Facebook Comments Box

Wednesday, October 8, 2014

BABA ATELEKEZA WATOTO WACHANGA HOSPITALI BAADA YA MAMA KUFARIKI

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Aison Majiyatamu mkazi wa Nankukwe Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya anatafutwa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha Ustawi wa Jamii kwa kutelekeza watoto wake Hospitalini.

Akizungumzia kisa hicho, Afisa Ustawi wa Jamii, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Annah Geretha, alisema wanalazimika kumtafuta mzazi huyo kutokana na kutoonekana Hospitali hapo kufuatilia maendeleo ya watoto wake kwa muda mrefu tangu walipozaliwa.

Alisema Mama mzazi wa watoto hao ambao ni mapacha wa kike aliyejulikanakwa jina la Edah Simia alifariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua watoto hao salama kabisa ambapo mume aliuchukuwa mwili wa marehemu kwa lengo la kwenda kuzika kijijini kwao "Namkukwe" lakini tangu kipindi hicho hakurudi tena.

Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu ambapo tangu kipindi hicho watoto wamekuwa wakihudumia na kuhifadhiwa kwenye chumba cha joto katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.

Alisema lengo la kuwatafuta ndugu wa watoto hao ni kutokana na muda wa kuendelea kukaa kwenye chumba cha joto umepitiliza kutokana na umri wao hivyo wanashindwa kuwatoa kwa sababu hawana mtu wa kuweza kuwahudumia nje ya chumba hicho kutokana na uhaba wa wauguzi unaoikabili hospitali hiyo.

Alisema yoyote atakayekuwa na taarifa za ndugu wa marehemu ama baba wa watoto hao atoe taarifa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya au Hospitali ya Wazazi ya Mbeya.



JK KUPEWA KATIBA MPYA LEO



Stori:  Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea ‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete
Bunge hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya katiba mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba inayopendekezwa iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.

Katiba hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi mbalimbali yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga. 
GPL.


MAGAZETI YA LEO: JUMATANO TAREHE 08/10/2014


1_581dd.jpg
2_5a0bd.jpg
3_10758.jpg
4_ef040.jpg
5_57bf7.jpg
6_d92aa.jpg
7_c0f48.jpg
10_189b2.jpg
11_82c0d.jpg
15_c58a5.jpg
16_8a44c.jpg
20_8d405.jpg
21_c74d5.jpg
22_b0c74.jpg
23_6a04b.jpg
24_6ebbc.jpg
25_f5ac9.jpg
26_eaaee.jpg
27_0310b.jpg
28_4ea31.jpg
29_cfcdd.jpg
30_7980d.jpg
32_89968.jpg
33_31f3a.jpg
34_b88ff.jpg
35_63e03.jpg
37_71f17.jpg


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU