Facebook Comments Box

Friday, June 28, 2013

NDEGE ZA MAREKANI ZAWASILI DAR ES SALAAM


DAR ES SALAAM.   MAKACHERO wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatar ajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu, ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Inaaminika kuwa helikopta hizo zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.
Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.
Meli za kivita na ndege ya kijeshi
Katika hatua nyingine, meli mbili za kivita ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zimeegeshwa Kigamboni.
“Jamaa wana meli kali kwa kweli, mimi nimekuwa askari wa Kikosi cha Maji kwa muda mrefu na kufanya mazoezi na mataifa kadhaa, lakini sijaona meli kama zile.


BARACK OBAMA KUPEWA PHD YA HESHIMA NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

Taarifa ambazo zinasikika zikimnukuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam zinasema ya kuwa Ocean Road itabadilishwa jina lake na kuitwa, "Barack Obama Avenue" kwa heshima ya Rais huyo wa 44 wa taifa la Marekani.

Taarifa nyingine zinasema kuwa Obama pia atatunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima na Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (OUT) kwa kutambua mchango wake katika maisha ya binadamu kwenye nyanja ya maendeleo ya kiuchumi.

Amenukuliwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwete akisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Rais Obama anatunukiwa tuzo hiyo akitanguliwa na hayati Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela na Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

OUT imeshatoa pia shahada za heshima kwa mtafiti na mtetezi wa Sokwe wa Gombe, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano bwana David Mellor.



HISPANIA YAFANYA KILICHOTAKWA NA WAPENZI WENGI WA SOKA PALE ILIPOING'OA ITALIA KWA PENATI 7-6 NA KUTINGA FAINALI

HISPANIA imeitoa Italia katika Kombe la Mabara kwa ushindi wa matuta wa 7-6 mjini Fortaleza, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo mkali wa Nusu Fainali.

Wataliano walifungwa na Waspanyola katika Fainali ya Euro mwaka jana wameshindwa kulipa kisasi na sasa Fainali ya michuano hiyo mwaka huu Jumapili Uwanja wa Maracana, itawakutanisha wenyeji Brazil na Hispania kama wapenzi wengi wa soka walivyokuwa wanataka ili waone soka ya uhakika ikichezwa ndani ya Maracana.

Leonardo Bonucci wa Italia alikosa moja ya penati yake na Jesus Navas akaweka nyavuni mkwaju wa mwisho na kuipeleka Hispania Fainali.


Close shave: Spain moved through to the Confederations Cup final after beating Italy on penalties in Fortaleza


Dramatic: Spain triumphed 7-6 in a dramatic shootout to set up a dream final against Brazil
Off target: Italy blinked first in the shout-out when Leonardo Bonucci fired over at 6-6
Decisive: Jesus Navas stepped up to score the winning penalty and send Spain to the final
Jesus Navas akiifungia Hispania Penati ya Mwisho na Kutinga Fainali ambapo watapambana na wenyeji Brazil ndani ya Uwanja wa Maracana.
Evens: The teams were locked at 0-0 after 120 minutes in the all European semi-final
Torres
Outnumbered: Italy's Giorgio Chiellini tries to win a header against Sergio Ramos and Gerard Pique
Effort: Fernando Torres attempts a shot on goal as Gianluigi Buffon watches
On the ball: Manchester City's David Silva attempts one of his elusive runs
David Silva
Held his nerve: midfielder Andres Iniesta slotted his penalty past Buffon in the Italian goal
Andres Iniesta.





ABASS MTEMVU AUNGURUMA TEMEKE


 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani katikati), akifuatwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. 
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimsikiliza Mweka Hazina wa Kikundi cha Kuweka na Kukopa (VICOBA), Anjela Ndigula ambaye alipokea sh. 50,000 alizotoa msaada kwa Muya Thabit ili ajiunge na kikundi hicho, baada ya kuambiwa hana haki hivyo anashindwa kulipia pango. Msaada huo aliutoa katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Muya Thabit akicheza kwa furaha baada Mbunge Mtemvu kumsaidia fedha za kujiunga na vicoba
 Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo, akiwazawadia fedha wasanii wa kikundi cha Msimamo

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akikizawadia fedha kikundi cha sanaa cha Msimamo kilichokuwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. Pia aliahidi kukipatia kikundi hicho sh. 500,000 za kununulia vifaa.
                  
                           Muya Thabit akiomba fedha kwa Mbunge Mtemvu ili alipe pango
                                    Wananchi wakiuliza maswali kwa Mbunge wao Mtemvu






 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU