Facebook Comments Box

Sunday, May 25, 2014

MAXIMO KUJA KUINOA YANGA?

Kuna habari za kurejea tena kwenye soka la Bongo kwa aliyekuwa
kocha wa timu ya Taifa Mbrazil Marcio Maximo lakini safari hii sio
kuinoa Taifa Stars, ni watoto wa Jangwani timu ya Dar es salaam
Young Africans maarufa kama Yanga.
Maximo ni kocha ambaye atakumbukwa kwa mambo mengi kwenye
soka la Bongo na machache kati ya hayo, ni namna alivyokuwa na
msimamo kwa wachezaji waliokuwa na utovu wa nidhamu,
kuhamasisha watanzania kuipenda timu yao ya taifa na kubwa
kuliko yote, ni kuipeleka Taifa Stars kwenye michuano ya kombe la
Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN.
Baada ya mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu ya Yanga Hans Ven
Der Pluijm kumalizika mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi
majuzi, kumekuwa na habari za wanajangwani hao, kumsaka mtu
ambaye atakuja kuungana na kocha msaidizi wa timu hiyo Boniface
Mkwasa ili kuirejesha timu hiyo kwenye makali yake baada ya
msimu huu, kujikuta wakipoteza ubingwa wao mbele ya watoto wa
mjini timu ya Azam dakika za lala salama.
Kama Mbrazil huyo atafikia makubaliano na kuja kuinoa timu hiyo,
ni wazi kuwa atakuwa na faida kutokana na kuyafahamu vema
mazingira na utamaduni wa watanzania. Maximo anajua kiwango
cha wachezaji wa kibongo na umuhimu wa mechi kubwa kama
“Kariakoo Derby” ambayo huwakutanisha timu za Simba na Yanga.
Kwa siku za hivi karibuni, Yanga ni mahali ambapo makocha
wamekuwa hawakai muda mrefu kutokana pengine na sababu
mbalimbali kama vile, maslahi na kutofikia malengo ya timu.
Mashabiki wa timu hiyo kwa muda mfupi, wamemuona kocha
Mbelgiji Thom Saintfiet na waholanzi Ernie Brands na Hans Van Der
Pluijm ambaye amemaliza mkataba wake wa miezi sita.
Pamoja na kufanya mawasiliano na kocha Maximo, bado Yanga
wanaendelea kusaka kocha mwingine ambaye atakuja kuwaletea
mafanikio endapo makubaliano na Mbrazil huyo hayatofikiwa.Huu
ni muda ambao mashabiki wa Jangwani wana hamu ya kujua
mwalimu wao mpya kuelekea kuanza kwa ligi kuu ambayo
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.
CHANZO: TANZANIA SPORTS


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU