Facebook Comments Box

Tuesday, June 18, 2013

MBUNGE JOSEPH MBILINYI (SUGU) APATA AJALI LEO



Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali hivi punde katika eneo la kasheki wilayani Hanan'g akielekea Arusha mjini.

Joseph Mbilinyi maarufu Sugu alikuwa akielekea Arusha mjini kuungana na wabunge wengine katika shughuli ya ku
aga marehemu waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita.  

Katika ajali hiyo hakuna mtu yoyote amejeruhiwa, Mbunge huyo yuko salama, gari la Sugu limeharibiwa vibaya baada ya kugongana na basi la abiria.


HIZI NDIO SABABU ZA POLISI KUTUMIA MABOMU KUTAWANYA WATU ARUSHA LEO JIONI


Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo  limeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao
 
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu

Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa  mabumu yalianza kusikika.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee


UPDATE YA VURUGU ZA ARUSHA LEO







Tundu Lissu na Mustafa Akunai wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa sasa.Hii ni taarifa toka kwa kamanda wa mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas akihojiwa na radio ya hapa jijini radio Sunrise fm..Kamanda Liberatusi amesema makosa ya Wabunge hao ni haya:

Mkusanyiko usio rasmi

Kufunga barabara

Kuwashambulia polisi

Kamanda amesema watashikiliwa na jeshi la polisi mpaka uchunguzi utakapo kamilika.Hilo ndilo linaloendea mpaka sasa.Hizi ni habari sahihi zilizotolewa na kamanda wa mkoa huu wa polisi Liberatus Sabasi.


VIDEO: MTANZANIA ALIEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MISRI AKIHOJIWA

Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita habari zilisambaa kwamba binti Mtanzania aliekamatwa na dawa za kulevya nchini Misri angenyongwa siku za karibuni kutokana na hizo dawa alizokamatwa nazo.
millardayo.com baadae ilimpata balozi wa Tanzania Egypt ambae alikanusha taarifa za kunyongwa na akakubali kwamba kweli kuna Watanzania wawili wamekamatwa ambao ni huyo msichana na ndugu yake wa kiume ambao ni wakazi wa Magomeni Dar es salaam na kwamba wanashikiliwa na polisi huku wakisubiri kesi yao.
Leo hii, kitongoni.blogspot.com inakupatia nafasi kuona video ya mahojiano ya TV na msichana huyu ambae anadai alikwenda Misri kumtafuta binamu yake, begi alilokamatwa nalo ni lake ila alikua hajui kama lina dawa za kulevya.


VIDEO: AY AKIHOJIWA KWENYE STUDIO ZA BBC WORLD




RIPOTI YA MABOMU YALIYOPINGWA ARUSHA LEO

.
Arusha.

Maripota wawili wa millardayo.com kutoka Arusha wanaripoti kwamba mabomu ya machozi yakipigwa na Polisi yameanza kusikika toka saa kumi jioni kwenye eneo la Soweto.
Mmoja wa maripota hawa amesema wakati alipokua karibu na mkusanyiko huo kuna Askari Polisi mmoja ambae alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa kwa mabomu na kufariki June 15 2013 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Baada ya hapo hawa Wafuasi hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka kama kutoelewana huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa huku pia Viongozi wa Chadema wakihutubia…. ndio mabomu yakaanza kusikika.
Ripota wa pili anasema “Baada ya Tundu Lissu wa Chadema kuhutubia na kusema chanzo cha vifo vya June 15 2013 ni Polisi, yani vifo hivyo viliratibiwa na RPC Arusha… mabomu ya machozi ndio yakaanza kulipuliwa”
Mpaka saa kumi na moja na dakika 40 hii post inaingia hapa, wafuasi wa Chadema bado wako maeneo ya Soweto Arusha, wamegoma kuondoka na kusema wanataka kujua kwanza usalama wa Viongozi wao…. lakini pia mabomu yanaendelea kusikika kwenye sehemu nyingine kama Sanawari, Arusha mjini, Mianzini na maeneo mengine.
 
 
 
SOURSE: MILLARD AYO


TAHADHARI: UGONJWA WA 'DENGUE' WAINGIA JIJINI DAR ES SALAAM


Kwa wale wafuatiliaji wa habari za magazetini, mtakuwa mmesikia kuhusu kuzuka kwa ugojwa uitwao "Dengue fever" ama kwa kiswahili huitwa Homa ya Dengue.

Habari zinasema kwamba tayari watu ishirini wameshathibitika kuwa na tatizo hili na tayari wako hospitali. Juma lililopita, ugonjwa huu uliua watoto wapatao 6 katika Wilaya ya Ilala na ikasemekana kwamba ni 'Malaria kali' lakini baada ya sampuli za damu kupimwa zaidi ilionekana walikuwa na homa ya dengue!

Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum. Na mbu hawa hupatikana kwenye Maji masafi yaliyoachwa wazi hivyo wananchi mnatahadharishwa kuhakikisha maji masafi yanafunikwa ili kuepuka mazalio ya Mbu hao.

Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida

  • homa kali zaid ya 40 degrees
  • maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
  • maumivu ya viungo na misuli
  • harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu

TIBA:

HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.

Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol. Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi. 
kwa mgonjwa ambaye ana shock yani kutetemeka au ana hali mbaya sana basi ni bora awahi hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha yake.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU