Facebook Comments Box

Thursday, August 29, 2013

MAKUNDI YA UEFA HAYA HAPA

 
Groups

Group A
Man. United(ENG)
Shakhtar Donetsk(UKR)
Leverkusen(GER)
Real Sociedad(ESP)

Group B
Real Madrid(ESP)
Juventus(ITA)
Galatasaray(TUR)
København(DEN)

Group C
Benfica(POR)
PSG(FRA)
Olympiacos(GRE)
Anderlecht(BEL)

Group D
Bayern(GER)
CSKA Moskva(RUS)
Man. City(ENG)
Plzeň(CZE)

Group E
Chelsea(ENG)
Schalke(GER)
Basel(SUI)
Steaua(ROU)

Group F
Arsenal(ENG)
Marseille(FRA)
Dortmund(GER)
Napoli(ITA)

Group G
Porto(POR)
Atlético(ESP)
Zenit(RUS)
Austria Wien(AUT)

Group H
Barcelona(ESP)
MmMilan(ITA)
Ajax(NED)
Celtic(SCO)


PICHA: SAMUEL ETO`O ASAINI CHELSEA

Samuel Eto`o akionesha jezi yake baada ya kusajiliwa kwa mwaka mmoja akitokea kilabu cha Anzhi Makhachkala.

Samuel Eto`o (32) akionesha jezi ya Chelsea baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na kilabu hicho cha London



BREAKING NEWS: MAJAMBAZI WAVAMIA BANK YA HABIB AFRICAN KARIAKOO

Majambazi wamevamia benki ya Habib African iliyopo K'Koo na kupora kiasi kikubwa cha fedha. Baadhi yao walivalia sare za polisi.

Kwa habari zaidi tutakuletea baadae

Chanzo: East Africa TV



YULE TRAFIKI FEKI KUMBE ALITOROKA GEREZANI

MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.
Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha. Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.
“Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.
“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.
Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.
Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.
Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.
Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, Makongoro Oging’ alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.
Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema: “Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”
Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa. James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.


TUNAOMBA UTUPIGIE KURA YAKO ILI TUWE WASHINDI KWENYE MASHINDANO YA BLOG TANZANIA



Wasomaji na wafuatiliaji wa blog ya kitongoni.blogspot.com tunapenda kuwafahamisha kuwa Blogu yetu itashiriki katika shindano la blog Katika vipengele Vifuatavyo

1.Best Entertainments
2.Best News Blog
3.Best Educational Blog
4.Best General Blog
5.Best Newcomer Blog
6.Best Religion Blog
7.Best Sports Blog

 Jinsi ya kufanya
 
Nenda sehemu ya kuandika ujumbe (email), yaani sehemu ya Email yako unapo compose kisha Andika 
Subject:- http://kitongoni.blogspot.com/
Sehemu ya kuandika ujumbe/Post:-  Andika hivi vipengele

1.Best Entertainments
2.Best News Blog
3.Best Educational Blog
4.Best General Blog
5.Best Newcomer Blog
6.Best Religion Blog
7.Best Sports Blog

Kwa maelezo zaidi na vipengele vingine ingia/bofya tanzanianblogawards
 
UNAWEZA KUFANYA YAFUATAYO 

Unaweza kupendekeza blog katika vipengele vingi upedavyo lakini katika kila email unayotuma ni blog moja tu utaruhusiwa kuipendekeza kwa wakati mmoja
Kwa mfano:  Kwenye subject unaandika jina la blog unayotaka kuipendekeza  yaani www.kitongoni.blogspot.com

 
Email iwe ni ya ukweli kama tukiwa tunataka kuwasiliana na wewe kuhusu link ya blog uliyopendekeza tuweze kufanya hivyo na tuma mapendekezo yako kwa hii hapa


nomination@bloggersassociationoftanzania.com
    au tanzanianblogawards@gmail.com
 
Mwanzo wa kupokea mapendekezo hayo ni Tarehe 17/8/ 2013 saa 12:01am mpaka tarehe 02/9/2013 saa 11:59pm saa za Afrika mashariki
 
UKIWA KAMA MPENZI NA MFUATILIAJI WA BLOG YETU HII TUNAOMBA UTUME MARA NYINGI UWEZAVYO ILI TUWEZE KUINGIA KWENYE MASHINDANO HAYA NA KUIBUKA WASHINDI,TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU.

ASKOFU DR SHAO ASEMA WACHAGGA KUZIKANA KWAO NI UTARATIBU WA HOVYO

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk Martin Shao, amekosoa utamaduni wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro, ambao wengi ni Wachaga, wa kuzikana nyumbani (vihamba) na kusema ni utaratibu wa hovyo.

Akifafanua kauli hiyo juzi, Askofu huyo alielezea hofu ya kupotea kwa mashamba ya mibuni mkoani humo, kutokana na utamaduni uliosababisha ongezeko la makaburi kwenye mashamba hayo.

“Naomba Serikali mkoani, iweke utaratibu wa kudumu wa maeneo ya maziko badala ya watu kuzikwa ovyo majumbani… ardhi hii ni ndogo, lakini bado tunaimega kwa kuzika, hapo baadaye hatutakuwa na 
mashamba ya mibuni,” alisema.

Askofu huyo aliiomba Serikali kuelimisha wakazi hao, ili wabadili mfumo wa kugeuza makazi na mashamba yao  sehemu ya kuzika ndugu zao, ili kutotumia vibaya ardhi ndogo iliyopo.

Alisema hayo wakati wa harambee ya kuchangia Sh milioni 95 za ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Nanjara  wilayani Rombo na kusisitiza umuhimu wa Serikali kuweka utaratibu wa maeneo ya kudumu ya maziko.

Kwa mujibu wa Askofu Shao, licha ya hatari ya kupunguza mashamba ya kahawa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi wa mkoa, lakini pia utaratibu wa sasa wa kuzikana majumbani, utaathiri vizazi vijavyo na kusababisha vikose maeneo ya ujenzi wa makazi.

Alisema kutokana na mkoa kubuni miradi mikubwa ukiwamo wa soko la biashara la kimataifa la Lokolova na mji wa kitalii wilayani Siha, ni matumaini ya Kanisa kuwa pia Serikali itaandaa utaratibu wa kila wilaya, kutenga maeneo ya maziko ya jumuiya.

Dk Shao alisema iwapo mpango wa kila wilaya kutenga maeneo hayo utashindikana, Kanisa litakuwa tayari kununua ardhi kwa ajili ya waumini wake.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, alisema amelisikia na atalifikisha kwa Kamati ya Ushauri ya Mkoa ili ufumbuzi upatikane.

Mwanri pia alishukuru Kanisa kwa kutambua mchango wa Serikali kuleta maendeleo ya wananchi. Katika harambee hiyo, Sh milioni 35.5 zilipatikana. --- Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la HabariLeo


TAARIFA KUTOKA TCRA KUHUSU URUDISHWAJI WA MATANGAZO YA RADIO IMAAN NA KWA NEEMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO


1.0 Utangulizi:

Mnamo tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za Utangazaji.

Kamati ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-

a)   Vituo vyote vilipewa  onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia
tarehe 26/02/2013;

b)  Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za utangazaji.

2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo na Mamlaka ya Mawasiliano:   

Baada ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani “Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla ya kuvifungulia.

3.0 Kurejeshwa kwa Matangazo

Kamati ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.

Kamati ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji. Kamati ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia leseni zao.

Kamati ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na kudumisha amani nchini.

Eng. Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013

----

KUHUSU KAMATI YA MAUDHUI:

1.1. Kamati ya Maudhui ni kamati iliyoundwa kwa mujibu wa sehemu ya IV kifungu cha 26 (1) cha Sheria Namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, na marekebisho yake katika kifungu 173 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) Mwaka 2010

Kwa mujibu wa sheria, majukumu na kazi za Kamati ya Maudhui ni pamoja na:-

(a) Kumshauri Waziri wa Sekta kuhusiana na Sera ya Utangazaji nchini;
(b) Kushughulikia malalamiko kutoka kwa watangazaji na watumiaji wa huduma za utangazaji nchini;
(c) Kusimamia na kuhakikisha kuwa kanuni za utangazaji zinafuatwa.
(d) Kusimamia na kufuatilia maudhui ya vituo vya utangazaji.

1.2. Kamati hii ilianza kazi zake Oktoba 2012 baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (MB) tarehe 4 Desemba, 2012. 

1.3. Kamati ya Maudhui inaundwa na wajumbe watano. Wanne ni wateuliwa wa Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Utangazaji na Mwenyekiti ambaye huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya TCRA. Muundo huo umetolewa na sehemu ya 26 (2) ya Sheria ya TCRA ya Mwaka 2003. 

Majina ya wajumbe ni kama ifuatavyo:- 

i. Mhandisi Margareth Munyagi -Mwenyekiti
ii. Bwana Walter Bgoya -Makamu Mwenyekiti
iii. Bwana Abdul Ngarawa -Mjumbe
iv. Bwana Joseph Mapunda -Mjumbe
v. Bwana Yusuf Nzowa -Mjumbe


ETO`O AWASILI LONDON KUFANYIWA VIPIMO KWA AJILI YA KUJIUNGA CHELSEA

eto c6562
Eto'o akiwasili London
eto2 85114
Chelsea inakaribia kumsajili mshambuliaji Samuel Eto'o kwa dili la mwaka mmoja lenye thamani ya £7million kwa mkataba wa mwaka mmoja leo Alhamisi baada ya kukiri kushindwa kumpata mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.

Eto'o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru.
Pamoja na hilo, lakini inaeleweka kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili kuweza kumuondoa katika listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya klabu ya Anzhi.

Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU