Facebook Comments Box

Sunday, August 4, 2013

MAWAIDHA: SHEIKH NURDEEN KISHK - MAMBO MATATU YA KUFANYA KATIKA KUMI LA MWISHO




MBWANA SAMATTA AENDELEA KUIBEBA TP MAZEMBE

Samatta
Yawezekana Taifa Stars ikawa haifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa kiasi cha kuwa chini kwenye chati za soka barani Afrika na duniani kwa ujumla lakini jina la Taifa hili limekuwa likitajwa na lina uhakika wa kutajwa katika level za juu za soka barani afrika, hii ni kutokana na makubwa yanayofanywa na kijana mwenye umri wa miaka 21 raia wa Tanzania ambaye ni Mbwana Samatta .
Mchezaji huyu ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa akifanya vizuri sana kwenye klabu yake ya Tp Mazembe ya Nchini Congo DRC kwenye michuano ya kimataifa na amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika .
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi iliyochezwa juzi kati ya timu yake ya Tp Mazembe na FUS Rabat ambapo Mazembe ilishinda 3-0 na mpaka sasa Samatta amekuwa akifunga kwenye mechi zote nne za michuano hiyo ambazo Mazembe imecheza hali inayomfanya awe na nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo wakati ikimalizika baadaye mwaka huu.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Samatta ambaye Mazembe ilimsajili toka Simba Sports Club ya Tanzania ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na amekuwa na rekodi nzuri sana ya kufunga karibu kila mechi ambayo anacheza kwenye klabu hiyo .
Samatta amefanya watanzania wengi kuwa na shauku ya kufahamu matokeo ya timu ya Tp Mazembe ambapo mara zote watu huuliza timu hiyo imeshinda au la na baada ya kuuliza hivyo huuliza tena Samatta amefunga mangapi kwa kuwa wana uhakika juu ya uwezo wake na rekodi yake ya kuzifumania nyavu.
Ubora wake umemfanya kuishi maisha ya kistaa akiwa nchini Kongo ambapo mashabiki wa Mazembe wanampenda kiasi cha kutaka kupiga naye picha kila wamwonapo mtaani na wakati mwingine kutaka kusukuma gari lake wanapoliona


BINGWA WA DUNIA WA KURUKA KAMBA AMUONESHA RAIS KIKWETE UHODARI WAKE

Picture
Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani (Picha zote, maelezo na video: IKULU)
Rais Jakaya  Kikwete amempongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita.

Kijana huyo, ambaye awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo, Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu.

Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema kuwa walipata
mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.

Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480 kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.

Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao  na kuitangaza Tanzania.

Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea katika kukiendeleza kipaji chake.

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Hamisi Mohamed. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre

Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 

Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.

Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU