Facebook Comments Box

Thursday, June 12, 2014

PAUNDI MILIONI 30 ZAMPELEKA FABREGAS CHELSEA

Wakati watu wakiwa na hamu kubwa na shauku ya kujua nini kitatokea leo usiku katika ufunguzi wa kombe la dunia kocha mwenye maneno mengi na machachari Jose Mourinho maarufu kama special one kafanya yake kwa kusajili kiungo wa Barcelona fabregas kwa paundi za uingereza milioni 30.



KIBONZO: LIFT YA KWANZA MKOANI MBEYA




CHINA YAKATAZA MATUMIZI YA WINDOW 8 KWENYE COMPUTER ZA SERIKALI PAMOJA NA TAASISI ZAKE

Katika wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na China , Serikali ya Marekani inailaumu china kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni zake na biashara nyingine huku china nayo ikiilaumu marekani. China baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo.

Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS (China Operating System) kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .

Suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita huko ulaya , lakini umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya

Kitu kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .

Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote.

Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni , ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani .

TAHADHARI YA PICHA: ASKARI AUAWA KINYAMA KWA KUKATWA NA MAPANGA KIMANZICHANA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi (SACP) Ulrich Mtei


Marehemu Joseph Ngonyani:
 huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzichana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.

Jambo la kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye
silaha ambaye amefahamika kwa jina la Joseph Ngonyani na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30.

Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. 

Askari Ngonyani alifariki alipokuwa anapatiwa matibabu
kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye Venance amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.

Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye Veronica Musime, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


SOKO LA MITUMBA LA KARUME LATEKETEA KWA MOTO

Soko la mitumba la Karume likiteketea kwa moto usiku wa saa saba. Chanzo cha moto kinatajwa kuwa hitilafu ya umeme katika moja ya vibanda vilivyopo ndani ya soko hilo. Polisi walifika na magari mawili ya kuzima moto lakini wakashindwa kuudhalilisha moto huo kisawasawa. Vibaka inasemekana walifaidika sana na moto huo.




KIBONZO: KIPANYA NA BAJETI MPYA.





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU