Mfanyabiashara Maarufu wa madini Mererani na Mmiliki wa SG RESORT ya Arusha, Bw. ERASTO MSUYA Amepigwa risasi ndani ya gari lake na kufa Papo hapo akiwa njiani akitokea Mererani kwenda Moshi. Habari zaidi tutaendelea kuwapa kadri muda unavyozidi kwenda.
Wednesday, August 7, 2013
WATAKA MAMBO MATANO YAONDOLEWE KWENYE MUUNGANO
Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Halmashauri ya Wilaya ya
Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametoa mapendekezo ya pamoja
wakitaka mambo matano yaondolewe kwenye Muungano, yabaki kwenye Serikali
washirika.
Waliyopendekeza yaondolewe ni Mambo ya Nje, Uraia
na Uhamiaji, Sarafu na Benki kuu, usajili wa vyama vya siasa pamoja na
ushuru wa bidhaa wakisema kwamba kama yataendelea kuwepo kwenye Muungano
kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatasababisha
Serikali shirikishi kuwa dhaifu.Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa
kazi za makundi yaliyopewa jukumu la kujadili suala la mihimili, wajumbe
hao walisema mambo hayo matano ndiyo yanayoweza kuzipa nguvu Serikali
shirikishi ambazo zitakuwa Tanganyika na Zanzibar.
Walitolea mfano wa mambo ya nje na kusema kuwa
ikiwa Rais wa Serikali ya Tanganyika au Zanzibar ataondolewa jukumu la
kuteua mabalozi na hata kuiwakilisha nchi nje ya nchi atakuwa
ameondolewa meno. “Nchi washirika ziachiwe masuala ya mambo ya
nje,”alisema Kassim Mohamed Kassi, mkazi wa Chimba akiwakilisha vijana.
Kuhusu Sarafu na Benki Kuu, walisema sababu za
kupendekeza iondolewe katika muungano ni kuwa itadhoofisha uchumi wa
nchi washirika.
Aidha kwa upande wa uraia na uhamiaji,
walisisitiza kuwa kila nchi watu wake wana utamaduni usioingiliana na
nchi nyingine washirika, hivyo kila upande uwe huru.
Ushuru wa bidhaa, wajumbe hao walipendekeza ubaki
kwenye nchi washirika na siyo Muungano kama inavyopendekezwa kwa sababu
ikiwa itaachwa hivyo sehemu kubwa ya kodi na ushuru kutoka nchi
washirika zitashindwa kuwanufaisha watu wake.
Kuhusu usajili wa vyama vya kisiasa, wajumbe hao
walisema hiyo ni moja ya kero za muungano iliyojitokeza baada ya kuingia
kwa mfumo wa vyama vingi. Sheria ya chama ili kisajiliwe sharti kipate
wanachama wa mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Walitaka mambo ya
muungano yabaki mawili tu ambayo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pamoja na Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano.
SOURSE:MWANANCHI
SHOMARI KAPOMBE AFUZU MAJARIBIO UFARANSA
Shomari Kapombe. |
Saleh Ally, Strasbourg :
BEKI nyota wa Simba, Shomari Kapombe, ameonyesha kweli ana kipaji baada ya kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Kapombe mwenye umri wa miaka 21, amefuzu kucheza soka katika timu mbili za hapa Ufaransa.
BEKI nyota wa Simba, Shomari Kapombe, ameonyesha kweli ana kipaji baada ya kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Kapombe mwenye umri wa miaka 21, amefuzu kucheza soka katika timu mbili za hapa Ufaransa.
Championi ambalo linaendelea kuranda nchini Ufaransa, limepata taarifa hizo za uhakika mjini hapa, lakini wakala wake, Dennis Kadito, ameendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwetu. “Kweli Kapombe amefanya vizuri sana, amefanya majaribio hapa na timu ya As Cannes ambayo ni kubwa kabisa na nyingine (ambayo hakuitaja) lakini baada ya mawakala wa timu ya Nice kumuona nao wamepiga simu na kutaka kumsajili, amefanya vizuri sana labda kama itatokea ishu nyingine lakini kwenye majaribio amekuwa gumzo.
“Kama unavyoona hali ya hewa hapa Ufaransa kwa sasa ni nzuri na hakuna tofauti na Dar es Salaam, hivyo imekuwa bahati kwake. “Alianza mazoezi Jumanne iliyopita baada ya kutoka Uholanzi na baadaye akahamia nyingine na zote amefuzu. Jamaa walimchezesha beki wa kushoto kwa dakika 15, wakaona uwezo wake, baadaye wakamhamishia namba sita na huko akacheza vizuri zaidi,” alisema Kadito na alipoulizwa kuhusu dau, akasema:
“Hapo kidogo inabidi nizungumze na Simba, unajua tunapata tatizo kutokana na Tanzania kutokuwa na jina katika soka la kimataifa. Hivyo nitazungumza na uongozi wa klabu yake na ninyi mtapata taarifa.” Pamoja na kuwa mgeni katika soka la Ulaya, Kapombe alionyesha uwezo mkubwa na kuwashangaza baadhi ya mawakala wengine ambao walialikwa kwa ajili ya kumwangalia huku wengi wakijaa wakati alipofanya majaribio Cannes kwa kuwa ni timu maarufu sana hapa Ufaransa.
Utulivu wake kwenye mpira, pasi za uhakika na ujuzi wa kukaba, zilionyesha kuwavutia mawakala wengi kutoka sehemu mbalimbali waliokuwa wakimuangalia katika majaribio nchini Uholanzi tangu alipotua zaidi ya wiki mbili zilizopita. Suala la Tanzania kutokuwa maarufu kisoka, huenda ndiyo limekuwa hofu kwao lakini tayari Kapombe amemaliza kazi yake, kilichobaki ni makubaliano tu kati ya klabu itakayomtaka na Simba.
Championi linaendelea kuranda anga hizi huku likifuatilia zaidi kujua kuhusiana na mchezaji huyo kinda Mtanzania ambaye kama atapata nafasi, huenda akawa amewasaidia Watanzania wengine kutoka.
HOTELI INAYOUZA NYAMA ZA WATU YAGUNDULIWA
Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Nigeria
katika hoteli moja iliyopo karibu na soko moja maarufu sana nchini humo
linalofahamika kwa jina la Ose-Okwodu katika mji wa Anambra baada ya kukamatwa
kwa vichwa viwili vya binadamu vikiwa bado vibichi lakini jina la hoteli hiyo
linahifadhiwakutokana na sababu za kiusalama
hotel human heads in onitsha
MOJA YA STAKE ZA NYAMA ZA BINADAMU ZILIZOKUTWA KATIKA HOTELI
HIYO
|
“kila wakati nimekuwa nakuja hapa sokoni na kufanya biashara
zangu katika hoteli hii kwasababu ipo karibu sana na soko.lakini nilikuja
kugundua mambo ambayo sio ya kawaida ikiwemo watu wakiingia na kutoka katika
hoteli hii,chakushangaza zaidi ni kutokana na watu hao kuwa ni wachafu sana
wakati mwingine wakiwa wamechafuka damu,kwahiyo sikushangaa sana kusikia polisi
wamegundua unyama huo jana asubuhi”alisema jamaa mmoja muuza mboga mboga katika
eneo hilo.
Mchungaji mmoja ambaye ni mmoja kati ya watu waliowatonya
askari kuhusu biashara hiyo ya nyama za watu katika hoteli hiyo alisema
"niliwahi kwenda kwenye hoteli hiyo mapema mwaka huu,niliagiza chakula
lakini baada ya kula nilihisi nyama ilikuwa na chumvi kwa kiwango cha
N700,nilishangaa sana.kwahiyo sikujua kama ni nyama ya binadamu au la
nilishangaa kwasababu ilikuwa inauzwa ghali sana”alimalizia mchungaji huyo
SOURSE: DJ SEK BLOG
HAWA NDIO WAMESAJILIWA NA COASTAL UNION NA MTIBWA SUGAR
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro.
Mgosi ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya JKT Ruvu amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akiongea na mtandao huu, kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime amethibitisha kwamba klabu yake imemsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, "Mgosi anakidhi vigezo vya mshambuliaji tunayemhitaji baada ya kuondoka wa Javu aliyejiunga na Yanga. Ameshaini mkataba wa mwaka mmoja na atajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya hivi karibuni
Mgosi ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya JKT Ruvu amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akiongea na mtandao huu, kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime amethibitisha kwamba klabu yake imemsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, "Mgosi anakidhi vigezo vya mshambuliaji tunayemhitaji baada ya kuondoka wa Javu aliyejiunga na Yanga. Ameshaini mkataba wa mwaka mmoja na atajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya hivi karibuni
Klabu
ya Coastal Union imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kiuganda Yayo
Lutimba kutoka timu ya mamlaka ya mapato ya Uganda URA.
Aliyefanikisha
zoezi hilo ni meneja wa Wagosi, Akida Machai ambaye amepanda ndege
mpaka jijini Kampala kunasa saini ya kijana mdogo mwenye miaka 19, Yayo
Lutimba Kato kutoka timu ya mamlaka ya mapato Uganda (URA).
Nassor
Ahmed ‘Binslum’, ambaye ni mkurugenzi wa ufundi amesimamia kwa kiasi
kikubwa kufanikisha usajili wa wachezaji takriban tisa ukijumlisha na
Kato amezungumza na blog hii usiku wa leo baada ya Meneja Machai kuenda
kumtambulisha Kato kwa Binslum na kuweka wazi kuwa tatizo la ukame wa
mabao litaisha kwa wana Mangush.
Itakumbukwa
kocha Mkuu wa Coastal Union, Hemed Morocco wiki chache zilizopita
wakati wa kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA,
aliweka wazi bado kikosi chake kina matatizo ya umaliziaji.
Alibainisha
kikosi hicho kipo vizuri kila idara kuanzia golikipa, mabeki na viungo
ila hakuna mtu mwenye uchu wa mabao hivyo kuahidi kuwatumia wachezaji
haohao kuwafundisha namna ya kuadhiri magolikipa wa timu pinzani.
Ndiyo
maana winga Danny Lyanga alikuwa akichezeshwa namba kumi ili
kumuangalia uwezo wake wa kupachika mabao lakini hakuonekana kucheza
vema kwenye mechi ya URA.
Kwa
usajili wa miaka miwili kuitumikia Coastal Union kinda huyu atakuwa na
nafasi nzuri sana kujitengenezea jina nchini Tanzania hasa baaada ya
kuwa na rekodi nzuri ya kuwafunga Simba na Yanga mabao mawili mawili
katika mechi walizokutana nazo kwa vipindi tofauti.
Zipo
taarifa kuwa Yanga nao walikuwa mbioni kumnyakua kinda huyu lakini
Meneja Akida Machai amewazidi akili kwa kumfuata hukohuko kwao Uganda.
Na hizi ni mbinu za ‘kimafia’ zinazotumiwa na timu kubwa duniani kote
kunasa wachezaji mahiri.
Mungu
akipenda kesho Kato ataungana na wachezaji wenzake katika kambi iliyopo
pembezoni mwa bahari ya hindi Raskazone Hotel, jijini Tanga.
Wagosi
wameanza vizuri mechi zao mbili za majaribio ambapo mechi ya kwanza
walishinda bao 1-0 dhidi ya URA na siku tatu baadaye wakashuka dimbani
dhidi ya Simba SC ambao nao walichapwa 1-0. Zipo taarifa za kucheza
mechi ya kirafiki siku ya Eid pili uwanja wa Mkwakwani lakini
zikishathibitishwa na timu tutakayocheza nayo tutawahabarisha.
Subscribe to:
Posts (Atom)