Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni ACP Charles Kenyela.
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujishughulisha na uchochezi wa kidini.
Watu hao wamekamatwa hivi karibuni katika msako maalum unaoendeshwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum katika hali ya kukabiliana na uchochezi wa kidini ambao lengo lake ni kuleta chuki pamoja na ubaguzi wa kidini
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleimani Kova amewataja watu hao kuwa ni Kombo Hassan Zuberi mkazi wa Mburahati Barafu (32), Basote Hassan Tandala Rayan mkazi wa Gongo la mboto (24), Mohamed Hassan Sharif mkazi wa Tabata Bima(33) na Salum Athman Mahambi mkazi wa Tunduma(46).
Aidha Kamanda Kova ametoa onyo kali kwamba Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaoleta uchochezi kupitia shughuli za kidini au kisiasa.
SOURCE:DJ-SEK