Facebook Comments Box

Thursday, May 9, 2013

DAVIS MOYES NDIO KOCHA MPYA WA MANCHESTER UNITED KWA MIAKA 6 IJAYO


Hatimaye Manchester United imethibitisha DAVID MOYES ndio atakuwa kocha mpya wa kumrithi Sir Alex Ferguson kwa mkataba wa miaka 6.

Alex Ferguson jana alitangaza kustaafu kuifundisha timu hiyo aliyodumu nayo kwa takribani miaka 27 na akiwa anamtaja mrithi wake wake Fergie alisema: "Wakati tunajadili mtu wa kunirithi wote tulikubaliana kuhusu David Moyes.
"David ni mtu makini mwenye miiko ya kazi. Nimekuwa nikipenda ufanyaji wa kazi yake kwa muda mrefu na niliwahi kumshawishi mwaka 1998 ajiunge nami kuwa msaidizi wangu hapa. Akiwa kijana mdogo na akiwa ndio anaanza maisha yake ya ukocha na tangu wakati huo amekuwa akifanya kazi nzuri na klabu ya Everton.


"Hakuna swali kwamba ana kila ubora ambao tulikuwa tunautegemea kwa meneja mpya wa klabu hii.”- alisema Ferguson.

SOURSE: SHAFFIH DAUDA

PICHA ZA HUKUMU YA SHEIKH PONDA


Kama kawaida walikuwepo pia!

Akiwa na furaha baada ya hukumu yake kumalizika leo katika mahakama ya kisutu jijini dar es salaam
Akiteta jambo na baadhi ya watu!
Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge  (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.

Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waislam nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.
Tutatoa tamko!
Kuna mengi yamejitokeza na wale waliokuwa wakiogopa sasa wamepata somo!

Safari ikaanza!


Akapewa ulinzi tena!

Akaingia kwenye gari!

Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa gari lake kulisimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito kwenye mataa ya Maktaba Squire. 

Wafuasi wakajimwaga barabarani!

Takbirrrrrrrrrr!Allahu Akibarrrr!

Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wagari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.
Walifukuza msafara huo hadi pale ulipotokomea!

Wananchi bado wakiwa na hamu ya kumuona mdai haki na kiongozi wao

Mpaka wamuone kiongozi wao
Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kubwa
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja ya muumini mwenzao ambae alishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.


Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.

Tumewashinda!




Furaha!
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!


Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.
Hoyoooooooooo!




Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia ndugu yake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.


Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia!




Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.


Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa.
Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu!






NIMEAMUA NISEME: HOTUBA YA KAMBONA YA 1966 NI SULUHISHO KWA CCM YA SASA (SEHEMU YA KWANZA)

Na Abukhayrat Hassan ka`bange
Habari za mishughuliko na mihangaiko ndugu zangu watanzania. Nikiwa katika mihangaiko ya kutafuta nini cha kusoma ili kushibisha akili zangu nikafanikiwa kupekuwa na kukutana na kitabu ambacho kimeandikwa ikiwa ni hutuba ya Marehemu Oscar Kambona akilihutubia bunge la Julai 14 mwaka 1966 ikielezea uongozi na misingi ya Tanu.Kitabu hiki kimepewa jina la UONGOZI BORA. Nikajiuliza kwanza kwanini kimeitwa jina hilo. Kikawa kimenivuta kukisoma. Niliyoyasoma nikajiuliza Je, wana ccm wa sasa kitabu hiki hawakijui? Au hiki kitabu wao hawana? Inakuwa vipi kama mimi kapuku tu nisiye husika na siasa kwa namna hiyo ya hao wanao jiita wanasiasa ninacho katika marundo yangu hapa ambayo mimi mwenyewe nayaita kwa jina zuri SHAJALA. Mfumo wa hotuba ulikuwa hivi:
KAMWE TUSISAHAU TANU:
Hapa Marehemu Kambona alikuwa akiwakumbusha wabunge kuwa wasiisahau TANU kwakuwa ndio iliyo wasababisha wakawa hapo bungeni na ndio chama kinacholeta misingi ya amani na umoja kwatika nchi. Na ileweke kuwa wao kama wanatanu watiifu ndio sababu iliyowafanya wawe hapo.Mtu mmoja mmoja binafsi sio jambo kubwa lakini wote kwa pamoja chini ya uongozi wa TANU ni jambo kubwa zaidi.
Kwenye CCM ya sasa tunaona hamna uwote kumeingia umimi,usisi,ukanda na mbaya zaidi udini kila mtu anataka lake hili ni moja linalo bomoa chama.

TUSIWEKE UBINAFSI MBELE:
Marehemu Kambona alilisema hili na kulikemea akaeleza kuwa ikiwa wanachama wa TANU wataleta ubinafsi chama kitadhoofika na hatimae kufa aliwanasihi wanachama wasiingiliwe na moyo huo wa ubinafsi.Viongozi hawawezi kutekeleza kazi zao bila ushirikiano wa wananchi. Na hawezi kushirikiana bila kujua utaratibu wa uongozi wa chama
Hili silisemei nani asiyejua ubinafsi ulivyotawala chamani leo?
TANU NI CHAMA CHA WATU:
Marehemu Kambona alielezea dhahiri bila kuficha kuwa TANU ni chama cha watu na watu hao wanaanzia katika ngazi za kijiji. Kwahiyo kama chama kinataka kuimarika inatakiwa chama kiimarike kuanzia vijijini ambako ndiko wanakokaa watu wengi. Hapa alikemea vilevile ubabe na utemi wa viongozi wa vijijini.
Kwa sasa vijiji tunavitenga kabisa hebu angalia bajeti tu ya maji vijijini ambako ndiko kunakadiriwa kuwa na watu zaidi ya asilimia themanini wanapewa kidogo kuliko asilimia ishirini ya mijini. Chama kinajenga hapa au kinabomoa?

VIONGOZI TUSHIRIKIANE-TUSIKOMOANE:
Marehemu Kambona alielezea kwa makusudi kabisa kuwa sehemu yenye maendelea ni ili ambayo viongozi wake wameshikamana wao kwa wao na wanachi. Wakianza migogoro wataunda makundi ambayo mwisho wake ni mbaya kwa chama. Alitoa suluhisho la kiongozi mwenye matatizo alisema apelekwe kwenye Halmashauri ya chama akajadiliwe na arekebishwe. Kumkomoa kiongozi mwenzio ni kubomoa nchi na kukiharibu chama
Tukiangalie chama chetu leo makundi yamekuwa mengi. Kukomoana kumezidi, Kiongozi mwenzio akikosea sehemu maalumu kwako kumsemea ni kwenye mitandao ya kijamii au magazeti

TUWAPENDE WANYONGE:
Hapa marehemu alijiaminisha kuwa viongozi wote wa TANU lao ni moja kuhakikisha hali ya mnyonge inainuliwa.Na akiasa viongozi washikamane katika kada mbalimbali kulifanikisha hilo. Alionya pia viongozi wanaotumia kadi za TANU kama hirizi zipo kwa ajili ya kutishia watu. Ukija anakuonesha kadi ya chama halafu anairudisha mfukoni wakati matendo yake ni kinyume na chama.
Tukiangalia chama sasa Je, viongozi wote wana dhamira ya kuinua hali za wanyonge? Vipi hawa wanaotumia vyeo vya vyama na kadi za chama kama hirizi. Kuna ofisi unakuta mtu kaweka picha kapiga na rais ukutani ili kuwatisha watu.

Itaendelea.......

SAKATA LA BOMU KANISANI: SERIKALI YA SAUDI ARABIA YASEMA RAIA WAKE WAMEKAMATWA KIMAKOSA

Serikali za Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE) zimezungumzia kukamatwa kwa raia wake, ambao wanahusishwa na tuhuma za kurushwa kwa bomu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Viongozi wa Serikali walikaririwa wakisema wageni waliokamatwa raia watatu ni wa Saudi Arabia na mmoja wa UAE ambao walikamatwa wakati wakiondoka nchini kupitia Namanga.
Balozi wa Saudi Arabia
Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Momina alikaririwa na mashirika ya habari ya kimataifa akikiri kukamatwa kwa raia wa nchi yake na kusisitiza kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumhusisha na shambulizi hilo kwani alikuja Tanzania kutalii.
Momina alisema alikutana na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kinachochunguza suala hilo kwenye kituo cha polisi anaposhikiwa raia wake akitaka kujua kama mtu wao amewekwa vizuri.
“Tuna matumaini makubwa kuwa wataachiwa na tutaendelea kufuatilia suala lao hadi tuone mwisho wake,” alisema Balozi huyo na kusisitiza kwamba hawaondoki Arusha.
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya UAE, kupitia mtandao wa Twitter ilieleza kuwa inafuatilia kwa karibu suala la raia wake watatu waliokamatwa. Ilisema walikuwa wanafanya kazi kwa karibu na ubalozi wa nchi yao huko Tanzania ili kufahamu hatima ya watu wao.
UAE imesema inapinga kwa nguvu zote vitendo vya ugaidi na iko tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania juu ya raia wake kuhusishwa na tukio hilo.
Na afisa mkubwa wa serikali ya Abu Dhabi anasema raia wake walikamatwa kimakosa na amesema mamlaka ya UAE wamepokea ripoti kutoka kwa wanaochunguza tukio hilo kuwa hamna uhusiano kati ya ulipuwaji wa bomu hilo na raia wake hao walio kamatwa. Na aliongeza kuwa wanasubiri raia wao waachiwe ili waweze kuwapokea nchini kwao.
 Sourse: GULF NEWS


SHEIKH PONDA AFUNGWA KIFUNGO CHA NJE

Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam,imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya na Taasisi za KiislamTanzania Shekhe Ponda Issa Ponda,huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru. Katika hukumu hiyo Sheikh Ponda anatakiwa asituhumiwe/asifanye kosa jingine lolote kwa miezi sita. Na ikitokea akifanya hivyo hukumu hiyo itahamishiwa kwenye hukumu halisi kwa maana ataenda jela kwa muda uliobaki.

Hali ilivyokuwa wakati wa hukumu





KASISI ALIETUHUMIWA KULAWITI AJIUA

KENYA-- Padri  wa kanisa Katoliki amekutwa amekufa baada ya kujiua leo asubuhi katika eneo la Turkana siku moja baada ya kufikishwa katika mahakama ya Lodwar kwa madai ya kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Mwili wa John Manzi ulipatikana ukining’inia katika makazi ya mapadri dayosisi ya Lodwar Jumatano, siku moja baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya KSh100,000 na kaimu hakimu mwandamizi Harrison Barasa.

Afisa mkuu wa polisi Turkana Kati  John Onditi,  alisema maiti ya kasisi huyo ilipatikana ikining’inia nyumbani kwake Jumatano asubuhi.

Upande wa mashitaka ulikuwa umedai kuwa padri huyo alimshawishi mvulana huyo mwenye umri wa miaka 18 nyumbani kwake Ijumaa usiku ambapo walipata vileo kabla ya kutekeleza kitendo hicho mwathiriwa akiwa amelewa.

Mwanafunzi huyo aliamka asubuhi na kugundua kuwa padri huyo alikuwa amemlawiti kabla ya kupiga ripoti polisi akiwa ameandamana na mzazi wake.

Marehemu kisha alijisalimisha mwenyewe kwa kituo cha polisi cha Lodwar baada ya kudokezewa kuwa mvulana huyo amepiga ripoti polisi.

Kuachiliwa

Tukio hilo liliibua maswali miongoni mwa waumini wa kanisa hilo na makasisi wengine waliojazana katika kituo hicho cha polisi wakimtaka padri huyo awachiliwe.

Daktari aliyemchunguza mwathiriwa alithibitisha kuwa matokeo yake yanaambatana na madai ya mvulana huyo ya kulawitiwa. Vile vile, madaktari walisema kuwa mvulana huyo anapokea ushauri hasa baada ya kutatizwa sana na tukio hilo.



MAHAKAMA YA RUFAA YAMREJESHEA UBUNGE DR DALALY PETER KAFUMU (CCM)

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania imemrejeshea ushindi wa kiti cha Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Igunga, Dk Dalaly Peter Kafumu (CCM).
 
Dk Kafumu Dalaly Peter Dk Kafumu Awali, ushindi wa Dk Kafumu (kura 26,428 kati ya kura zote halali 53,672) ulikuwa umetenguliwa baada ya mgombea wa CHADEMA, Mwl Joseph Kashindye (aliyepata kura 23,260) kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka 2011 baada ya aliyekuwa akishikilia kiti hicho, Rostam Aziz (CCM) kujiuzulu Julai ya mwaka uo huo. Mwezi uliopita, Mahakama ya Rufaa iliketi na kukamilisha kusikiliza rufaa ya kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ikipinga uamuzi uliomnyang’anya ushindi Dk Kafumu. Wakili wa Serikali, Gabriel Malata, katika hoja zake za kutaka uamuzi wa Mahakama Kuu utenguliwe, amedai kuwa jaji aliyesikiliza kesi hiyo, alikosea kuanza kuisikiliza kwa kuwa mlalamikaji hakutimiza matakwa ya kisheria. Malata alidai kuwa mlalamikaji hakulipa ada ya Mahakama Shilingi milioni moja alizotakiwa kutoa au hati ya nyumba, kabla kesi hiyo haijaanza kusikilizwa kama Sheria ya Uchaguzi inavyoelekeza. Aliendelea kudai kuwa mjibu rufaa, aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi huo, Joseph Kashindye, na wenzake hakutekeleza sharti hilo na hivyo usikilizwaji wa shauri hilo, pamoja na mwenendo mzima wa kesi ni batili. Wakili huyo amedai kwamba malalamiko yaliyopelekwa Mahakama Kuu ni ya kutengeneza, kwani hayajawahi kuwasilishwa katika Kamati ya Maadili ya Uchaguzi, kama ilivyofanyika katika suala la Mbunge wa Tabora mjini, Ismali Aden Rage, ambaye alitozwa faini ya Sh laki moja kwa kutembea na silaha kwenye mkutano. Hoja hizo zilipingwa na wakili wa Kashindye, Profesa Abdalah Safari, ambaye aliitaka Mahakama ya Rufaa, kutupilia mbali hoja hizo. Profesa Safari alidai kwamba Mahakama Kuu iliyosikiliza kesi hiyo, iliridhika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ndipo ikaridhia kutengua matokeo. Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa chini ya uenyekiti wa Jaji Nathalia Kimaro, akisaidiana na Jaji William Mandia na Jaji Semistrocles Kaijage, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, waliahidi kutoa uamuzi wao mara baada ya kupitia kwa undani mwenendo mzima wa shauri hilo. Mahakama Kuu ya Tanzania ilitengua matokeo ya uchaguzi huo, baada ya kubainika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura. Jaji Mary Nsimbo Shangali wa Mahakama Kuu, alitangaza kutengua matokeo hayo, baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji kati ya hoja 17 zilizowasilishwa katika mahakama hiyo.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU