Facebook Comments Box

Sunday, June 16, 2013

WACHEZAJI WAISLAM WA NEWCASTLE WAGOMA KUVAA JEZI ZENYE NEMBO MPYA

imageimage 
Siku chache baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Pappis Demba Cisse kutoa kauli yakugoma kuvaa nembo ya kampuni ya Wonga ambayo hutoa mikopo yenye riba , mchezaji wa pili ametoka na kuungana na Cisse kwenye msimamo huo wa kutovaa logo ya Wonga kwa kuwa kampuni hiyo inafanya biashara ambayo kwa mujibu wa misingi ya dini ya kiislamu ni Haramu.
Kiungo wa Ivory Coast ambaye atakuwepo uwanjani siku ya jumapili kucheza dhidi ya Taifa Stars Ismael Cheikh Tiote amesema kuwa atazungmza na wanasheria wake kuangalia  wa kutoivaa nembo hiyo . Tiotte kama ilivyo kwa Cisse ni muislamu anayefuata misingi yote ya dini hiyo na kwa mujibu wa sheria za dini yake riba kwenye mkopo unaotolewa kwa mtu mwingine ni haramu.
Newcastle United imesaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Wonga mkataba ambao umeifanya klabu hiyo kuingia kwenye utata na wachezaji wenye imani ya dini ya kiislamu . Newcastle United ina wachezaji wasiopungua watano ambao wamezungmzia kutokuwa tayari kuvaa nembo ya Wonga jambo linaweza kusababisha klabu hiyo kulazimika kuwauza wachezaji kama Pappis Cisse , Tiotte na wenzao kwani hawako tayari kutumiwa kwenye kampeni za matangazo ya kampuni hiyo.


BAADA YA TUKIO LA BOMU UCHAGUZI WA AHIRISHWA ARUSHA


Kufuatia tukio la mlipuko jana jumamosi Arusha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha chaguzi za madiwani katika kata zote nne (4) jijini arusha hadi jumapili ya tar 30/6/2013.

 Tume ya taifa ya Uchaguzi imesimamisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani ktk kata nne jijini Arusha. Akizungumza kwa njia ya simu na Radio TBC FM,kutoka Zanzibari mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi alisema kua wameamua kusimamisha uchaguzi huo ili kuwapa nafasi vyombo vya usalama kuchunguza swala hilo.
Alisema kua sheria inawapa mamlaka kufanya hivyo pale wanapogundua kuwa hakutakua na uhuru wa mpiga kura kwenda kupiga kura. Alisema haiwezekani uchaguzi ufanyike ktk hali kama hiyo huku kukiwa na wasiwasi.


ANGALIA HIGHLIGHT YA MECHI YA BRAZIL 3 - 0 JAPAN


Brazil vs Japan 3:0 MATCH HIGHLIGHTS by footballdaily1

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU