Friday, August 16, 2013
TRA ILALA YAKAMATA BIDHAA AMBAZO WAFANYABIASHARA WADAIWA KUKWEPA KODI KUPITIA MASHINE ZA EFD
Meneja
Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mkoa wa Ilala, Catherine Nkelebe
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana ,
kuhusu TRA mkoa huo kukamata bidhaa mbalimbali za dukani ambazo
wafanyabiashara wanadaiwa kukwepa kuzilipia kodi kupitia mashine za
kielektroniki.
Marobota ya bidhaa mbalimbali yakiwa TRA Mkoa wa Ilala baada ya kukamatwa.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA),
Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, imekamata bidhaa mbalimbali za
dukani zenye thamani ya mamilioni ya fedha ambazo wafanyabiashara
wamefanya hujuma ya kukwepa kulipa kodi kupitia mashine za
kielektroniki (EFD-Electronic Data Enterchange).
Meneja Msaidi wa TRA Ilala,
Catherin Nkelebe akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, alisema bidhaa hizo ambazo ni pamoja na sufuria, Khanga na
mitumba zilikamatwa kufuatia msako unaoendeshwa na mamlaka hiyo kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Nkelebe alisema wafanyabishara
wamekuwa wakitumia mbinu nyingi kuwepa kulipa kodi kwa kukataa kutumia
mashine maalum za kielektroniki zilizotolewa na TRA kwa kukata
stakabadhi kwa wateja wanaokwenda kununua bidhaa katika maduka yao.
Alisema ujanja unaofanywa na
wafanyabiashara ni kwamba mteja akienda kununua bidhaa hususan katika
maduka ya jumla wanampatia stakabadhi yenye thamani ndogo wakati mzigo
huo unakuwa na thamani kubwa.
“Unakuta mfano mteja amenunua
bidhaa za thamani ya shilingi milioni moja lakini mwenye duka anampatia
stakabadhi mnunuaji yenye thamani ya Sh. 200,000 ili kukwepa kulipa
kodi,”alisema.
Nkelebe alisema hujuma nyingine
inayofanywa na wafanyabiashara ni kutoa stakabadhi ambazo hazina maelezo
yeyote au mchanganuo wa bidhaa zilizonunuliwa kwa lengo la kuiibia
serikali mapato yake.
Aliongeza kuwa wafanyabishara
wanafanya ujanja huo kwa hofu ya kwamba iwapo wataandika stakabadhi
yenye malipo halali watakadiliwa kiwango kikubwa cha kodi wakati siyo
kweli kwani TRA haifanya hivyo kwani inamkadiria mtu kodi kulingana na
biashara yake.
Alisema TRA kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi wataendelea kufanya msako wa wafanyabiashara wanaofanya
hujuma hizo na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
NGASSA AHALALISHWA KUCHEZEA YANGA
Kwa mujibu wa Page ya mwandishi maarufu wa habari za michezo ndugu Edo Kumwembe amesema kuwa Mrisho Khalfan Ngassa amehalalishwa kuchezea Yanga na atarudisha hela asilimia hamsini ya gharama za Simba na amefungiwa mechi sita.
Hapo chini ni jinsi Bwana Edo Kumwembe alivyo andika:
CHINI NI HABARI HIYO KUTOKA VYANZO VINGINE:
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.
Hata
hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini
kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho
alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea
(sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya
fedha hizo kwa Simba.
Kamati
pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya
Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha
kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa
fedha hizo.
Vilevile
Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa
wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe
zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).
Kwa
upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza
hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali
vya kufanya kazi nchini (work permits).
Kamati
hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za
pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na
kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.
WABUNGE 11 WANASURIKA KIFO BAADA YA BASI WALILO PANDA KUTAKA KUUNGUA
Wakati
msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani
Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa
Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 570 BYU
lilowabeba Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu na kutaka kuungua.
Ajali
hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa
Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa
lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye
mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari
hilo.
Mara baada ya dereva kugundua kuwa
gari analoendesha linataka kuungua alilisimamisha na kuwaambia abiria
wake kuwa gari linaungua.
Kwa
mujibu wa wabunge waliokuwemo kwenye gari hilo, baada ya kuambiwa kuwa
gari linaungua kila mmoja alifanya juhudi za kujiokoa, wengine wakipitia
madirishani.
Kwa Bahati hakuna Mbunge aliyeumia isipokuwa Mhe. Batenga aliumia mkono kidogo baada ya kubanana sana mlangoni.
Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa halikushika moto na baadae lilizimika na kuacha kutoa moshi.
Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa halikushika moto na baadae lilizimika na kuacha kutoa moshi.
Wabunge
waliokuwemo katika gari hilo ni Rebbecca Mngondo (Arusha Viti Maalumu),
Rita Kabati (Iringa Viti Maalumu), Mariam Msabaha (Zanzibar Viti
Maalumu), Mhe. Batenga (Kagera Viti Maalumu), Mhe. Madabida (Dar es
Salaam Viti Maalum), Clara Mwatuka (Mtwara Viti Maalumu).
Wengine ni Mzee Hussein (Zanzibar),
Mussa Haji Kombo (Pemba Zanzibar), Abdul Mteketa (Jimbo la Kilombelo),
Mutula Mutula (Jimbo la Tunduru Kusini).
Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.
Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.
SHEIKH PONDA APELEKWA GEREZANI SEGEREA
Leo
hii, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) aliyekuwa amelazwa katika wodi ya
Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu
(MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu, amehamishiwa katika gereza la
Segerea.Sheikh Ponda bado anauguza majeraha yake ya mkono aliyoyapata huko Morogoro ila jeshi limemchukua na kumpeleka Segerea akamalizie kuuguza majereha huko huko Segerea.
Kwa mujibu wa mashtaka aliyosomewa akiwa MOI, Sheikh Ponda atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapotajwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Kwa mujibu wa mashtaka aliyosomewa akiwa MOI, Sheikh Ponda atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapotajwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
VIDEO: KIJANA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE WA DAR ES SALAAM
Siku moja baada ya ziara ya kushtukiza ya waziri wa uchukuzi Dk. Harison
Mwakyembe, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar-es-Salaam, kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimekamatwa uwanjani
hapo katika harakati za kusafirishwa kwenda nchi za nje.
Chuma Kikikatwa ili kutoa Heroin iliyofichwa ndani yake.
Heroin ikionekana baada ya Chuma kukatwa kama unavyoona hapo pichani.
Subscribe to:
Posts (Atom)