Facebook Comments Box

Friday, July 26, 2013

WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA "TAIFA STARS" WAKIWASILI JIJINI KAMPALA LEO KWA MECHI YA KESHO


John Bocco akiwasili katika Hotel waliyofikia jijini Kampala

Wachezaji wa Timu Ya Taifa (Taifa Stars) wakiwsili katika hoteli ya Mt. Zion ambapo wamefikia huku wakijiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi ya Uganda Cranes kuwania kufuzu mashindano ya CHAN.

Stars leo wamepumzika na kesho watafanya Mazoezi katika Uwanja wa Mandela uliopo Nambole ambapo mechi ya Jumamosi itapigwa.
Erasto Nyoni


Mrisho Ngassa

Nahodha Juma Kaseja

Kevin Yondani

Aggrey Morris


UBALOZI WA MAREKANI WAIPONGEZA TTCL KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO


US1Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw.Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.US11Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango wa         TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani alipotembelea Nchini Tanzania.
US14
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.
 
 Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.US16Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa Marekani kwa huduma bora iliyotoa  wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa nchini.
Akitoa shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka  ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora na za uhakika  kutoka TTCL wakati wote wa ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza kuwa huduma walizozipata  zimethibitishwa na taarifa kutoka ofisi inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi walizopita Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya kiwango cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Katika Shukurani zake Bw. Jeff Shrader alioa pia zawadi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura  na kwa baadhi ya wawakilishi kutoa fani mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL kama ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.


RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIENDELEA NA ZIARA YAKE YA SIKU SITA MKOANI KAGERA, LEO YUPO WILAYANI MULEBA

Raisi Jakaya Kikwete akiendelea na ziara yake Mkoani Kagera, hatimaye leo ameingia katika wilaya ya Muleba hebu fuatilia habari na picha zaidi hapa chini:









CHANZO:MATUKIO MICHUZI

VIDEO: ANGALI UTAPELI HUU MCHANA KWEUPE




TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUSITISHA UCHIMBAJI WA MADINI MERERANI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAUAJI YA MFANYAKAZI WA MGODI WA TANZANIE, KITALU C, MIRERANI WILAYANI SIMANJIRO

Tarehe 20 Julai, 2013 kulitokea mauaji ya mfanyakazi wa mgodiwa Tanzanite ulioko kitalu C, Mirerani wilayani Simanjiro kwakupigwa risasi na mchimbaji kutoka mgodi wa wachimbaji wadogowa kitalu D katika eneo hilo.

Kitendo hicho kimetokana na wachimbaji wadogo wanaopakanana Kitalu C kuvuka mipaka ya vitalu vyao na kuendesha uchimbajindani ya Kitalu C, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 na Kanuni zake.

Kwa sasa Kitalu C kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Tanzanite One kwa asilimia 50 kwa 50. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika. Wizara imesikitishwa sana na mauaji hayo ambayo ni ukiukwaji wataratibu za usalama migodini.

Serikali haitavumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea nakuhatarisha usalama wa wachimbaji katika migodi ya TanzaniteMirerani.

Tunapenda kuwatangazia wamiliki wa migodi yote ya wachimbajiwadogo katika vitalu B na D ambayo uchimbaji wake unafanyikandani ya mipaka ya Kitalu C kuwa wasitishe shughuli zao mara moja
na wahakikishe kuwa uchimbaji unafanyika ndani yamipaka ya vitalu vyao.

Aidha, uchimbaji uzingatie taratibu za usalama migodini ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na utumiaji wa silaha za aina yoyote migodini. Ukaguzi wa migodi kubaini migodi inayoendeshauchimbaji ndani ya mipaka ya kitalu C utafanywa na Timu yawataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. Vitalu vitakavyobainika kuhusika leseni zake zitafutwa na uchimbaji utatakiwa kusitishwakatika migodi hiyo.

IMETOLEWA NA,
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
26 JULAI, 2013



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU