Facebook Comments Box

Monday, August 26, 2013

HII NDIO TAREHE AMBAYO RADIO IMAAN ITARUDI HEWANI

Tv Imaan ikiwa kazini wakati wa sala ya Idd wakimuhoji Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahdi

Mtaalam wa Mitambo wa Radio Imaan na Tv Imaan Muhammad Maembe akimuelekeza Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahadi mitambo inavyofanya kazi katika jengo jipya la makao makuu ya Radio na Tv Imaan

Mwenyekiti wa Radio Imaan Br Arif Nahdi akikagua jengo jipya la Tv Imaan na Radio Imaan

Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahdi akihojiwa na Radio MuM juu ya ujio wa Radio Imaan



SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA: VIONGOZI NAO KUPEKULIWA KAMA ABIRIA WA KAWAIDA

KULIA: Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam. KUSHOTO: Dk Harrison Mwakyembe. 

Kuanzia sasa viongozi wote serikalini watakaopita kwenye viwanja vya ndege nchini, watakuwa wakikaguliwa kama abiria wengine, isipokuwa Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge.
Waziri  wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema ipo tabia ya  viongozi  wenye madaraka, kukiuka utaratibu na kupita   katika  viwanja vya ndege  bila kukaguliwa.Alisema kutokana na hali hiyo, amewaambia watumishi  wanaofanya kazi katika viwanja hivyo, hususan Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) viongozi wasiokaguliwa ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge.

Alitoa msimamo huo wiki iliyopita  kupitia kipindi cha Jenerali on Monday, kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten. Alisema viongozi wengine wote, wakiwamo mabalozi na mawaziri lazima wakaguliwe.



Dk Mwakyembe alisema aliwaambia viongozi wasiopenda kukaguliwa, wasipande ndege. Alisema pamoja na baadhi kuona ni usumbufu, inawezekana wakajikuta wamesahau vitu hatari, kama vile risasi na wakaenda kugundulika nje ya nchi ikawa tatizo.

Alitoa mfano kwamba aliwahi kupigiwa simu na mmoja wa mabalozi, akilalamika kwamba vijana wake wamemkagua uwanja wa ndege. Alisema alimjibu kwamba wanatimiza wajibu wao.

Katika mahojiano yaliyojikita juu ya tatizo la  dawa za kulevya  nchini, Dk Mwakyembe alisisitiza  kwamba hatua alizoanza kuchukua kudhibiti upitishaji dawa hizo kwenye viwanja vya ndege, siyo moto wa kifuu wala nguvu ya soda.

 “Ninachokifanya hapa  ni kile ambacho kinapaswa kufanywa…na hili la dawa za kulevya katika viwanja vya ndege, nitalikomesha,” alisema. Alisisitiza kwamba udhibiti huo ni kwa viwanja vyote vya ndege nchini.

 Dk Mwakyembe alisema,  “kwa sasa mizigo yote inayoingia katika eneo hilo, lazima ikaguliwe, kwani huo sio mzaha, sio moto wa kifuu wala nguvu ya soda.”
Kwa mujibu wa Waziri, mizigo inayoingia imekuwa haikaguliwi. Alisema katika kutekeleza ukaguzi huo wa mizigo inayoingia, imenunuliwa  mitambo kwa  ajili hiyo.  Kuhusu wanaomeza dawa za kulevya,  alisema wamekuwa wakigundulika kutokana na ufuatiliaji kuanzia kwenye ndege.

Alitoa mfano kwamba  kwa sasa endapo abiria atapanda ndege katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, mathalani kwenda Dubai, akipewa chai au pombe, akakataa kunywa,  kwa vyovyote huyo lazima akaguliwe zaidi.
Katika hilo, aliwaasa vijana wa Tanzania kujiepusha na hali hiyo, kwani pindi akishuka kwenye uwanja wowote, namba yake ya kiti itashikiliwa na atakaguliwa ipasavyo, kubaini kama amemeza dawa.

Hatua ya Mwakyembe kuamua kuvalia njuga dawa za kulevya, inatokana na kile ambacho kinaelezwa kuwa ni kuchafuka kwa Tanzania, kutokana na baadhi ya watanzania kukamatwa nje ya nchi, wakisafirisha dawa hizo, wakiwa wamezipitisha uwanja wa ndege.  Dk Mwakyembe alieleza kuwa hatua yake ya kuvalia njuga suala hilo, inaungwa mkono na serikali kwa ujumla. Hivi karibuni waziri huyo alifanya ziara ya ghafla  katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na kubaini kuwa tatizo si vifaa vya ukaguzi, bali ni baadhi ya wafanyakazi wasio waadilifu. Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema hivi karibuni serikali imeanzisha mkakati wa kutokomeza wimbi la dawa za kulevya kwa kudhibiti viwanja vya ndege na sehemu mbalimbali za mipakani, zinazotumiwa kupitisha.
 


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU