Facebook Comments Box

Tuesday, June 17, 2014

SHAMBULIZI JINGINE MPEKETONI KENYA

Shambulizi lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na
Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri
kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja
usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia
shirika la habari la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi
itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku
wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na
kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.

 CHANZO: BBC


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU