Facebook Comments Box

Sunday, September 28, 2014

UTURUKI WARUHUSU HIJJAB KWA WANAFUNZI

Nchi ya Uturuki imeondoa marufuku ya kuvaa Hijabu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari iliyodumu takribani kwa muda wa muongo mmoja.

Uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumanne na Naibu Waziri Mkuu Bulent Arinc.


Akizungumza na waandishi wa habari Bulent Arinc alisema kwa sasa serikali imeruhusu wanafunzi kuhudhuria shuleni wakiwa wamevaa Hijabu katika shule zote zilizo chini ya Wizara ya
Elimu.

Bulent Arinc ambaye ni msemaji pia wa chama cha Justice and Development (AK) alisema agizo hilo baada ya siku mbili litakuwa lenye kutekelezwa baada ya kupeleka taarifa za kimaandishi katika Wizara husika.


Hijabu ilipigwa marufuku mwaka 1980 kwa wanafunzi, wafanyakazi katika taasisi za umma na serikali muda mfupi baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Tangu wakati huo wanawake waliokuwa wakivaa hijabu nchini humo walilazimika kuacha kazi katika ofisi za serikali.

Utawala wa Uturuki umekuwa ukijaribu kuwa mbali na taratibu za kiislamu kwa ajili ya kuridhisha nchi za Ulaya ili kuingizwa katika
umoja wa nchi hizo. Uturuki kwa muda mrefu imetaka kuwa mwanachama wa nchi hizo
za Ulaya bila mafanikio.

Waziri Mkuu ErdoÄŸan aliahidi kuondoa marufuku yote juu ya uvaaji wa Hijabu wakati aliposhinda kwa mara kwanza mwaka 2002.


Tangu wakati huo aliondoa marufuku ya kuvaa Hijabu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Hata hivyo bado vazi la Hijabu halijaruhusiwa kwa majaji, waendesha mashtaka, maafisa wa kijeshi na wafanyakazi wa kijeshi.

 Cha kuzingatia ni kuwa katika baadhi ya nchi za ulaya ikiwemo uingereza vazi la hijjab linavaliwa na watu wote hata askari kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.




MATOKEO NA PICHA YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA TANZANIA

Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo September 27,2014.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ramadhani Singano 'Messi'
Timu ya soka ya Simba SC imelazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni hii Septemba 27,2014,kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Hiyo ni sare ya pili mfululizo kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya wiki iliyopita kutoka 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Taifa, licha ya kuongoza 2-0 hadi mapumziko. 




Hadi mapumziko, tayari Simba SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. 


Timu ya Polisi inayofundishwa na Mohammed ‘Adoph’ Rishard ilibadilika na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa Simba SC ambapo Danny Mrwanda, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, aliisawazishia Polisi baada ya kumzidi mbio na maarifa beki Joseph Owino kabla ya kumchambua vizuri kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’. 


Azam FC imepata ushindi wake wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Chamazi. 
 

Azam FC ambao walianza ligi kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 3-1, imeshinda mabao hayo mawili leo, yote yakitupiwa kimiani na Mrundi, Didier Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne. 
 


Matokeo mengine ya Ligi Kuu Vodacom 2014/2015 ni kama ifuatavyo:- 

Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting 

Mtibwa Sugar 3 – 1 Ndanda FC 

Mbeya City 1 – 0 Coast Union 

Mgambo Shooting 0 – 1 Stendi United


COUTINHO NA TEGETE FITI KUWAVAA PRISONS LEO

IMG_0152
KIKOSI cha timu ya Young Africans kitashuka dimba la Uwanja wa Taifa siku ya jumapili kupambana na Wajelajela, Timu ya Jeshi la Magereza,Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya ikiwa ni mchezo wa pili wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/2015.
Akiongea na tovuti rasmi ya klabu leo mara baada ya mazoezi, kocha mkuu wa Young Africans Mbrazil Marcio Maximo amesema vijana wake wako fiti kuelekea mchezo huo wa siku ya jumapili huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu.
Maximo amesema baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar, kikosi chake kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola huku wakiyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo wa awali.
Kuhusu timu ya Tanzania Prisons, Mbrazil Maximo amesema anatambua walishinda mchezo wa awali dhidi ya Ruvu Shooting hivyo wana morali bado ya kuendeleza ushindi siku ya jumapili, lakini pia kikosi chake kipo fiti kusaka pointi tatu muhimu.
Aidha Maximo amesema habari njema kwa wana Yanga ni kurejea dimbani kwa kiungo Andrey Coutinho pamoja na mshambuliaji Jerson Tegete ambao wanatarajiwa kuonekana kwenye mchezo huo na kuhakikisha wanaisaidia timu yao kupata ushindi.
Wachezaji watakaoukosa mchezo wa siku ya jumapili ni Oscar Joshua na Hussein Javu ambao wote ni majeruhi, wakisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, na jumatatu wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kuwa kwenye matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr Suphian Juma.
Marcio Maximo amewaomba wapenzi, washabiki, wanachama na wadau wa soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili katika mechi dhidi ya Prisons kuja kuwapa sapoti vijana na kuwashangilia muda wote wa mchezo.


Chanzo:shaffihdauda


RADIO ONE WAIBOMOA ZENJ FM: HUYU NDIO MTANGAZAJI WALIO MCHUKUA


Rama B akiwa na Kocha wa Simba Phiri

Kama  ukifika  Unguja  leo  hii  na ukimuuliza  hata  mtoto  mdogo  Rama  B  ni  nani  basi  jibu  utakalolipata  huyo  ni  mtangazi  mahiri  sana  wa  kipindi  cha michezo na burudani  cha  Zenji  fm, na kama  kuna  taarifa  iliyokuwa  gumzo kwa  wanamichezo  kwa  mwezi  ulipita  basi  ni  kuacha  kazi  kwa  ghafla  kwa  watangazaji  wawili  wa kutegemewa  wa  vituo viwili   ndugu  Itv  na  Radio  one  Maulid  Baraka  Kitenge  Maulid  Kambaya,siku chache  baada  ya  kuacha  kazi  Itv / Radio  One  watangazaji  hao  kila  mmoja  kwa  wakati  tofauti  aliripoitiwa  kujiunga  na  kituo  kipya  cha  redio  jijini  ambacho  kimekuwa  gumzo kwa  sasa cha  E  fm,hali  hiyo ilizua  hofu  kuwa  kipindi  cha  spoti  leo  huenda  kikadorora  na  hata  kupoteza  sifa  yake  tofauti  na awali  walivyokuwepo  Maulid  Kitenge   na  Katanga.
Kufatia  kuondoka  kwa  watangazji  hao  wawili  hali  ilionekana  kuwa  si  shwari  hasa  katika  kipindi  hicho  cha  spoti  leo   kuonekana  kama  hakina  mwenyewe  na  kuonekana  kama  kinakwenda  kwa kuunga  kuunga  hasa  pale  alipokuwa  hajulikani  ni  nani  sasa  mfanyaji  wa  kipindi  hicho  tofauti   na  awali, kuna  wakati  alisikika  Isac  Gamba, Deo Rweiyunga ,Amri  Masare  na mara  nyingine  pia  alisikika  Ally  Kashushu  ambaye  yeye  kwa  kawaida  huwa  anatangaza  michezo  kwenye  kituo  cha  redio  cha  Capital  fm  ambacho  pia  ni  kituo  chao.

USAJILI  WA  KIMYA  KIMYA.
Tofauti  na  kituo  kilicho  wanyakuwa  watangzaji  wao  kufanya  mbwe  mbwe  kwa  kuweka  picha  za  kuwasainisha  mikataba  watangazaji  hao  nyota  Redio  One  wao  wameonyesha  kukomaa   zaidi  kwa  kufanya  vitendo  kimya  kimya  kwani  mara  baada  ya  kufanya  usajili  wao  kimya  kimya  usio  na  mbwe  mbwe  hata  chembe  na tayari  sasa  ni  wiki  ya  tatu  tangu  wafanye  usajili  wao kwa  kumnyakua  mtangazaji  mahiri   kutoka  Kisiwani  Unguja  katika  kituo  kikubwa  sana  visiwani  humo  Ramadhan  Yusuf   Madogo  na  ameanza  kuunguruma   katika  vipindi  kadhaa  vya  Redio  One  kama  vile  Nipashe, Muziki  na  michezo na hata  kwenye  kipindi cha  leo  alisikika  samba samba  na  Amri  Masare,pia ameisha sikika  katika  kipindi  cha  Africa  Panorama na  Spoti  leo na  kuonyesha  kuwa  ana  uwezo  mkubwa   wa  kutangaza  na pia  wa  kuwenda  na  kasi  ya  kipindi  hicho.

RAMADHAN  YUSUF  MADOGO  NI  NANI?
Ramadhan  Yusuf  Madogo  ni  Kinyozi, Mwanamuziki  wa  muziki  wa kizazi  kipya, Mc  wa  shughuli  mbali  aliyegeukia  utangazaji, Ramadhan  Madogo  ni mtoto  wa  9  kati  watoto  14  wa  marehem  mzee  Yusuf  Madogo, alipata  elimu ya msingi  shule  ya  Kawawa  mkoani  Lindi na Elimu  ya  Sekondary  aliimalizia  katika  shule  maarufu  ya  High lands  ya  mkoani  Iringa  mwaka  1998,mwaka  1999  alifanya  kazi  ya kunyoa  kabla  ya  kuipa  kisogo  na kuingia  kwenye  muziki  wa kizazi  kipya kwa  takriban  miaka  8 na mpaka  leo  ana  nyimbo  zake  kadhaa  alizofanya  wakati  huo  ambapo  muziki  aliuanza  wakati  yupo  mkoani  Dodoma  wakati  akiishi  mkoani  humo, mwaka  2002 - 2003  aliachana  na  muziki  na kuingia  katika  chuo cha  Stone town  Computer, mwaka  2007  alijiunga  na  Zanzibar  Cable  Tv  akiwa  mtangazji  na  wakati  huo  alikuwa  akitangaza   vipindi  vya  sanaa  na  wasanii  tu,mwaka  2008  alijiunga  na  chuo  cha  cha  Royal   College  na   kufanikiwa  kupata  Diploma  ya  uandishi  wa  habari, na  baada  ya  mafunzo  hayo  ndiyo  akajiunga  na  Redio  ya  Chu chu  fm  ya  Marehemu  Yusuf  Chu  chu   Bwana  Chu  chu, mwaka  2009   alijiunga  rasmi  na  redio  ya  Zenji  fm  96.9  inayomilikiwa  na  Mh.Mohammed  Seif  Khatib  ana amedumu  nayo  kwa  miaka  takriban  6  mpaka  mwezi  huu  wa  September 2014 ndiyo  amejiunga  na  kituo  cha  Redio   One  huyu  ndiyo  Ramadhan  Madogo  al  maarufu  kama  RAMA   B  mtu   muhimu  sana  kwa  ZENJI  FM   wakati  huo, ambaye   wa Zanzbar  wanaona  ni  zaidi  ya  Kitenge  na  Katanga   kwa  kuwa  yeye  muandaaji  vipindi  mbali  mbali  siyo  michezo  pekee, alikuwa  akifanya  kazi  kwenye  vitengo  vyote  vya  Zenji  fm  kuanzia  Michezo, Vipindi  vya  Burudani, Vipindi  vya  habari  na  matukio na vya  kijamii  na  kisiasa  pia, Je  RAMA   B   ataweza  kuvivaa  viatu  vilivyovuliwa  na  Kitenge  na  Katanga ?


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU