Facebook Comments Box

Saturday, August 30, 2014

HII NDIO TIMU ANAYOENDA RADAMEL FALCAO

Mchezaji wa Monaco Radamel Falcao ameuthibitishia ulimwengu kuwa atajiunga na Madrid. Mchezaji huyo alituma ujumbe wa furaha katika akaunti yake ya tweeter na baadae kuufuta ujumbe huo ila tayari watu tulikuwa tumesha upiga picha.
 Wadadavuaji wengine wanasema huenda akaunti yake itakuwa imetekwa na maharamia wa mtandao maarufu kwa jina la kiingereza la "hackers "
Chini ni picha ya ujumbe huo.




RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA MAZAO KIBAIGWA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea soko la nafaka la kimataifa la Kibaigwa mkoani Dodoma katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo Agosti 28, 2014 , ambapo alijionea shehena kubwa sana ya mahindi iliyoletwa kutoka mashambani na kusafirishwa kila pembe ya nchi. Mwaka huu, kama ilivyokuwa mwaka jana, mavuno ya mahindi yamekuwa makubwa kiasi hata cha kupatikana kwa mavuno ya ziada yanayolemea maghala yaliyopo, ikiwa ni muendelezo wa mafanikio ya sera ya kilimo kwanza ambayo imekuwa ikileta matokeo mazuri kila mwaka. (picha hii na zote zinazofuata hapo chini ni kutoka Ikulu).














SALUM MWALIMU ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA CHADEMA

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi kuu za CHADEMA kisiwani humo.

Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chjama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar

Salum Mwalim anayewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kundi la Zanzibar akitia saini kitambu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi kuu za chama hicho Zanzibar kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Mbunge wa CHADEMA viti Maalum wa CHADEMA Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za CHADEMA Zanzibar.


MAJAMBAZI YABAKA NA KUPORA MILIONI 20

Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wanadaiwa kumvamia mwalimu mmoja, wampora zaidi ya Sh. milioni 20 na kumbaka
mwalimu mwingine na kutokomea.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nassa Ginery, wilayani Busega mkoani Simiyu.
Polisi mkoa wa Simiyu imethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia juzi.
Akisimulia tukio, mwalimu aliyepatwa na mkasa huo, Samwel Mbochi alisema watu hao waliruka ukuta wa nyumba yake na kumvamia na kuanza kumshambulia mwilini na kudai awape pesa.
Alisema kuwa pesa hizo alikuwa ameziandaa kwa ajili ya kununua bidhaa kesho yake kwa kuwa amekuwa akijishughulisha na biashara
ya duka.

Alisema baada ya kuchukua pesa hizo, watu hao walimvamia mpangaji wake katika chumba kingine ambaye pia ni mwalimu na kumbaka kwa zamu kisha kutokomea kusikojulikana.
Afisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Simiyu, Evance Mwijage jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo. Mwijage alisema atawataja watu waliohusika kwenye tukio hilo
mara baada ya kupata taarifa rasmi kutoka polisi. 

CHANZO: NIPASHE


MAGAZETI YA LEO: JUMAMOSI TAREHE 30/08/2014





VIDEO: INSTAGRAM WAANZISHA HYPERLAPSE NA KAMERA YA KIPEKEE KWA MBWA

CHANZO: BBC SWAHILI

YANGA NA OKWI WAITWA NA TFF KWENYE KIKAO

Chini ni barua ambazo TFF wamewaandikia klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi kuwaita kwenye kikao cha kamati.



VIONGOZI WA SHURA YA MAIMAM WAMTEMBELEA DR SLAA

Viongozi wa Shura ya Maimam leo asubuhi wamemtembelea Dr. Slaa ofisini kwake iliyopo mtaa wa Ufipa Kinondoni. Lengo la ziara hiyo ni
kumweleza Dr. Slaa juu ya udhalilishaji wanaofanyiwa Masheikh 19 wanaotuhumiwa kwa kesi ya Ugaidi wakiwa chini ya vyombo vya
sheria.

Hivi karibuni imeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa Mashekh hao wamekuwa wakidhalilishwa kijinsia na kuharibiwa sehemu za siri. Viongozi hao wamemwomba Dr. Slaa na Chama chake kuwaunga mkono katika kupaza sauti juu ya udhalilishaji huo na kumwomba ushirikiano katika maswala ya kisheria hasa ikizingatiwa kuwa CHADEMA ni wahanga wa matukio hayo ya udhalilishaji kwa vijana waliobambikwa kesi za ugaidi


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU