Facebook Comments Box

Wednesday, October 9, 2013

HILI NDIO GARI LA MTOTO WA BAKHRESA LENYE THAMANI YA MILIONI 805

                             Gari aina ya Brabus ambayo inayomilikiwa na mmiliki wa klabu ya Manchester City ya England, imeonekana leo Dar es Salaam, lakini ni mali ya Yussuf Bakhresa, mtoto wa bilionea Mtanzania, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa. Vyanzo vimesema Yussuf alitoa oda maalum kutengenezewa gari hili na thamani yake jumla si chini ya dola za Kimarekani 500,000 sawa na shiingi milioni 805 za kibongo.

Hii hapa mali ya Yussuf Bakhresa

Huyu jamaa ndiye anayeendesha gari la hili la mtoto wa Bakhresa

Angalia alivyotulia ndani ya mzigo wa dola 500,000

Ni oda maalum kwa ajili ya Yussuf Bakhresa 



Mwingine mwenye gari kama hii Dar es Salaam nani? 

Kutoka Manchester hadi Dar es Salaam


SOURCE: BIN ZUBEIRY

HIZI NDIO KAULI ZA WANASHERIA WANAO MPINGA TUNDU LISSU KUHUSU KATIBA MPYA

Baadhi ya wanasheria wameunga mkono utaratibu wa  Rais kutia saini Muswada wa  Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, uliopitishwa hivi karibuni na Bunge kwa hoja kwamba umepitia   mchakato sahihi na halali wa Kikatiba.

Wanasheria hao wakaeleza kumshangaa mwanasheria mwenzao na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), kwa ushauri wake alioutangaza kwa umma, kumtaka Rais asisaini muswada huo, kwamba ushauri huo ni wa 
kisiasa zaidi, usio na tija kwa uongozi wala unaofuata utaratibu na sheria.

Wamenukuliwa wakizungumza na mwandishi kwa nyakati tofauti jana, wakisema kuwa muswada huo kama ilivyo miswada mingine ya sheria, una nafasi ya kusainiwa na yakiwepo marekebisho, unarudishwa bungeni kujadiliwa na kurekebishwa.

Wakili wa kujitegemea, John Mapinduzi alisema: "Lazima muswada huo usainiwe ndipo urudishwe bungeni kwa marekebisho, Lissu ni mwanasiasa tu anapotosha umma… sasa utarudishwaje bungeni wakati ulishapita?" Alihoji Mapinduzi.

Mwanasheria mwingine wa kujitegemea, Jerome Msemwa alisema kusainiwa muswada huo ni njia sahihi na inafanyika mara nyingi (??) na kama kuna marekebisho, yanafanyika baadaye: "Wabunge kama Lissu waliamua kutoka wenyewe bungeni wakati muswada unajadiliwa… hakuna aliyewafukuza, sasa iweje leo watake usisainiwe? Haina maana leo hii kumshauri Rais kutosaini. Ushauri wa Lissu, kisheria hauna maana yoyote, hawezi kumshauri Rais leo asisaini wakati anafahamu kuwa hata baada ya kusainiwa, kuna nafasi ya kurudishwa bungeni na kujadiliwa kwa marekebisho yoyote," alisema Msemwa.

Msemwa alisema Rais asiposaini muswada huo na kuurudisha bungeni, maana yake vikao vya wabunge vilivyokaa Dodoma  kujadili muswada huo, vilipoteza muda na fedha za wananchi bure.  --- via HabariLeo


MISHAHARA YA WAZIRI MKUU, MAWAZIRI NA RAIS WATAJWA

Picture
Zitto Kabwe: "Siku ya Nne ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetupeleka Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora. Nikiwa na Wenyeviti wa chama wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora pia Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi Ndg. Mambo tumefanya mikutano 4."
Mishahara ya Viongozi wa Umma lazima iwe wazi kwa umma. Sheria za Mishahara ziweke wazi kabisa kuwa mishahara hii itakuwa wazi na itakatwa kodi. Juzi Mpanda nimewaambia wananchi Mshahara wa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa mwezi. Nikiwa Igunga mnamo tarehe 13 Oktoba tutawaambia wananchi mshahara wa Rais na Makamu wa Rais. Iwapo Rais wa marekani mshahara wake na mapato yake ni wazi na unakatwa kodi, iweje Rais wa nchi ndogo kama Tanzania. Wameifungia Mwananchi kwa kutaja viwango vya mishahara ya watumishi wa Umma. Wamfungie Mbunge kama wanaweza. --- Zitto Kabwe.
Akizungumza katika mkutano wake mjini Mpanda jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe  ameutaja mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  kuwa ni jumla ya shilingi milioni 26 pasipo
kukatwa kodi. Akichanganua alisema Pinda anapokea sh. mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya Waziri na kiasi kinachosalia  kufikia sh mil. 26 kwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa Waziri Mkuu pia siku zijazo nitataja na wa Rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza. (nukuu kutoka TanzaniaDaima)


ANGALIA DIAMOND ALICHOSEMA KUHUSU KURUDIANA KWAKE NA WEMA


Diamond akimkiss Penny kuonesha mapenzi yao
Katika siku za hivi karibuni katika magazeti mbali mbali ya hapa Bongo pamoja na mitandaoni kumekuwa na habari inayosema kuwa Naseeb Abdulmalik "Diamond" amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye aliachana nae kutokana na mwana dada huyo Wema  Sepetu kukosa uaminifu katika mapenzi yao.
 
Taarifa zaidi zilisema kuwa Wema na Diamond walikutana Dubai wakati Diamond akienda Indonessia na Wema akielekea Hong kong na kula bata sana tu na kuashiria kuwa wamerudiana.
 
Lakini Diamond ameeleza kwenye Blog yake This is Diamond habari yote kama ifuatavyo:-
 
"Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana 
Mitandaoni na Kwenye Media tofauti... kwamba mimi na Mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu
 ambacho Sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?..
 
Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana
 
Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania na si kuwekeana chuki zisizo na faida.." alisema Diamond.
Diamond akiwa na Penny



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU