Facebook Comments Box

Friday, February 8, 2013

WEMA AONESHA PICHA YA MTU ANAESEMEKANA KUWA MUMEWE

Wema Sepetu akiwa kimahaba na mwanaume aliyedai ni 'mumewe'. Picha hiyo ambayo aliiweka kwenye mtandao wa BBM inamuonesha msanii huyo akibusiana na mwanaume huyo lakini wakionekana kuanzia kwenye kidevu hadi kwenye kiuno kama unavyoweza kujionea mwenyewe hapo.
 
Baada ya kuitupia picha hiyo, Wema aliandika: ‘Miss you mume wangu, wewe ndio kila kitu katika maisha yangu, watasema sana lakini mambo yetu yanatuendea vizuri.” Maneno hayo yanaashiria kuwa Wema anampenda sana mwanaume huyo na si Nasib Abdul 'Diamond' tena.

HATIMAYE MATUMAINI AREJEA DAR NA KUPOKELEWA NA WASANII WENZAKE

    Matumaini (katikati) akisaidiwa na wasanii wenzake muda mfupi baada ya kutua.

 Matumaini (kulia) akiwa na Bi. Mwenda (wa pili kushoto) na anayefuata (kushoto) ni msanii mwenzake Kiwewe wakisubiri gari la kumpeleka hospitali.


    Askari wakiwaelekeza wasanii kukaa upande mmoja ili apate hewa.

 Matumaini akiwa amebebwa mgongoni na msanii mwenzake, Mariam Athuman ‘Kalunde’ akimpeleka kwenye gari.

Mama mkubwa wa Matumaini, Bi. Elizabeth (kushoto) na Matumaini (katikati) wakiwa ndani ya gari tayari kuelekea hospitali ya Amana.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza na wasanii maeneo ya Amana wakati Matumaini akiwa kwa daktari.

MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.


DKT. GHARIB BILAL KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA MAREKANI




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Mazingira, Seneta,Robert D. Hormats, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc Marekani, Feb 6, 2013.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU