JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA
KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE
05/05/2013
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara
ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara
kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa
bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi
parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu
watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.
Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya
tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana
na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor
Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph
Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George
Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia
watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30)
mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem
Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika
Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha
traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia
Al-Mahri Saeed Mohseens (29)
Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na
wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen.
Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala
jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni
jijini Arusha.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya
upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na
INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini
kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo. Baada
ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao
wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama
kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati
walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao. Pia
ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor
S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji
na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea
kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenye na Uganda ambao tunashirikiana nao
katika upelelezi wa shauri hilo.
Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa
tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika
hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu
katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St.
Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini
dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.
Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea
kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili
waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi
linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa
zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine
wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari
mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs.
50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa
kukamatwa kwa watu hao. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.