Athumani Idd Chuji - Kiungo mpigaji wa pasi ndefu Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts amewataka wachezaji wake 
wacheze pasi fupi zenye akili kwa sababu ndiyo ushindi wao na si ndefu 
kama wanapopoa maembe mtini na akaweka wazi kuwa, alimtumia kiungo wake 
mkongwe, Athuman Idd ‘Chuji’ kama mchezaji wa akiba kwa sababu hajafanya
 mazoezi na timu kwa muda mrefu.
Chuji aliingia kipindi cha pili katika mechi dhidi
 ya Ruvu Shooting akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo na 
dakika chache baadaye Yanga ikapata bao la ushindi lililofungwa na Hamis
 Kiiza raia wa Uganda matokeo yakawa ya ushindi wa bao 1-0 mwishoni mwa 
wiki.
Kutokana na kitendo hicho mashabiki wa soka 
walihoji na kupiga kelele kulikoni kiungo huyo aachwe nje wakati ni 
msaada kwenye timu.
Brandts alisema: “Nataka timu icheze mpira kwa 
pasi fupi fupi na kwa umakini na si ndefu zisizo na mpango kwa sababu 
ndiyo zinatugharimu na hata mechi yetu na Ruvu kipindi cha kwanza 
hatukuwa vizuri.” 
Akimzungumzia Chuji, kocha huyo alisema: “Sikuweza kumtumia kipindi cha kwanza kwa sababu hakuwa na muda mzuri wa pamoja na wenzake katika mazoezi na alikuwa kwao, kulikuwa na matatizo ya kifamilia.
Akimzungumzia Chuji, kocha huyo alisema: “Sikuweza kumtumia kipindi cha kwanza kwa sababu hakuwa na muda mzuri wa pamoja na wenzake katika mazoezi na alikuwa kwao, kulikuwa na matatizo ya kifamilia.
Hali hiyo ndiyo ilinifanya nisimpange kikosi cha kwanza na ndiyo maana nilimtumia kipindi cha pili.”
Chanzo:Mwanaspoti
Chanzo:Mwanaspoti









