Kumetokea
 ajali mbaya mida hii maeneo ya Jeti Lumo mwisho wa lami ambapo gari 
kubwa la mizigo limeangua daladala iliyokuwa kituoni.
 Ajali 
hiyo imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa 
lami ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.
 Mtoa taarifa wangu amesema hali ni mbaya na bado hajajua idadi ya vifo na majeruhi ujumla.Pia gari imepondeka sana jambo ambalo linaashiria hatari zaidi.
 Kuna gari la kunyanyua makontena limeshafika pale lakini limeshindwa 
kutoa msaada wa uhakika kutokana na kuzidiwa uzito na kontena ambapo 
likijaribu kunyanyua kontena ushuka.
Hamna mtu yoyote aliepoteza maisha maana Hiace hiyo ilikuwa imepaki kusubiri muda wake wa kupakia abiria.



