Facebook Comments Box

Saturday, October 26, 2013

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA OFISI ZA AZAM TV


Waandishi wa Habari wa vituo mbali mbali vya Televisheni pamoja na magazeti wa hapa Jijini Dar es Salaam  siku ya Jumamosi tarehe 26/10/2013 walipata fursa ya kutembelea ofisi za Azam Tv zilizopo Tazara.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media, Rhys Torrington akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Rhys Torrington akionyesha King'amuzi cha Azam TV kwa baadhi ya Waandishi wa habar.
Baadhi ya Wakuu wa vitengo mbalimbali vya kampuni ya Azam media wakimsikiliza Mkurugenzi wao.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Azam Media, Loth Mziray (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya Waandishi wa habar.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Azam Media Kitengo cha huduma kwa Wateja wakiwajibika.
Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media, Mehboob Al-Addad akionyesha moja ya mixer za sauti zilizopo ndani OB Van ya Azam TV ambayo ni ya kisasa na yenye vigezo vya kimataifa.
Wazee wa Kazi ndani ya OB Van la Azam Tv,toka kulia ni Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media, Mehboob Al-Addad, Meneja wa Azam FM na Matukio ya Moja kwa Moja,Yahya Mohamed pamoja na Fundi Mitambo wa OB Van hiyo, Saleh Mansoor aliyekaa wakifatilia moja ya kazi zao.

 OB Van ya Azam Tv



DAWA BARIDI ZATUMIWA KAMA DAWA ZA KULEVYA

Picha na Maktaba:

Matumizi ya dawa za kulevya nchini yamechukua sura mpya, baada ya kubainika kuwa watumiaji wengi wa dawa hizo aina ya heroin na cocaine sasa wanatumia dawa za hospitali zenye uwezo wa kulevya kuwa mbadala.
 
Watu wanadhani dawa za kulevya ni heroin na cocaine pekee, lakini vijana wanavuta petroli, gundi, dawa za maumivu na za kifua ambazo zina codeine, vyote hivi vinaathari,”    
 
Matumizi hayo mabaya yamebainika kutokana na kuwapo ongezeko la matumizi ya dawa za hospitali zilizo na nguvu inayoelezwa kulingana na dawa za kulevya zikiwamo heroin, cocaine na amphetamine.
 
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu na Dawa za Kulevya (UNODC) ya mwaka 2013, inathibitisha ongezeko hilo la matumizi ya dawa hizo, ambazo kitaalamu zinaitwa ‘new psychoactive substances (NPS).
 
“Dawa mbadala za dawa za kulevya zimezua wasiwasi mkubwa siyo kwa sababu ya ongezeko la matumizi yake, bali hata ukosefu wa utafiti wa kisayansi na uelewa wa matumizi yake,” ilisema sehemu ya ripoti ya UNODC.
 
Katibu Mkuu UNODC, Yury Ferdotov alieleza katika ripoti hiyo ya hali ya dawa za kulevya mwaka 2013 kwamba, changamoto kubwa iliyopo katika kudhibiti dawa hizo duniani ni matumizi ya dawa za hospitali na kemikali zinazotumika kuzitengeneza kutumika kama dawa za kulevya.
 
 Alisema nchi nyingi duniani hazina sheria wala uelewa kuhusu kemikali hizo, jambo linalosababisha wafanyabiashara wakubwa kuendelea kusafirisha kemikali hizo au kutumia teknolojia kulima mimea inayotumika kutengeneza dawa hizo.
 
UNODC limefafanua kuwa matumizi mabaya ya dawa hutokea wakati dawa za hospitali zinapotumika kwa malengo mengine kinyume na tiba.



DIAMOND PLATNUMZ AVAMIWA AKIWA MLIMANI CITY


Msanii Naseeb Abdulmalik 'Diamond'Akiwa katika harakati za hapa na pale kutafuta vitu vyake binafsi kundi kubwa la wanafunzi lilikuja na kumvamia huku wakiomba sign ya msanii huyo na wengine wakitaka kupiganae picha.
   










 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU