Facebook Comments Box

Saturday, May 3, 2014

WARIOBA NI "BWANA KERO" KWA SERIKALI TOKEA ZAMANI

Kama alivyoandikika Edson Kamukana katika makala yake moja
"ukiachilia mbali wasomi kadhaa walioamua kulamba matapishi
yao na kumtusi Jaji Warioba na wana-CCM wengi wanaotukana
bila kujua wanamtusi nani, katikati yake utaona wanaosalia si bure
wana jambo na sababu za kufanya hivyo, hawa bila shaka
wanalipa kisasi."
Mnamo tarehe Julai 17, 1997, Rais Mkapa alimteua Jaji Warioba
kuongoza Tume ya Rais (Warioba Commission) kuchunguza na
kubainisha mianya na vyanzo vikuu vya rushwa nchini. Baada ya
kufanya mapitio ya sheria, kanuni na taratibu ndani ya serikali na
kuonyesha mianya ya kukua na kuongezeka kwa rushwa nchini,
Tume ya Warioba ilichapisha ripoti yake (Ripoti ya Warioba) tarehe
7 December 1997.
Baadhi ya mambo ambayo Tume ya Warioba iliyakuta ni pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa umma kuchukua rushwa kama
sehemu ya kujazia mishahara yao (petty corruption) midogo.
Lakini pia Tume ya Warioba ilikuta kuwa kulikuwa na rushwa
nyingine (grand corruption) aka ufisadi iliyohusisha maafisa wa
ngazi za juu na baadhi ya wafanyakazi wa serikali walio na ulafi wa
kujilimbikizia mali.
Tume ya Warioba ilitoa mapendekezo ya hali ya juu yaliyogusa
wizara na idara zote za serikali. Ripoti ya Warioba iligusa mioyo ya
walalahoi na wengi waliotoa maoni ya kumtaka Rais Mkapa
awafikishe mahakamani wale wote waliohusishwa na ufisadi
kwenye Ripoti ya Warioba. Hata hivyo, ripotii hiyo iliwekwa
kabatini na kutiwa kofuli. Ripoti ya Warioba ni imekuwa adimu
sana kupatika ilivyokuwa kwa Hati ya Muungano.
Japokuwa ripoti hiyo iliwekwa kabatini, iliwagusa moja kwa moja
vigogo kadhaa hasa wa CCM na wengi wao au watoto, ndugu na
jamaa zao ndio wanaoshika madaraka leo. Kama mnakumbuka
baada ya ile ripoti, ndipo vyombo vya habari vilianza kuripoti
masuala ya rushwa, ikiwemo ile skendo ya IPTL iliyomfanya
Mwalimu Nyerere aseme kuwa "kama huu ndiyo ushirikiano wa
nchi za kusini, basi bora ukoloni urudi." Waliounga mkono au
kuipinga IPTL wanajulikana. Wengine mtakuwa mnawakumbuka
hata watawala wa miaka hiyo na wizara/idara walizokuwa
wanaziongoza.
Akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Mei 13, 2008, Jaji Warioba
alisema kuwa "Baadhi yetu tumepiga kelele muda mrefu kuhusu
hali ya rushwa nchini mpaka ikafika mahali ikawa watu wanatoa
dhihaka tu. Kuna rafiki yangu mmoja, yeye alinipachika jina la
‘Bwana Kero’ kwa sababu ya taarifa ile ya Tume ya Kero ya
Rushwa. Alisema mimi nimegeuka kuwa kero kwa kuzungumzia
rushwa kila wakati." Bado anaendelelea kuwa "Bwana kero" kwa
kutetea Rasimu ya Katiba Mpya.
Kama alivyouliza Edson Kamukana, inawezekana kweli hao vigogo
au watoto wao, ndugu na jamaa zao walioguzwa moja kwa moja
na ile ripoti wakamsifu "Bwana Kero" wakati alishawaharibia
kitumbua chao? Hatuoni vigogo hao wanautumia mchakato
mzima wa Katiba mpya kama mwanya pekee was kumdhoofisha
"Bwana Kero" na kujaribu kuendelea kuficha madhambi yao
yaliyoyafichuliwa na "Bwana Kero" kwenye ile ripoti yake ya kero
za rushwa 1997?
Kwa wale ambao hawakuwahi kuisoma Ripoti ya "Bwana Kero"
itafuteni muisome halafu muone "kero" ambazo "Bwana Kero"
aliziodhoresha kwenye ripoti yake. Halafu muunganishe the dots
kwa kujiuliza ni kwa nini kigogo A na B au mtoto/ndugu/jamaa wa
Kigogo C "anakereka" sana mpaka kumtusi "Bwana Kero"? Mara
ya mwisho nilisoma muhtasari wa ripoti kwenye maktaba ya
HakiElimu. Ilikuwa imejaa vumbi kweli kweli. Inaitwa " The Report
of the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption",
kwa kifupi "The Warioba Report".
CHANZO: JAMII FORUM


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU