Saturday, May 18, 2013
MPAMBANO WA YANGA NA SIMBA KATIKA PICHA
Haruna Shamte akipambana na Simon Msuva wa Yanga. |
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub akinyanyua ubingwa wa ligi kuu ya VODACOM msimu wa 2012/2013 |
kikosi cha Simba kilichoanza hii leo. |
Makocha wa Yanga Ernest Brandts pamoja na Felix Minziro wakijadiliana jambo. |
Sir Juma Nature pia alikuwepo kutoa burudani. |
Hili ndo lilikuwa bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Didier Kavumbagu kwa kichwa. |
Mrisho Ngassa akiwa amevalishwa jezi ya YANGA kwa mara nyingine tena huku akiwa amefurahi kweli kweli. |
Mwamuzi wa mchezo wa leo Saanya akiwa chini mara baada ya kuumia. |
ATHUMAN IDD "CHUJI" ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA
Athuman Idd Chuji |
Kiungo mkongwe wa Athumani Idd
‘Chuji’ ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya watani.
Chuji aliyecheza namba sita
katika mechi ya watani leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar amekuwa mchezaji bora wa
mechi hiyo.
aliouonyesha uwezo mkubwa SuperSport imemtanza Chuji kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.
Chuji aliwathibiti washambuliaji
wa Simba na ndiye alikuwa akianzisha mashambulizi karibu yote ya Yanga.
Chuji alipiga zaidi ya pasi nne
ndefu ambazo zilifika, pia alikuwa akimchezesha kiungo Haruna Niyonzima ambaye
pia alimtumia kama sehemu ya kuhifadhi mipira anapokwama.
ELIMU YA MSINGI KUWA MIAKA 10
WAZIRI KAWAMBWA.WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAKIWA DARASANI.
RASIMU ya Sera ya Elimu na Mafunzo
nchini inapendekeza kuunganisha elimu ya msingi na sekondari ya kawaida
ya sasa ili kuunda elimu-msingi itakayotolewa kwa kipindi cha miaka 10
kuanzia mwaka 2018, imefahamika.
Rasimu ya kwanza ya Sera hiyo
imeshakamilika na sasa wadau mbalimbali wanatoa mapendekezo yao
kuiboresha, kabla ya kupelekwa bungeni ili kutungiwa sheria.
Aidha, mikakati hiyo itakayotekelezwa ni
kuhuisha muundo na utaratibu mpya wa elimu na mafunzo kwa kuhakikisha
kila mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na mitano anapitia elimu ya awali
kwa kipindi kisichop
ungua mwaka mmoja kabla ya kujiunga na
elimu-msingi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Philipo Mulugo alithibitisha kwa gazeti hili wiki hii mjini hapa
kuhusu kukamilika kwa rasimu ya kwanza ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2013.
“Ni kweli Sera hiyo imekamilika baada ya
kuandaliwa kwa miaka mitatu. Imepita kwa wadau mbalimbali, mashuleni,
vyuoni na katika taasisi mbalimbali nchini ambao wametoa maoni yao.
“Jumapili (kesho) tunatarajia kuwa waheshimiwa wabunge nao watapata
fursa ya kuijadili na kutoa maoni yao katika semina iliyoandaliwa
maalumu kwao,” alisema Mulugo katika Viwanja vya Bunge.
Alisema baada ya maoni hao ya wabunge,
watapeleka Rasimu hiyo kwa mamlaka husika kwa ajili ya andiko la mwisho
kabla ya kupelekwa katika Bunge lijalo ili itungwe sheria kuhusu Sera ya
Elimu na Mafunzo.
Hata hivyo, semina hiyo huenda
isifanyike kesho kutokana na kuingiliana na ratiba nyingine, kwani
wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakuwa na mkutano na Mwenyekiti
wao wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kwenye Ukumbi wa White House mjini
hapa.
Wiki moja iliyopita, wakati akiongoza
kikao, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwaambia wabunge kuwa makabrasha
waliyokuwa wakipewa na wahudumu ni kuhusu Sera ya Elimu na hivyo waende
wakayasome, kwani kuna siku wataijadili.
Kwa mujibu wa rasimu, mambo mengine
yanayotarajiwa kutekelezwa na Sera ni kuhuisha mitaala ya sasa ya elimu
ili ikidhi muundo mpya wa elimu na mafunzo, kuhuisha sheria na taratibu
mbalimbali za utoaji elimu ili ziendane na muundo mpya wa elimu-msingi.
Kuimarisha mfumo wa usimamizi, ithibati
na udhibiti wa utoaji wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali ili
kukidhi malengo na muundo mpya wa elimu-msingi.
Nyingine ni kuongeza ubora wa
miundombinu katika shule za sasa za msingi ili kukidhi mahitaji na
malengo ya elimu-msingi ikiwa ni pamoja na kuongeza madarasa ya
elimu-msingi katika kila shule ya msingi ya sasa, kujenga maabara za
sayansi na maktaba katika kila shule ya elimu-msingi.
“Kutenga rasilimali fedha za kutosha kwa
ajili ya nyenzo, vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia, vitabu vya
kiada na ziada, maandiko, machapisho ya maktaba pamoja na vifaa vya
maabara,” ilieleza rasimi hiyo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Kuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza katika ngazi ya
elimu – msingi kama lugha za kujifunzia na kuwasiliana.
Kuweka utaratibu utakaohakikisha kuwa
wanafunzi wanaomaliza elimu na mafunzo ngazi husika kwa ufanisi na wale
wanaokatisha masomo au mafunzo yao kwa sababu mbalimbali, wanaendelea na
kuhitimu masomo au mafunzo yao katika mfumo rasmi wa elimu na mafunzo.
Jambo jingine litakalotekelezwa ni kutoa elimu kwa umma kuhusu
madhumuni, malengo na matarajio ya Sera mpya ya Elimu na Mafunzo.
Rasimu ilieleza kuwa mambo chanja
yanayotarajiwa kupatikana baada ya mkakati kutekelezwa ni kuwepo kwa
elimu ya awali ya lazima kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja kabla ya
kujiunga na elimu msingi, kuwepo kwa elimu msingi ya miaka 10 kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne cha sasa kwa watoto wote wenye rika
la kwenda shule.
Matokeo mengine ni kuwepo kwa mfumo
nyumbufu, miundo na taratibu za kujiendeleza katika mikondo anuai ya
kitaalamu na kitaaluma, kuwepo kwa elimu na mafunzo yenye viwango, ubora
na sifa zinazotambulika kitaifa, kikanda na kimataifa.
“Kuwepo kwa fursa mbalimbali za elimu na
mafunzo zinazokidhi mahitaji ya wananchi na ya nchi kiuchumi, kijamii,
kisayansi na kiteknolojia.
“Kuwepo kwa ugharimiaji endelevu wa
elimu na mafunzo na kuwepo kwa mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatia
masuala mtambuka,” ilifafanua Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo.
Kuhusu elimu ya awali, ilieleza kuwa
mkakati ni kuweka vigezo, viwango na taratibu ili elimu ya awali iwe ya
lazima na itolewe katika kila shule ya elimu – msingi, na kuwa sheria,
miongozo na taratibu kuhusu elimu hiyo lazima kuwekwa na kutekelezwa
ifikapo mwaka 2018.
Katika elimu msingi, ni kuwa ya lazima
kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, na kutolewa kwa miaka 10
na umri wa kuanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita
kulingana na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.
Shabaha katika eneo hili ni sheria na
miongozo kuhusu elimu-msingi kuwekwa na kutekelezwa ifikapo mwaka 2016,
mpango wa utekelezaji wa utoaji wa elimu-msingi kuwepo ifikapo mwaka
2018 na elimu-msingi kutolewa ifikapo 2018.
Kwa mujibu wa dibaji ya Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Sera mpya imeandaliwa na
Serikali kwa kushirikiana na wadau ikitilia maanani mafanikio
yaliyoletwa na Sera zilizotangulia na kulifanya Taifa kupiga hatua
katika nyanja za elimu na mafunzo.
AMA KWELI KUISHI KWINGI KUONA MENGI JIONEE MERCEDES S-CLASS INAYO JIENDESHA YENYEWE HAIHITAJI DEREVA
The backrests recline to 45 degrees, the heated seats have an energising massage function and even the armrests can be heated or cooled. But it’s not all about relaxation.
You get working desks in the back, plus two DVD screens which can be linked to the web for connectivity, along with a mega-music system, all of which can be operated from an app on your phone.
There’s even a climate control with air balance and an active perfuming system with four different smells to waft around the cabin!
Also, 115 years after cars were first fitted with electric headlamps, the S-Class is the first car since to have virtually NO lightbulbs — although its 500 LEDs mean it won’t leave you in the dark.
Smooths out potholes ... Mercedes S-Class
It’s a trailblazing, advanced trendsetter for business high-fliers when they are on the ground.
Over the years the car has been the best-selling luxury limo.
Alongside its high-spec standards it has always been at the forefront of technology, a winning recipe which has made it the favourite wheels of executives and politicians.
Gari hili Tayari lipo sokoni UK na Inakadiriwa kuuzwa kati ya £65,000 na £170,000.
Subscribe to:
Posts (Atom)