Facebook Comments Box

Monday, August 25, 2014

MAMBO MATANO NILIYO YAONA KATIKA MECHI YA ARSENAL NA EVERTON


Arsenal tumecheza mechi mbili katika ligi kuu ya Uingereza na tumecheza mechi ya awali katika ligi ya mabingwa na timu ya  Besiktas,lakini bado kumeonekana kuna tatizo kidogo katika timu. Kuna matumaini kidogo ya timu kuimarika yalionekana juzi wakati wa mechi na Everton. 

Hapa watu ndio wanapokuwa hawanielewi vizuri wanashangaa haya matumaini yanatoka wapi. Wengi wakidhani naongea kishabiki zaidi kuliko kitaaam. Hebu tukumbuke ile hamasa ya kishambuliaji ambayo wachezaji wetu walikuwa nayo msimu uliopita, kumbuka mchezo mzuri tulio onesha wakati wa mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Manchester City pale Wembley.

Kwahiyo ninavyomjua Wenger sasa atakuwa ameusoma mchezo tulio ucheza pale Goodison Park na kwasasa atakuja na njia sahihi na nzuri katika mechi kubwa na ngumu na zingine zifuatazo.

Kuna mambo matano ambayo tumejifunza katika mechi ile:

Hata kama anatupa hasira na machungu kutokana na magoli ya wazi ambayo kuna wakati anayakosa bado hatakiwi kukosa katika kikosi kwa kuwa kwasasa yeye ndio mshambuliaji wetu tumaini kwasasa na huyu si mwingine bali ni  Olivier Giroud. Ukiangalia kipindi cha kwanza katika mechi yetu na Everton utaona ni kiasi gani tulikosa kushambulia na hivyo kuwaacha watushambulie muda wote.

Pili, Aaron Ramsey bado kidogo hajarudi katika hali yake ya kawaida. Bado mashuti na pasi zake si nzuri kihivyo. Bado tunamkosa katika mechi ya jumatano kutokana na kadi nyekundu na kuna uwezekano akakosekana kwenye mechi na Leicester mwisho wa wiki maana huwezi jua kwani nani alijua kuwa atapewa kadi nyekundu. Lakini pamoja na yote bado ni mchezaji wetu ambae anaweza akaingia kwa nguvu kwenye kumi na nane na kufunga goli kwa juhudi binafsi. Na kama utakumbuka kurudisha kwetu magoli kulianza na yeye na goli lake ndio lilioipa uhai timu yetu. Nina imani atarudi na kuwa bora na tumaini letu katika msimu huu.

Calum Chambers ni beki mzuri ila anahitaj kujua anapocheza na Per Mertesacker anatakiwa acheze vipi. Nina matumaini huu utakuwa wakati muafaka kwa Arsene Wenger kujaribu kumuweka Chambers acheze na Koscielny ili kuweka ulinzi imara na sio Per Mertesacker.
Chambers na imani ni beki mzuri na anaweza akaitendea haki nafasi ya beki vizuri kama akiwekwa na mtu sahihi ambae uchezaji wake unaenda. Ana makosa madogo madogo ambayo sio ya hatari sana kwa timu.

Alexis Sanchez ni mchezaji mzuri ila anahitaji muda ili aweze kuendana na mchezo na ligi ya uingereza. Najua amekuwa akijaribu sana kufanya hivyo na kuonesha kuwa hakusajiliwa kimakosa na ile gharama timu iliyoingia ni sahihi kwake. Ni vizuri ila anatakiwa asiwe na pupa sana atulie na aisome ligi hii, maana ni ligi ngumu na ndefu ambayo katikati ina mashindano mengi ambayo huchosha sana wachezaji. Mfano ni dhahiri katika wiki moja Arsenal tumecheza klabu bingwa ulaya na mechi ya ligi. Sitaki hii iwe kisingizio cha kutoa suluhu mbona Manchester United hawapo katika mashindano makubwa wamefungwa na kutoa suluhu?

Kwa hii mechi na Everton naweza kusema kwa mwisho pamoja na kuwa Arsenal bado hatujaonesha makali yetu ila bado tumeonesha muelekeo mzuri na tumeonesha Dira ya nini tunataka na kuhitaji. Sitakuwa mmoja wa watu wanao shangaa kama tutanyanyua kikombe kikubwa mwezi wa tano ujao.


MCHEZAJI APIGWA NA KITU KIZITO NA KUFA AWANJANI

Mchezaji mmoja wa soka raia wa Cameroon amefariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake kilichorushwa kutoka kwa mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Albert Ebosse aliyekuwa akiichezea kilabu kubwa ya JS Kabylie alikuwa ameifungia timu yake bao la pekee katika mechi ambayo timu hiyo ilishindwa kwa mabao mawili kwa moja na kilabu ya USM Alger.
Kitu kilichomgonga kichwani kilirushwa baada ya mechi kukamilika,wakati ambapo wachezaji walikuwa wanarudi katika chumba cha kujianda.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa
uchunguzi kuhusu mauaji hayo

 CHANZO: BBC SWAHILI


MAGAZETI YA LEO: JUMATATU TAREHE 25/08/2014




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU