Facebook Comments Box

Friday, October 25, 2013

SUMATRA YAWATAKA WAMILIKINA MADEREVA WA PIKIPIKI NABAJAJI KUZINGATIA SHERIA NAKANUNI ZA USAFIRISHAJI.


Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. David Mziray akitoa wito kwa wamiliki wa Pikipiki na madereva wa usafiri huo kushirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza sheria na kanuni zilizowekwa na Mamlaka hiyo, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Udhibiti wa Usafiri Barabarani kutoka Mamlaka ya
Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Gilliard Ngewe akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Kanuni za Kudhibiti Usafiri wa Pikipiki na Bajaj, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi.Fatma Salum.


Picha na Hassan Silayo-MAELEZO Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imewataka wamiliki na madereva wa pikipiki na Bajaji kufuaata na kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa barabara Gilliard Ngewe wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.


Ngewe amewataka wamiliki na waendesha vyombo hivi kuzingatia
wajibu wao kwa kujiwekea mfumo wa udhibiti wa ndani wa kuhakikisha wanaheshimu sheria, na kudhibiti vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria na kulinda usalama wao na abiria
wao. Aliongeza kuwa ni vyema wamiliki wakatambua masharti ya Leseni zao ambayo aliyataja kuwa ni kwanza pikipiki husika kutoa huduma katika eneo lililoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na lazima pikipiki husika zikidhi viwango vya shirika la
viwango.


Alifafanua zaidi kuwa dereva wa pikipiki haruhuswii kubeba abiria
zaidi ya mmoja ambapo kwa pikipiki za miguu mitatu zinatakiwa kubeba abiria kama inavyotakiwa kwa mujibu wa leseni zao zinazowapa kibali cha kubeba abiria wasiozidi watatu. Pia Dereva wa pikipiki anatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga na kuwa na alama ya eneo analofanyia biashara ya kubeba abiria. Ngewe alisema
Ngewe aliongeza kuwa abiria wanatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga
wakati wote wanapotumia usafiri  wa huo ili kuepusha madhara
yanayoweza kuwapata mara ajali inapotokea.


Naye Meneja mawasiliano wa Mamlaka hiyo David Mziray alisema wanashirikiana na mamlaka nyingine kama halmashauri za miji na polisi katika kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za usafirishaji zilizowekwa zinazingatiwa.


Sumatra  imewataka wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivi
kujiwekea mfumo wa udhibiti wa ndani na kuhakikisha wanadhibiti
vitendo vya kihuni na kulinda usalama wao wenyewe na abiria.


DKT GHARIB BILAL AWASILI MKOANI KIGOMA KWA AJILI YA UZINDUZI WA KIVUKO CHA MV MALAGALASI


Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma za asili kutoka kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma, kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagalasi siku ya Ijumaa tarehe 25/10/2013  Wilayani Uvinza.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU