Facebook Comments Box

Monday, February 25, 2013

ANGALIA LIVE HAPA MDAHALO WA MWISHO WA WAGOMBEA URAIS WA KENYA

Live Video streaming by Ustream

MDAHALO WA MWISHO WA WAGOMBEA URAIS KENYA UMEANZA



Mdahalo wa mwisho wa wagombea wa uchaguzi nchini Kwenya unafanyika jioni ya leo.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mgombea wa Urais Uhuru Kenyatta alikuwa amesusia mdahalo huo akidai kuwa mdahalo wa kwanza waliokuwa wanauendesha mjadala wenyewe waliangazia sana swala la ICC na kuwafanya wagombea wengine kumlemea.
Duru zilisema kuwa Uhuru alisitisha kampeini zake leo ili kuweza kujiandaa vilivyo kwa mjadala huo.
Wagombea wengine akiwemo waziri mkuu Raila Odinga wanajiandaa kwa mjadala huo ambaop hii leo utalipa kipao mbele mbele swala la ardhi, sera za kigeni, na uchumi.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa asilimia tisini ya wapiga kura wanaona mjadala huu una manufaa kwa wakenya. Asilimia themanini na tano walisema wako trayari kutazama mjadala huo.
Asilimia robaini ya wapiga kura waliohojiwa punde baada ya mjadala wa kwanza walisema wangempigia kura Uhuru Kenyatta wakati asilimia 33 walisema wangempigia kura Raila Odinga.Wawili hao ndio wagombea wakuu katika uchaguzi huu.



RAGE AKATAA KUJIUZURU ILA ASEMA MAAMUZI YATAKAYOFUATA NI MAGUMU

Mh Aden Rage akiwa amependeza katika rangi za kijani na njano
Na Dina Ismail
KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba inatarajiwa kutoa uamuzi mgumu kuhusiana na mwenendo mbaya ulionayo timu hiyo katika ligi kuu ya Vodacom.
Aidha, Rage amekanusha taarifa za kujiuzulu kwake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema kwamba kamati ya utendaji ya Simba ilitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya kujadili mustakabali wa timu yao.
Alisema kikao hicho kitajadili kwa kina hali iliyopo sasa ambayo imesabababisha timu yao kupoteza hata matumaini ya kutetea ubingwa wao.
“Tutakuna baadaye leo na kujadili hali hii maana tukiiacha hivi hivi inaweza kutuletea madhara makubwa sana…pia tutatoa maamuzi mazito baada ya kikao chetu,”alisema.
Kuhusu na taarifa za kujiuzulu kwake, Rage alisema anashangazwa na taarifa hizo zinapotoka kwani kama atafikia uamuzi huo ataitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia hatua hiyo.
“Mimi sijasema nitajiuzulu jamani hata hiyo taarifa yenyewe ukiisoma haileweki, hivyo nawaomba wanasimba kutulia kuona kipi kitakachofuata,”aliongeza Rage
Simba imeonekana kusuasua sua katika ligi hiyo baada ya kutokuwa na matokeo ya kuridhisha sambamba na kuamulia vipigo katika mechi zake.
Hali hiyo ilianza kujitokeza tangu mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambao ulipelekea kutoka kileleni hadi kushika nafasi ya tatu.
Aidha, tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, Simba imeshinda mechi mbili dhidi ya African Lyon 3-1 na Tanzania Prisons 1-0, huku ikitoka sare mbili dhidi ya JKT Ruvu na JKT Oljoro kwa bao 1-1 kabla ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar juzi. 

SOURCE:  BIN ZUBEIRY 

SERIKALI YAITOA KATIBA YA TFF YA MWAKA 2012 YAAGIZA UCHAGUZI UTUMIE KATIBA YA 2006

Serikali imeingilia kati sakata la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuamuru kufutwa kwa katiba ya sasa ya shirikisho hilo na badala yake kuamuru itumike katiba ya zamani (mwaka 2006) baada ya kubaini kuwa iliyopo ina kasoro nyingi.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari leo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeeleza kuwa katiba ya sasa ya TFF si halali. Imeelezwa vilevile kuwa msajili wa vyama vya michezo aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa.

Mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF umesimamishwa kutokana na mgogoro mzito uliotokana na kuenguliwa kiutata kwa wagombea kadhaa, wakiwamo Jamal Malinzi anayewania urais na Michael Wambura anayetaka kugombea nafasi ya makamu wa rais.

Kamati ya rufani ya TFF inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ndiyo iliyozua balaa lote la sasa baada ya kuwaengua kina Malinzi na mwishowe kumuacha makamu wa sasa wa rais, Athumani Nyamlani abaki kuwa mgombea pekee.


Hata hivyo, tayari mchakato wa uchaguzi huo uliozua mabishano makali umeshasimamishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na maafisa wa chombo hicho cha juu cha mchezo wa soka duniani wameshaanza kuwasili kufuatilia kinachotokea nchini.

Uamuzi wa serikali wa kufuta katiba ya sasa na kutaka itumike ya 2006 unampa ahueni kubwa Wambura ambaye alishasema hadharani kuwa  ataiburuza TFF mahakamani kama isipoachana na katiba mpya na kufuata ya zamani; huku akitoa sababu kadhaa za kupinga matumizi ya katiba mpya, mojawapo ikiwa ni kupitishwa kwake kwa njia ya waraka wa barua pepe (e-mail) kwenda kwa wajumbe badala ya kufuata maelekezo ya katiba yanayotaka mabadiliko kufanywa na wajumbe kupitia mkutano mkuu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za FIFA, ni marufuku kwa shughuli za soka kuingiliwa na serikali au mahakama na nchi yoyote inayokwenda kinyume na taratibu hizo hujikuta ikifungiwa kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya.


HUYU NDIO MTOTO WA MIAKA NANE ALIE MUOA MWANAMKE WA MIAKA 61

Zaidi ya watu mia moja walikusanyika katika nchi ya Zimbabwe kushuhudia mtoto wa miaka nane (8) akimuoa mwanamke mwenye umri wa miaka (61) ambae anaweza akafaa kabisa kuwa bibi yake. Cha kushangaza zaidi familia zote mbili za wanandoa hao pamoja na watoto watano wa mwanamke huyo walikuwepo.
Shangazi wa mtoto huyo mwenye miaka (46) alitoa sababu za kutokea ndoa hiyo alisema "Huyu kijana alipewa jina la bibi yake ambae hakuwahi kufunga ndoa, mizimu imemuamuru afunge ndoa na Hellen (Mmama huyo) ndio imekuwa chaguo lake.
Wanafamilia walichukulia matamanio ya huyo kijana kufunga ndoa kwa umakini sana na kuamua kumruhusu kufunga ndoa na kulipia kila kitu. Na bibi huyo alieolewa na kijana huyo pamoja na kuwa na mume alikubali kuolewa kwa kuwa alijua ndio mizimu ya mababu waliokufa inavyo waamuru na kutaka.
Mtoto huyo alimuambia mama yake "Nataka kuoa kwa kuwa nataka kufanya hivyo na nimemchagua mwanamke huyu kwa kuwa nampenda na baada ya ndoa hii nitasoma kwa bidii sana na nikiwa mkubwa nitamuoa mwanamke ninalingana nae"
Mume wa mwanamke huyo alisema yeye hana shida wala wivu na kijana huyo kwa kuwa ni mdogo na ni mizimu iliyoyataka hayo. "watoto wangu na mimi hatuna shida na hili na tumefurahi sana"
Baadhi ya wanafamilia walioneshwa kushitushwa na ndoa hiyo na wanafamilia wenzao kuchukulia swala la mizimu kwa umakini wa kiasi hicho.
Wanandoa hao walimaliza harusi yao kwa mabusu moto moto.




TAASISI YA AL JAZIRA ISLAMIC CENTRE KULIBURUZA GAZETI LA MTANZANIA MAHAKAMANI


Shekh Jabir Katula ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa kituo cha Aljazira Islamic akizungumza na waandishi wa habari huku akishuhudiwa na baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.
Uongozi wa Taasisis ya Al Jazira Aslamic Centre umekanusha habari ilizotaja kuwa ni za uongo, uzushi na ufitini zilizochapishwa na gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 13 februari 2013 na toleo la tarehe 20 februari 2013 zikikitaja kituo hicho kufadhiliwa na makundi ya Al-Qaeda na Al-Shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani.

Aidha kituo hicho kimesikitishwa na taarifa hizo na kutia mkazo kulitaka gazeti hilo (Mtanzania) kuomba radhi kabla ya siku saba kutokana na demand note waliyoitoa, kinyume na hapo taasisi hiyo imesema kuwa itachukuwa hatua zaidi za kisheria.
Kusanyiko lililofika kushuhudia tamko.

Shekhe Mohamed Salum Mbala Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza.
"Habari iliyotangazwa imetustusha sana imetudhalilisha, imetuudhi ni taarifa ambayo haikufanyiwa utafiti, imevunja heshima ya waislamu sio wa Mwanza Tanzania pekee bali dunia nzima, tunasema wazi kuwa sisi waislamu tunapenda amani na tuko kwa ajili ya kuitangaza amani na hatuko tayari kuvurugwa kuipoteza amani ya nchi hii"

"Kwa kweli tunalaani sana udhalilishaji huu tunaomba mwandishi wa habari hizo atoe ushahidi na hatutokubali kama hatotoa ushahidi"
Shekhe Musa Kunenge ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre Ukerewe amesema kuwa chuo chake kilipata idhini ya waislamu kwenye msikiti, kisha kikafuata njia zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kupata kiwanja hatimaye usajili na shughuli zote zinatendeka kwa haki na uhalali na wala kituo hicho hakijihusishi na yale yanayotajwa kwenye magazeti kukichafua chuo hicho. 


HIZI NDIO PICHA ZINAZOSEMEKANA ZA TIMBULO BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA BURUNDI




TCRA YAIFUNGIA TV IMAAN

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Televisheni pekee ya Kiislam ambayo inamilikiwa na Taasisi ya The Islamic Foundation ya Mjini Morogoro. Hiyo ndio Televisheni pekee ya Kisslam ambayo imekuwa ikimilikiwa na kuupasha habari umma wa Kiislam nchini Tanzania. 
Sababu za kuifungia Televishni hiyo bado hazijawekwa wazi. Televisheni hiyo imefungiwa tokea jumamosi.
Baadhi ya wananchi walioongea na Blog hii wamekuwa wakihisi labda ni katika mchakato wa kuendelea kuwashughulisha ili wasikae sawa katika malengo yao. Wenfgi wa wakazi wa Morogoro wamekuwa wakiitambua Taasisi ya The Islamic Foundation kama msaada mkubwa kwao na kwa jamii bila kujali hata rangi, kabila wala dini.
Kufungwa kwa Televisheni hii kumekuja huku serikali ya Morogoro ikiwa imekitambua kwa kuitunuku cheti maalumu Taasisi hiyo ya The Islamic Foundation kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa jamii. Wengi wamekuwa wakilaumu mamlaka hiyo ya mawasiliano kwa kitendo hicho tena kuifungia jumamosi wakati ofisi za kiserikali zikiwa zimefungwa.
Chini ni baadhi ya habari zilizowekwa na mmoja wa waandamizi waliokuwa wakishughulika na Televisheni hiyo ikitanabaisha kufungwa kwa Televisheni hiyo na kuwaomba Waislam Tanzania kuwa na Subra na kuongeza moambi katika ukuta wa mtandao wa jamii. Muhusika huyo anajulikana kwa jina la Ahmed Bawazir ambae jina lake limekuwa likisomeka hivyo kwa kiarabu

www.kitongoni.blogspot.com
 




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU