Ikiwa ni siku moja tu baada ya
kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya
mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa
Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati
iliyoundwa kuchunguza kifo hicho. Namnukuu akisema “ni kweli
wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na
shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana” Juzi September 12 ndio askari
anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa
mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.