Facebook Comments Box

Sunday, March 10, 2013

IJUE HALI YA ABSALOM KIBANDA AFRIKA KUSINI



 
Nachukua fursa hii kuwapa maendeleo ya tiba ya Mwenyekiti wa TEF Absalom Kibanda ambaye amelazwa Hosipitali ya Millpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini.


1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.


Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

MICHUANO YA NSSF CUP 2013 YAZINDULIWA RASMI



Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akikagua timu ya Changamoto kabla ya pambano lao na timu ya Habari Zanzibar. Changamoto iliwavua ubingwa wa michuano hiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Habari Zanzibar kwa kuitandika 3-0.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (katikati) akifuatilia mchezo wa netiboli kati ya NSSF na Mlimani Tv, katika mchezo huo NSSF ilishinda 46-1 Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.

Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa wa ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup dhidi ya NSSF uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Changamoto imeshinda 3-0

SOURCE:MICHUZI

SAFARI YA UHURU KENYATA KUINGIA IKULU YAIVA



Mhe Uhuru Muigai Kenyatta akionesha hati aliyokabidhiwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya jana katika ukumbi wa Bomas na kutangazwa kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo. Mpinzani wake Mhe Raila Odinga amekataa kukubali matokeo hayo na kuonesha nia ya kwenda kuyapinga mahakamani.

Walinzi wakiwa wamelizingira gari lililombeba Rais mteule wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta alipokuwa akiwasili Bomas of Kenya mara baada ya kutangazwa mshindi.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU