo tafsiri ya maisha ya Tanzania. Hakuna kitu kinachoweza kufanyika kwa urahisi hata kama ni haki ya mtu, bila kutoa rushwa,” anasema.

Anaongeza kuwa: “Mwalimu Nyerere alikua ni rafiki ya baba yangu na walikua wakionana na kuongea, nakumbuka siku moja kulikuwa na sherehe nyumbani na kwa kuwa tulikuwa watoto, nilimhudumia chai Mwalimu.

“Nakumbuka Mwalimu aliwahi kumuuliza baba yangu; Lini Malaria itaisha nchi hii? Baba alimjibu kuwa, kamwe malaria haitaisha ikiwa hakutakuwa na kujitolea kwa kila mmoja wetu, bila kumtegea mwengine,” anasema.

Katika kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Dar anaishauri Tanzania iendeleze misingi ya maisha ambayo Hayati Mwalimu Nyerere aliisimmamia, ikiwamo umoja na mshikamano, ili kuondoa tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri.

“Tunaona namna ambavyo matajiri wanendelea kuwa tajiri zaidi, wakati maskini wanazidi kudidimia. Kama kungekuwa na ushirikiano kati ya watu hawa wawili, tofauti kati yao ingekuwa ndogo au isingekuwepo kabisa,” anaeleza.

Anashauri pia kuwepo na sanamu za utambulisho wa Baba wa Taifa kila mahali, ili kulienzi jina lake liishi milele. “Kwa ninavyomjua Mwalimu natamani jina lake liishi milele na litangazwe lijulikane dunia nzima,”anasema.

Mohammed Iqbal Dar aliazaliwa mwaka 1944 jijini Tanga, ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Tufail Ahmad Dar. Dar ni baba wa mtoto mmoja, ambapo kwa zaidi ya miaka 40 sasa amekuwa akiishi nchini Uingereza alikoenda kwa ajili ya kusoma kabla ya kuwa raia wa nchi hiyo.

Mbunifu huyo wa jina la Tanzania ni Mhandisi wa Masuala ya Redio, kazi anayoifanya nchini Uingereza, akieleza kuwa katika kuienzi nchi yake, nyumba yake iliyopo mjini Birmingham, ameipa jina la Dar es Salaam, ikiwakilisha ubini wake, pamoja na Jiji la Dar es Salaam.


Wednesday, December 25, 2013

MKURUGENZI WA KCMC AACHIA NGAZI

Mkurugenzi wa Hospitali ya KCMC ameachia ngazi. Hii imefuatia uamuzi wake alio utoa kwenye kikao cha bodi ya wakurugenzi wa msamaria mwema.
Dk Ntabaye ameomba bodi ya wakurugenzi wa msamaria mwema wasimuongeze mkataba mwingine tena.
Inasemekana mkurugenzi huyo ameacha manung'uniko na malalamiko mengi hospitali hapo pamoja na kushusha ari ya kazi kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Nafasi ya ukurugenzi kwa sasa imekaimiwa na Pro ulomi.


KOCHA WA SIMBA AFARIKI DUNIA

James Kisaka enzi za uhai wake.
Aliyekuwa kocha wa makipa wa Klabu ya Simba, James Kisaka amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Burhan, Dar es Salaam. Kisaka aliyewahi kuwa kipa wa timu hiyo miaka ya nyuma, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichwa, macho na miguu kwa muda mrefu.
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI. AMINA
CHANZO: GPL


Tuesday, December 24, 2013

PICHA: WAZIRI MWAKYEMBE AFANYA UKAGUZI WA NAULI ZA MABASI LEO




Waziri wa Uchukuzi,Dr Harisoni Mwakembe afanya ukakuguzi wa tiketi ilikubaini mabasi yaliyo toza gharama kubwa za nauli zakusafiria katika kipindi cha Xmass na mwaka mpya,badhi ya mabasi yalikamatwa nakuamuliwa kurudisha nauli zilizozidi abiria wao.zoezi hilo limefanyika majira ya alfajiri katika eneo la Visiga mkoani pwani na kila basi lilozidisha nauli lilitozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu. 



WANNE WAKAMATWA NA HEROIN ARUSHA


GEDSC DIGITAL CAMERAKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari bunduki aina ya SMG iliyokamatwa wilayani Ngorongoro hivi karibuni huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika kifurushi chenye madawa ya kulevya aina ya Heroin yaliyokamatwa jana wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
 
Kuelekea katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas, Jeshi la Polisi Mkoani hapa limeendelea kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya ambapo safari hii limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin. Tukio hilo limetokea jana tarehe 23.12.2014 muda wa saa 12:30 jioni maeneo ya Elikyurei wilayani Arumeru.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas amesema kwamba tukio hilo limefanikiwa baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema ambapo askari wa Jeshi hilo walikwenda katika eneo husika na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa ndani ya chumba cha mtuhumiwa mmojawapo huku wakiwa wanaendelea kufunga kete za madawa hayo na tayari walikuwa wamefunga kete 25.
 
Kamanda Sabas aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Seifu Bakari (28) na Hamid Makame wote ni wakazi wa Elikyurei wilayani Arumeru pamoja na wenzao ambao ni Evance Gidion (29) Mkazi wa Ngarenaro na Abraham Hamis (23) Mkazi wa Kaloleni jijini hapa.
 
Kamanda Sabas alisema kwamba madawa hayo yenye uzito wa gramu 100 yanakadiriwa kuwa na thamani ya Tsh 10 Mil. Mpaka hivi Jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kufahamu undani zaidi na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
 
Kufuatia tukio hilo na mengine ya nyuma Kamanda Sabas alizidi kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa jinsi wanavyoonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo juu ya kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu na kuahidi kuendeleza falsafa ya Polisi Jamii ambayo inaleta mafanikio makubwa katika suala zima la kuimarisha amani na utulivu Mkoani hapa.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU