Wednesday, September 5, 2012
EWURA YAPANDISHA TENA BEI YA MAFUTA
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya petroli na mafuta ya taa zimepanda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo jana bei mpya zitaanza kutumika kuanzia leo.
Sambamba na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye soko la Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012.
Petroli imeongezeka kwa sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50 Dizeli imeongezeka kwa Sh 199 kwa lita sawa na asilimia 10.26 na mafuta ya Taa Sh 67 kwa lita sawa na asilimia 3.63
Ameeleza kuwa kampuni zipo huru kuweka bei inayotaka kulingana na ushindani ilimradi isivuke bei elekeze ya mamlaka hiyo (EWURA)
MKUU WA MKOA WA TANGA AMKAMATA MWENYEKITI WA KIJIJI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA RASILIMALI ZA TAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama katika mpaka wa Tanzania na Kenya |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiangalia magunia ya mkaa ambayo yapo tayari kusafirishwa kupelekwa nchi ya Kenya katika kijiji cha Mwakijembe |
Askari akimsindikiza mwenyekiti wa kijiji Ngd Fransis Mtambo kwenda kumuaga mkewe |
Subscribe to:
Posts (Atom)