Facebook Comments Box

Monday, June 3, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-rose Migiro, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Makamu, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa rasimu ya Katiba uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kabla ya  uzinduzi rasmi wa rasimu ya Katiba uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Viongozi mbali mbali wakifuatilia hotuba hiyo 
 Wanahabari


 Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Katiba,Dkt. Salim Ahmed Salim.


TAIFA STARS SUDAN NGUVU SAWA


                         Kikosi cha Timu ya Taifa 'Taifa Stars'

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetoka sare ya bila kufungana na Sudan (Nile Crodcodile) katika mechi ya kujipima nguvu iliyochezwa jana (Juni 2) kwenye Uwanja wa Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Bamlak Tessema wa Ethiopia ilikuwa sehemu ya maandalizi kwa timu zote ambazo wikiendi ijayo zinacheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia. Wakati Stars itakuwa ugenini nchini Morocco, Sudan itacheza nyumbani dhidi ya Ghana.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilicheza vizuri mechi hiyo, hasa kipindi cha pili ambapo ilifanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini ama washambuliaji walipiga nje au mipira yao kuokolewa na kipa Ehab Abdelfatahh wa Sudan.

Washambualiji wa Stars akina Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Amri Kiemba wakiongozwa na John Bocco walilitia msukosuko mara kwa mara lango la Sudan ambalo lilikuwa chini ya beki wa kati Nadir Eltayeb ambaye alifanya kazi ya ziada dakika ya 72 kuokoa mpira uliokuwa ukielekea wavuni.

Stars katika mechi hiyo iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nadir Haroub/Vicent Barnabas, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba/Khamis Mcha na Simon Msuva/Athuman Idd.

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

Timu inaondoka kesho alfajiri kwenda Morocco kwa kupitia Cairo, Misri ambapo inatarajia kuwasili Casablanca saa 8 mchana.


MIMBA YA DIAMOND YAANZA KUMPELEKESHA PENNY

 
Penny akiwa hospitali.
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha  akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.
 
Diamond na Penny katika pozi.
Akizungumzia hali hiyo, Penny aliliambia Bongoclantz.com  kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.
Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.

AJALI MBAYA MOROGORO WATU WAPOTEZA MAISHA


  Foleni kubwa sana ambayoilisababishwa na ajali hiyo

 Ni Zaidi ya Kilometa 5 foleni ya Maroli na mabasi

Scania ilikuwa inaelekea Jijini Dar es salaam na Fuso ikielekea Morogoro Ziligongana uso kwa uso na kusababisha haya uyaonayo katika picha hizi.

 Zilikuwa barabarani ikalazimu zisukumwe pembeni kidogo angalau watu wapite.Ajali hiyo imehusisha FUSO lililokua linatokea Moro limesheheni mkaa,na SCANIA SEMI-TRAILER lililokuwa linatokea Dar,haya malori yamegongana,na baada ya kugongana Fuso imegeukia ilikotoka yaaan moro,na cabin ya Scania imeng'oka yote,watu watano kwenye Scania wamekufa hapohapo.

Kinachohangaikiwa sasa ni jinsi ya kuitoa hii folen ambapo magari yanayokadiriwa 3000 yamenasa kwenye foleni......
Ila inaonesha uhaba wa vifaa kama vile BREAK DOWN ndo umesababisha foleni.
Hii si ajali ya kwanza maeneo ya MASEYU,mwezi mmoja au miwili nyuma,kuna watu walibanwa na lori lililopata ajali na mmoja alikufa baada ya kushindwa kuokolewa.


 Hili Fuso inasemekana Dereva alipoteza uhai wake hapohapo na Konda ameumia sana sana.



 Kama unavyoweza kuona hapo Hata Uskani hauonekani unaweza pata picha kuwa Dereva anaweza akawa katika hali gani.


Hii ni Scania iliyogongana na Fuso hiyo waliokuwa humu wako Hospitali kwa matibabu.


MMOJA WA WAANZILISHI WA JAMII FORUM (MAXENCE MELO) AWASHUKURU WATANZANIA


 Wana JF,
 Kwanza namshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kuishi tena (2nd chance) mimi na mdogo wangu. Mungu yu mwema kwetu.
Katika ajali hii, huwezi kutarajia kuwa tumetoka tukiwa hai na tunaendelea vema kama tulivyo sasa.

Aidha, nawashukuru wote waliotoa pole zao kwetu via JF na kututakia kupona haraka. Tunashukuru sana na tunazidi kufarijika kwa ushirikiano wenu katika maombi (na baadhi walituma michango itusaidie katika matibabu). Moderators, shukrani kwa kuendelea kulisimamia jukwaa hili kwa weledi mkubwa.

 Napenda kuwashukuru wanasiasa watatu; ndugu Zitto Kabwe, Dr. Faustine Ndugulile na Ndugu Hussein Bashe - ambao wameonyesha kujali tangu tunapata ajali hadi sasa (wanatujulia hali tunavyoendelea); hii inatia moyo na kuonyesha kujali kwao kwetu. Mungu awazidishie muendelee kuwa na moyo huu. Shukrani zetu ziende kwa wana JF wa Nzega, Mwanza na Dar; ambao wamekuwa nasi bega kwa bega tangu siku ya ajali. Ni wengi lakini inakuwa vigumu kuwataja kwenye shukrani zetu hizi bali tunapenda wafahamu kuwa tunawashukuru sana.
Tunawashukuru sana wengine wote ambao kwa njia tofauti wamekuwa wakitaka kujua tunaendeleaje kiafya na kuwajuza hapa; kutokana na mazingira tulikuwa tunashindwa kuwajibu wote lakini wengi tumewajibu kuwafahamisha kilichotokea na tunavyoendelea.
Ndugu zangu, tupo hai kwa mapenzi ya Mungu tu!

Nini kilitokea?

Inakuwa vigumu kuelezea kwa kirefu kilichotokea. Kuwa ni mwendo kasi? Sijui. Kuwa ni mkono wa mtu? Pia sijui. Kuwa ni bahati mbaya? Naweza kusema hivyo! Hatumlaumu yeyote katika hili na hatumnyooshei kidole yeyote. Kwa dereva yeyote anafahamu nini kinaweza kutokea pale 'Sterling Rod' inapokatika ukiwa katika mwendo zaidi ya spidi 80.
Yapo mengi yanaweza kuhisiwa, yapo mengi yanaweza kusemwa lakini ambacho tunaweza kukiri ni kuwa Mungu yu mwema kwetu.

Hali yetu:

Baada ya ajali, mdogo wangu ambaye pia ni member wa JF kama Chachu Ombara, alibainika kuvunjika mfupa wa kati ya kiwiko na bega mkono wa kushoto na sasa amefanyiwa upasuaji na madaktari bingwa Muhimbili, anaendelea vema.
Binafsi nilibainika kuwa na uvimbe kidogo kwenye ubongo upande wa kulia; naendelea vema namshukuru Mungu.

Mwisho: 

Ushauri wangu kwa wanaoendesha magari, wasafiri kwenye ruti ndefu na hata katika hali ya kawaida: - Kabla ya safari yoyote mwite Mungu na ujikabidhi kwake, atakuitikia kwa namna ya kipekee - Unapoendesha, funga mkanda. Hata kama umekaa siti ya nyuma (katika gari binafsi). - Ukiwa barabarani (dereva), jitahidi kuzingatia alama za barabarani; wajali madereva wengine kama ambavyo ungependa wakujali.

Nasikitika kuwa huenda nisijibu maswali ambayo labda yanaweza kujitokeza kutokana na kuwa nina matatizo ya kuumwa kichwa (kilijigonga sana chini wakati gari linapinduka) lakini naamini nikikaa vema nitarejea na aidha kujibu au nikiwa nimechelewa nitatuma PM kwa mhusika.

Asanteni sana.

Maxence
 ===================
Tokana na maoni ya wengi wa wadau wa Jukwaa La Siasa kutokua na taarifa hii mbaya ya Ajali ilipokua imetangazwa hapa, mtuwie radhi Moderators kwa maamuzi ya kuhamishia habari hii Jukwaa La Siasa toka habari na hoja Mchanganyiko.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU