WARAKA WA STAR TV KUHUSU KUJITOA KWAO NDANI YA STAR TIMES:
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa Star TV kwenye Star Times.
TCRA imeagiza Chaneli ya Star Tv irudishwe mara moja kwenye Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.
Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakiwa kujitetea tarehe 17 Juni 2013.
Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari.
Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA)
Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Star TV kujiondoa Star Times.
Tarehe
23 Mei 2013 Star TV kupitia mwanasheria wake iliwataka Star-Times
kuiondoa kwenye king’amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 31 Mei
kutokana na kurusha na kuuza maudhui na vipindi vyake bila idhini hivyo
kukiuka sheria za haki miliki (Copyright laws).
Katika barua hiyo Star TV iliwakumbusha Star Times kwamba hawakuwa na mkataba wa kurusha kituo hicho kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano EPOCA pia hawana haki ya kutumia maudhui yake bila idhini chini ya sheria ya haki miliki ya Tanzania na Kimataifa.
Tarehe 31 Mei 2013 Star Times/Star Media walijibu na kudai kwamba hawajakiuka sheria yoyote wakasisitiza wataendelea kuirusha Star TV kutekeleza matakwa ya sheria ya EPOCA na kanuni zake.
Tarehe 6 Mei 2013 Star TV iliwaandikia tena Star Times ikisisitiza nia yake ya kuchukua hatua zaidi kutokana na wao kuendelea kukaidi ombi hilo na kuainisha mapungufu kadhaa ya kisheria kwa upande wao yanayoifanya Star TV ijiondoe kwenye king’amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 08 Mei 20013. Star TV Ilieleza Star Media (T) Ltd. ambayo inamilikiwa kwa pamoja na Star Times
na TBC ina leseni ya miundo mbinu ya kurusha matangazo ya Televisheni kupitia mfumo wa DTT (Multiplex Operator License).
Leseni hiyo inawaruhusu kuingia makubaliano (Service Level Agreement- SLA) na vituo mbalimbali kuwarushia matangazo yao lakini Star-Times hawana leseni ya kutoa huduma ya maudhui (Content Service Provider License-CSP). Star Times ni kampuni ya kimataifa iliyoandikishwa (China) inayotoa huduma ya maudhui katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania. Ili kupata maudhui inalazimika kuingia mikataba na vituo vya televisheni kabla ya kuviingiza kwenye king’amuzi chake na baadaye kuuza maudhui hayo subscription/Pay TV) kwa watumiaji katika mataifa hayo.
Star Times inachukua vituo vya TV ikiwemo Star TV bila idhini yao na kuviweka kwenye king’amuzi chake kwa kisingizio kwamba wanaruhusiwa na sheria ya EPOCA na Kanuni zake. Sheria hiyo inasisitiza juu ya kuwepo kwa mkataba wa makubaliano (SLA) kati ya pande mbili husika.
Kwamba maudhui ya TV za Tanzania yanauzwa kwa watumiaji katika nchi nyingine kama vile Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Nigeria na nyinginezo bila idhini ya wamiliki wake. TV zinazomiliki maudhui hapa nchini hazina uwezo wa kuidhibiti Star Times isirushe maudhui yao nje ya Tanzania kwa kuwa baadhi ya maudhui wanayoyanunua nje kama vile tamthilia na vipindi vingineyo haviruhusiwi na watunzi au wasambazaji wake yarushwe nje ya Tanzania (Territorial Rights).
Lakini pia uhusiano wa makampuni haya mawili Star Media (T) Ltd na kampuni ya Star Times ambayo ni ya China yenye matawi katika nchi mbalimbali za Afrika katika uendeshaji wa matangazo ya Dijitali haujabainishwa vizuri ili kujua nani ni nani na nini anachofanya hapa Tanzania katika misingi ya maelewano ya kibiashara.
Ni kutokana na mantiki ya hoja hizo Star Times waliondoa mara moja Star TV kwenye king’amuzi chao tarehe 08 June 2013 kama walivyoelekezwa na Star TV. Star TV haioni sababu ya kulazimishwa na TCRA kurushwa na Star Times pasipo kuondoa hitilafu hizo za kisheria na bila kuangalia sheria nyingine zinazolinda haki za TV huru kama sheria ya haki miliki na sheria ya ushindani katika soko moja. TCRA kwa kutozingatia hili, inabeba umiliki wa sheria hata zisizokuwa chini ya mamlaka yao (supra organ).
Taarifa iliyotolewa magazetini na Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy kwamba chaneli tano za kitaifa lazima zirushwe na ving’amuzi vyote bure ni za kupotosha kwa kuwa hata hiyo Star Times haizirushi bure imekuwa ikibadilika badilika mara kwa mara pasipo TCRA kuwachukulia hatua za kisheria licha ya wananchi kulalamika kwamba wanatozwa pesa ili kuona.
Hata hivyo Vituo vikubwa vya TV vikiwemo Star TV, ITV, Channel 10 na TBC na vinginevyo visivyo vya kitaifa vinarushwa na akampuni ya BTL na TING bila malipo yoyote ya mwezi na kwa ubora zaidi kuliko Star Times lakini inashangaza kuona TCRA nawakingia kifua Star Times wanaowalipisha watanzania badala ya kutetea vituo vya ndani visivyotoza chochote.
Star TV inarusha matangazo yake bure kwa wananchi na matangazo hayo yanaweza kuonekana kupitia king'amuzi chochote ambacho kina ubora na kuweza kung'amua matangazo ya bure (Free To Air - FTA). Hata hivyo kwa uchunguzi ilioufanya Star TV
imegundua kwamba ving'amuzi vya Star-Times vimefungwa kupokea matangazo ya FTA kutoka kwa warushaji wengine (network locked). Jambo ambalo linakinzana na sheria za EPOCA na hivyo matangazo ya chaneli ambazo ni FTA hayaonekani kwenye Star Times mpaka wayarushe kutoka minara yao na hivyo kupoteza dhana nzima ya FTA, (kwa maana kwamba wana [re-broadcast] chaneli za FTA badala ya kuonekana moja kwa moja kutoka kwa wamiliki).
Star TV inaamini kwamba kazi ya usimamimizi wa matangazo ya TV inayofanywa na TCRA haipaswi kupendelea upande wowote na haipaswi kuingilia masuala ya kibiashara kuilinda Star Times kwa kuwa sio jukumu lao. Kwa mfano, Star TV na TV nyinginezo nchini zilizimiwa matangazo yao ya analojia na TCRA pahala mbalimbali na hivyo kuwalazimu wananchi kununua ving'amuzi vya Star Times bila dhana nzima ya ushindani na uwezeshwaji wa washindani wa ndani kutiliwa maanani na hivyo kuwanyima Watanzania haki yao ya kupata habari.
Sasa miundo mbinu ya humu nchini imejengwa na kampuni za kizalendo kwa gharama kubwa na kwa ubora zaidi kuliko Star-Times. Sasa inaelekea ushindani umewaelemea Star-Times, hivyo TCRA inajaribu kuwasaidia tena. Hili halikubaliki na tupo tayari uwaonyesha watanzania matumizi mabaya ya chombo hiki kwa maslahi ya wageni na watu wachache wasio waaminifu kwa nchi yao.
Pamoja na kazi ngumu ya kujenga miundo mbinu ya DTT ambayo imewakamua wawekezaji wa Kitanzania, Mkurugenzi wa TCRA hajawahi kuwatembelea kuwatia moyo. Star TV inapinga kwa nguvu zote TCRA kufanya usimamizi kwa mtizamo wa kibiashara kwa kujaribu kuwasaidia Star-Times ambao, nia yao ni kupata bure matangazo yanayotayarishwa kwa gharama kubwa na vituo vya Tanzania na kuhodhi urushaji wa maudhui ya TV za humu nchini kupitia DTT kwa faida yao. Kimsingi Star-Times ni TV ya kigeni na kwa mujibu wa sheria mpya ya EPOCA haistahili kupewa leseni ya ndani ya maudhui kushindana kama local TV.
Hata hivyo, kama inadaiwa kwamba Star Media (T) Ltd na Star Times ni kitu kimoja basi kampuni zote mbili zinafanya kazi kinyume cha sheria ya EPOCA na kanuni zake ambayo kwa mujibu wa kifungu cha 12(h) kinaonyesha jinsi mwenye leseni ya miundo mbinu (Multiplex) anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake. Kinasema:“Multiplex Operator hataruhusiwa kurusha maudhui yake mwenyewe, vituo vyake vya TV au kifurushi chenye maudhui yake (Bouquet)”.
Kwa hiyo Star TV haiko tayari kujihusisha na Star-Times au kufanya biashara na chombo chochote ambacho mwenendo wake wa kibiashara haufuati matakwa ya sheria. Pia, Star-TV haikubali kusukumwa kwenye makubaliano ya kibiashara kwa matumizi ya nguvu na tafsiri potofu ya sheria zetu. Hii ni kugombanisha watanzania kwa kutumia sheria zao wenyewe zinazotafsiriwa vibaya kukidhi tamaa ya watu wachache.
Intellectual Property Rights ni mali ya mwenye nacho, sio mali ya serikali na hivyo hakuna mtu wa kuamrisha mtu atoe kipindi, wimbo, sanaa, shairi, au mchezo wake kwa mtu mwingine. Sheria ya Hatimilki imetungwa ikizingatia maelekezo ya shirika la biashara la kimataifa (WTO), na Shirika la utambuzi wa hakimilki la kimataifa (WIPO), ambayo Tanzania ni mwanachama. Kulazimisha mtu kutoa haki yake ni uvunjaji wa sheria na haki za kibinadamu. Hakuna yeyote hata kama ni nani anayo haki hiyo isipokuwa mwenye nacho. Tupo tayari kutafuta haki hii mahakamani kama TCRA wanataka tufanye hivyo!

Imetolewa na Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group Ltd.
Nathan Lwehabura
kwa niaba ya uongozi.