Facebook Comments Box

Wednesday, April 10, 2013

RAISI KIKWETE NA MAMA SALMA KATIKA SHEREHE YA KUAPISHWA KWA RAIS WA KENYA UHURU KENYATA


Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta huko Ikulu mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa nne wa nchi hyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi-Kasarani jijini Nairobi jana tarehe 9.4.2013.
Rais Mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwashukuru Marais na wakuu wa nchi waliohudhuria sherehe za kumwapisha wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa huko ikulu jijini Nairobi.
Rais wa Kenya aliyemaliza muda wake, Mwai Kibaki akifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kukamilika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na wake wa viongozi wa juu wa Kenya, Mama Magrate Kenyatta (kushoto) ambaye ni mke wa Rais Uhuru na Mama Recheal Ruto (kulia) Mke wa Naibu Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa William Ruto huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya kuapishwa viongozi hao jana tarehe 9.4.2013.
Rais wa Kenya aliyemaliza muda wake, Mheshimiwa Mwai Kibaki akifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kukamilika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mama Magrate Kenyatta katika ikulu ya Kenya jijini Nairobi mara baada ya sherehe za kuwaapisha kukamilika.


VIBONZO: ELIMIKA NA VIBONZO HIVI VICHACHE VYA KIPANYA








HAWA NDIO WALIOANDAMANA KUSHEHEREKEA KIFO CHA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA

Waandamanaji wa Uingereza wakiwa waameumia kichwani baada polisi kuwatandika kutokana na kusherehekea kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Magret Thatcher.
 
Wakati Waingereza wengi wakihuzunika kwa kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Magreth Thatcher, kundi moja la wakazi wa nchi hiyo waliamua kuandamana huku wakinywa pombe na kufurahia kicho cha kiongozi huyo.

Watu hao walionyesha kufurahia kifo cha mama huyo ambaye alikuwa waziri wa kwanza wa kike nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa, mamia ya wakazi katika Miji ya Brixton na London Kusini walionekana wakiwa na michoro mbalimbali ya kumkashifu marehemu.

Sababu za kuandamana hazikuwa wazi, lakini wengi wanaamini kwamba ni kutokana na msimamo mkali wa marehemu Thatcher.

Kwa nyakati tofauti wakazi wa miji hiyo walioneka kusherehekea kifo hicho kwa kunywa pombe na kuchora picha zenye mionekano ya ajabu,
huku wakiliandika jina la Waziri Mkuu huyo wa zamani kwenye mabango yao ambayo walikuwa wakiyatembeza.

Polisi katika maeneo hayo wanawashikilia baadhi ya watu waliokuwa kwenye makundi wakishangilia na kunywa pombe tangu saa 11.0 jioni ya juzi.

Zaidi ya watu 300, vijana na wazee walisherehekea hadi wakati wa usiku katika Mitaa ya London, wakiwa na makopo ya maziwa mikononi huku wakicheza muziki wa rege.
Watoto wadogo walionekana wakiambatana na wazazi wao, huku wengi wakivalia nguo na nywele za bandia .
 SOURSE MWANANCHI


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU